Serikali isitishe kujenga Dodoma kwanza

Serikali isitishe kujenga Dodoma kwanza

Hali kwa Watanzania ni mbaya sana mifukoni kipindi hiki cha kupanda kwa bei za bidhaa zote na ongezeko la kodi.

Kuna miradi ambayo inaweza kusimama kwa muda hadi hapo vumbi litakapo tuwama. Kama serikali Ina nia nzuri ya kuwasaidia Watanzania kwa njia ya kubana matumizi basi mahali pa kuanzia ni kujenga Dodoma kipindi hiki.

Kila wizara ilikuwa na ofisi tayari Dar es Salaam tunaweza kuendelea na ofisi hizo kwasasa hadi hapo hali yetu itakapokuwa sawa.
Stupidity thread
 
Hivi nani kawambia kwamba hali ni mbaya kwa serikali pia? wakati wana uwezo wa kukusanya pesa nyingi kutoka kwenye matozo yao, mbali mbali ambayo haikuwekwa kwenye bajeti awali.

Hali ni mbaya tu kwa raia wa kawaida na watumushi wa chini wanao pokea mishahara bila allowances mbalimbali, disposable income yao imeshuka kwasabb ya mfumuko wa bei na tozo, kwa hiyo wana kosa megi katika maisha yao ya kila siku.

Hili la kufanya wana nchi masikini ni mpango maalumu wa CCM kama nchi nyingi Africa kuweza kufanya wananchi masikini zaidi na zaidi ili wa tawalike vzri hata wakipewa rushwa ndogo ya mchvi au kanga waweze kuwapa kura zao ili waendelee kuwatawala.( make them more poor and poorer to rule them)
Loud and clear
 
Hakuna wa kukuelewa kwenye hili. Watu wanendeleza biashara zao za kandarasi za ujenzi kwa soko bandia la ujenzi lilokuwa created hapo Dodoma kwa jina la Makao Makuu ya nchi
Uache majengo ya serikali yaliyo tayari DSM ukadurufu mengine Dodoma. Uache kukusanya kodi za pango DSM uhamie Dodoma ili uwabebeshe wananchi zigo la tozo. Ni bahati mbaya sana watu hawana hofu ya Mungu wala kujua maisha hapa duniani tuwapitaji tu. Wanafanya maaumuzi kana kwamba wataishi hapa milele yote au atakuwa Waziri maisha yake yote.
Watanzania tuache habari za kumuachia Mungu. Watu waovu kwa watu wanamtanguliza kama kichaka, hata wakoloni walitufanyia hivyohivyo wakati wanakuja kutupora. Binafsi sihudhurii mkutano wa siasa ambao unatanguliza masheikh na wachungaji, ni kupumbaza wananchi. Wabunge kama hawa hawezi kuwepo kwenye katiba, bunge na mahakama kama za Kenya.
 
Kenya
Nivugumu kubadili watanzania CCM au Nyerere ni kunyima watanzania elimu bora, yakuwafanya wa jutegemee kimawazo, 90% wa hawana elimu wengi walushia darasa la 7. la kukalilishwa na kusifia upuuzi wa watawala, CCM ili fanikiwa kwa 100% kufanya wa Tanzania kua mbumbumbu
Itatutawala huko mbele ya safari
 
Ushauri wa ajabu Sana Yani unataka Sasa mawaziri warudi dar? mnaweza simamisha iyo SGR, madaraja yasiyokua na tija maana Kuna upigaji, uza mav8, punguza posho za viongozi wenu na malupulupu, punguza mishahara ya viongozi wenu, ila makao makuu DODOMA LAZIMA Yakamilike, Yani katika yote umeona kusitisha ujenzi wa makao makuu ndo suluhu,na je hao wabunge 19 wasiokua na Chama wanafanya nini bungeni?

KWANZA napendekeza makazi ya Rais yawe rasm Dodoma ikilu ya dar ikiwezekana ivunjwe Kama Serikali imekosa matumizi mbadala, maana tumechoka daily mav8 yapo barabarani dar- Dom KWa nini? Wakati Serikali ipo Dodoma ,LAZIMA makao makuu kuisha iyo haina mbadala
Hapo kwa wabunge 19 umekosea,hata ukiwatoa hao bungeni nafasi zao zotajazwa na wengine fasta na kuendelea kula pesa. Bora waendelee kula haohao mpaka wananchi watakapokuwa serious na katiba mpya
 
Hapo kwa wabunge 19 umekosea,hata ukiwatoa hao bungeni nafasi zao zotajazwa na wengine fasta na kuendelea kula pesa. Bora waendelee kula haohao mpaka wananchi watakapokuwa serious na katiba mpya
Ziliwe na walio Halali, Sasa tangu wako pale izo pesa zinalika kihalali, si wizi tu,
 
Dawa ni kufundishana namna nzuri ya kupiga kura. Kila mtu awe tayari kudai katiba mpya inayolinda kura yake isipotee.

