Serikali isitishe kulipa mishahara watumishi walioamua kurudi tena masomoni ni upotevu mkubwa wa pesa tena wengine wanahama fani kabisa.


Msameheni huyo jua Kali mtaaani,kama anauwezo abadili Sheria za utumishi wa umma lasivyo atakuwa noise maker tu.
 
Unaroho ya Kimaskini sana! Kawaida roho za kimaskini zina wivu mkali. Na inaonekana hauna elimu kubwa na hutaki wenzako waendele wabaki kama wewe! Pole sana Kazi ya serikali ni pamoja kumfanya mtumishi wake astawi kitaaluma na kicheo.
Baki na uvivu wako wa kusoma usiroge wenzako wanaojitutumua kuongeza uthamani wao.
 
Sio uchawi ni uhalisia , kama watumishi zaidi ya elfu 5 au 10 wote wapo masomoni unadhani ni kiasi gani cha pesa kinapotea bure?

Wewe umeamua kujiendeleza basi pambana na hali yako.
Hakika kama wew utakuwa ni mtumishi utakuwa ni wale watumishi wavivu, goigoi kazini muda wote kuzunguka kufanya majungu na kusoma kwako kichwa ni kizito. Na wenzio wakirudi shule unakabwa na kijiba cha roho.........Mtumishi wa serikali anayefanya kazi kweli kweli ukiangalia maslahi/malipo yake huwa hayaendani na anachodeliver kwa hiyo huduma, hivyo kujiendeleza na kuendelea kulipwa ni haki kabisa maana bado pia ataendelea kua mtumishi.
 
SIKU HIZI WACHAWI SIO WAZEE! YULE ALIEIMBA WIMBO HUO APEWE TUZO AZAWADIWE NA PHD...nguvu hii ungeitumia kukemea mafisadi yanayochota mabilioni kwa mabilioni na kuwekeza nje ya nchi ungekuwa na akili kdg.
 
Napiga Picha kwa mfano Mtumishi wa Afya lets Say Daktari anaenda kusomea udaktari Bingwa, kwahiyo huyu daktari asitishiwe mshahara na akimaliza shule aombe kazi upya?
Huyu ni mpumbavu na ni mchawi! Qmmk!
 
Mkuu acha watu walw keki ya taifa.

Hasara hazitokai na hivi vimishahara vya laki 8 kwa mwezi.
 
"Nik wivu tu" - Rashid Gwaji Boy
 
Kuajiri mtu mpya kwenye taasisi sio jambo dogo. Hata sisi wenye biashara binafsi inatakiwa kuendeleza watu tulio nao na sio kuhangaika kutafuta watu wapya. Kimsingi ulichoandika ni ushuzi mtupu.
 
Umetumia akili gani kuandika mkuu ! Acha ubinafsi kila mtu ana nafasi ya kukua kafika kile anachokifanya!
Aliyepewa kapewa bhna
 
Hoja ni nzuri ila nadhani muktadha wake ni sio sahihi. Nitakueleza mambo kadhaa:
1. Kujiendeleza kielimu au maarifa ni sehemu moja ya msingi na muhimu sana kwa mwajiriwa pamoja na mwajiri. Nimefurahi kuona ukitoa mfano wa madaktari, hawa ni watu ambao wapo kwenye kundi la kipekee kwani wanapaswa kuongea maarifa kila uchwao! Sambamba na watu kama Laboratory technicians pamoj na Clinical Officers. Ukisema aende kusoma halafu arudi kwenye eneo lille sio sahihi, mfano, kama Clinical Officer alikuwa Maternity Ward basi tunategemea akirudi atakuwa mkuu wa idara ya LHC ili apate kutumia ujuzi wake katika kuleta maendeleo.

2. Ukiwauliza HR watakuambia kuwa kuna aina mbili za matangazo ya kazi au ajira. Kuna internal pamoja na external job posting. External huwa inatangazwa nje na mtu yoyote mwenye vigezo anaweza kuomba ila upande wa Internal huwa ni wale wenye vigezo ndani ya ofisi husika kama wanaweza kuomba. Mara kadhaa huwa ni kwa sababu mtu mmoja amestaafu au ameondoka na hawawezi kufanya process za kuajiri mtu ila wanaweza kumchukua mtu na kuziba nafasi.​

HII KITU SIO YA KUIZIMA MAANA NDO ROHO YA KAZI NYINGI SERIKALI NA KWA JAMII.
 
Huyo unahe mwelekeza ni simple mind .
 
Nadhani umetumia akili ndogo sanaa kufikiri,

Pia huna uelewa kuhusu utumishi wa umma na mamlaka zinazosimamia.

kumbuka hii ni jf sio fb, kuna viongozi wengi ila wana fake ID
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…