Njia nzuri ya kufikia huko ni machafuko tu.
 
Kama una pesa ya Bando ni wazi huna njaa..

Vijijini bando ni anasa.
Ndo maana tulioko Mjini ndo tunawatunza walioko vijijin, ukitumia bibi au ndugu yako Kijiji 40, tiyari umeongezea mzunguko wa mahali pale , ila vijijin watu pia wameelimika wengine kwao sio anasa kama tulio mjini
 
Watanzania tuache habari za kumuachia Mungu. Watu waovu kwa watu wanamtanguliza kama kichaka, hata wakoloni walitufanyia hivyohivyo wakati wanakuja kutupora. Binafsi sihudhurii mkutano wa siasa ambao unatanguliza masheikh na wachungaji, ni kupumbaza wananchi. Wabunge kama hawa hawezi kuwepo kwenye katiba, bunge na mahakama kama za Kenya.

Wewe fikiri Mtu anamuomba Mtu kunukuu mistari ya Neno la Mungu anaye muamini. Huyo mtu anaye ombwa anafanywa amkufuru Mungu pengine bila yeye kujua. Anaye omba anamdhalilisha Mungu wake bila kujua. Matendo ya Mitume 12:21-23
 
Wewe fikiri Mtu anamuomba Mtu kunukuu mistari ya Neno la Mungu anaye muamini. Huyo mtu anaye ombwa anafanywa amkufuru Mungu pengine bila yeye kujua. Anaye omba anamdhalilisha Mungu wake bila kujua. Matendo ya Mitume 12:21-23
Mtu yeyote anaetaka kukufanya punda wake atakupumbaza kwanza kwa neno la mungu, lakini wao hawaliishi neno la mungu ila wanakutaka wewe umuogope mungu. Kila kulikokuwa na ofisi za wakoloni kulikuwa na wamissionari. Sasa hivi kila waliko wanasiasa wako masheikh, mapadre na wachungaji sawa na walivyofanya wakoloni, copy and paste.
 
Natamani kusikia serikali ikisema kwasasa kutokana na hali mbaya ya uchumi, ukame, COVID-19 na kupanda kwa bidhaa tumesitisha kujenga mji wa serikali Dodoma badala yake tutajikita kwenye miradi ya mkakati kama kupeleka mawasiliano(mkongo) hadi ngazi ya kila wilaya na tarafa, maji, umeme, dawa, mikopo ya elimu hadi hapo hali ya uchumi itakapotengemaa.

Lakini sio kuendelea kujenga majengo ambayo tayari yapo dar es salaam na kwingine kwa kuongeza tozo kwa wananchi. Hebu fikiria serikali imeshakata Kodi (PAYE) kwenye mshahara wa mtumishi, halafu kile kilichobaki kilichopelekwa Benki serikali wanakivizia tena njiani wakati unakotoa Benki na kukikata tena. Ni sawa na mnunuzi wa ng'ombe aliyenunua ng'ombe wako mnadani kisha akatuma wezi wakufuate nyumannyuma wakuibie hizo hela njiani wakati ukielekea nyumbani kwako.
 
Unajua gharama ya kuwarudisha watumishi Dar es salaam??. By the way ujenzi wa Dodoma unachukua percentage ndogo sana ya bajeti ya Serikali. Ungekuwa hata umekuja na facts tu basi huenda ingesaidia kufanya judgement. Pia ujenzi wa Dodoma unaongeza pesa kwenye mzunguko na umetoa ajira kwa watu wengi wasio na elimu na wenye elimu pia
 
Unajua gharama ya kuwarudisha watumishi Dar es salaam??. By the way ujenzi wa Dodoma unachukua percentage ndogo sana ya bajeti ya Serikali. Ungekuwa hata umekuja na facts tu basi huenda ingesaidia kufanya judgement. Pia ujenzi wa Dodoma unaongeza pesa kwenye mzunguko na umetoa ajira kwa watu wengi wasio na elimu na wenye elimu pia
Kama lengo ni kuboresha mzunguuko wa fedha na ajira kwa watu tungeweza kuuongeza mzunguuko wa pesa kwenye jamii zaidi kama pesa hiyo ingetumika kuwapa wananchi wengi kazi ya kuchimba na kutandika mkongo kuelekea kwenye kata zao. Kazi hiyo ingekuwa na multiplication effect kwa taifa. Kwani watu wengi wangeweza kuhudumiwa hukohuko kwenye kata zao bila kulazimika kusafiri na kukusanyika makao makuu ya wilaya, mkoa au wizarani. Hata shule za kata zingeweza kufundishwa na walimu walioko dsm.

Tunajua kuwa kwenye miradi hiyo ya dodoma kuna maslahi ya watu. Badala ya kuipeleka serikali kwa wananchi mnatengeneza mradi wa kuikusanya serikali sehemu moja, yaani bomu likipigwa linalipua serikali yote kwa wakati mmoja. Haya ni matope sio ubongo.
 
Back
Top Bottom