Serikali isiwalipe posho waliokuwa wakimsafirisha kwa gari mtoto mahututi toka Kigoma kwenda Dar es Salaam

Serikali isiwalipe posho waliokuwa wakimsafirisha kwa gari mtoto mahututi toka Kigoma kwenda Dar es Salaam

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
21,741
Reaction score
26,735
Uongozi wa mkoa na hospitali ya Maweni ulishindwa kutumia akili kabla ya kuamua mtoto aliye mahututi asafirishwe kwa gari toka Kigoma mpaka Dar es Salaam kwa ajili ya tiba iliyowashinda, walishindwa kupata ndege ya Flying Doctor au kumpeleka Mwanza!

Walizipita hospitali za Kitete Tabora, Mkapa Dodoma na wakawa na nia ya kuipita ya Morogoro na mtoto akawafia njiani mkoani Morogoro! Hiki kitendo ni cha kijinga sana.
 
Angekuwa wa familia fulani,mtoto wa mtu maarufu...angepelekwa kwa ndege na kupata michango ya kutaka sifa watu
Ila kwa sababu mtoto hyo katokea familia ya kawaida/chini watu hawana habari

Ova
 
Angekuwa wa familia fulani,mtoto wa mtu maarufu...angepelekwa kwa ndege na kupata michango ya kutaka sifa watu
Ila kwa sababu mtoto hyo katokea familia ya kawaida/chini watu hawana habari

Ova
Familia yote iliuawa yeye wa 7.
 
Bila kutaja sababu iliyowafanya hao watumishi kufanya hivyo, wote nasema mnaropoka tu.
 
Huwatendei Haki, wao wamefuata utaratibu tu. Air Ambulance ni kazi ya Wizara.
 
Nadhani waanze na uongozi ndio uliotoa order dereva aandae gari, patron aandae manesi wa kumsindikiza mgonjwa.

Hawa wahakukurupuka tu na kuondoka bila viongozi wakuu wa hospitali kutoa maelekezo.
 
Africa kuna wakati unaweza usione umuhimu wa watu kusoma....

Ushauri: zinapotekea speacial cases katika mkoa ambao hauna huduma nzuri na mgonjwa anapaswa kupelekwa Dar au Moshi KCMC kwa haraka ni vyema tu kuwe na utaratibu wa flydoctor kwa gharama za serikali.... lakini ni vyema sasa Serikali ikaboresha huduma kwenye mahospitali ya mikoa au kuwa na hospitali kubwa ya rufaa kila kanda zenye madaktari na vifaa vya kisasa.
 
Nilikuwa nasoma comment nione kama kunaatakae jali hata mmoja. Mods naombeni radhi kwa comment hii

1. Kuhusu kwenda Mwanza Bugando au Mkapa Dodoma nadhani Dokta alipima kulingana na hali ya mtoto na alijua alicho kifanya, usimuone zuzu kabisa.

2. Wakati wewe unamnyandua mke wako huko madaktari na manesi wamepambana kufa kupona kumsafirisha mtoto huyu aliyekatwa na mapanga vibaya. I know haikuwa safari rahisi kama ulivyokaa kwenye keyboard unatype... safari ya uchungu mwendo wa kasi kufa na kupona kuokoa maisha ya mtoto akafariki saa 1 kabla ya kufika muhimbili.

3. Watumishi hawa chini wanafanya kazi kama punda... mateso makali... wewe sijui ndio nyie wa wizarani huko mnao toaga maagizo kama MCD...

4. Binafsi nimewaza ipo umuhimu kuimalisha hospitali za kanda na mikoa. Kuliko kushikilia huo mzero iq harafu unaandika comment za kuwatukana punda wenzetu hao.

5. Chukueni posho... posho ya damu na uchungu japo najua hata hamtaweza kununulia kilo ya nyama kwa kumbukumbu ngumu ya usiku wa Giza la mauti
 
Kutowalipa hao uliosema ni uonevu wa hali ya juu.

Huenda hao waliomsafirisha ni machalii wenye diploma tu walionza kazi mwaka jana tu, hawana expirience, hawana sauti kwa wakubwa wao, wanafuata kile mamlaka imesema.

Wa kuadabishwa hapo ni kuanzia mkuu wa mkoa, hao digidigi wanaofata maelekezo huo uwezo wa kupata hiyo ndege mpaka dar wanautoa wap? Achilia mbali kuipata hata tu kuiona usikute hawajawahi, halafu uwahukumu kwa kutopata ndege mbona u muonevu sana mtu wewe.
 
Uongozi wa mkoa na hospitali ya Maweni ulishindwa kutumia akili kabla ya kuamua mtoto aliye mahututi asafirishwe kwa gari toka Kigoma mpaka Dar es Salaam kwa ajili ya tiba iliyowashinda, walishindwa kupata ndege ya Flying Doctor au kumpeleka Mwanza!

Walizipita hospitali za Kitete Tabora, Mkapa Morogoro na wakawa na nia ya kuipita ya Morogoro na mtoto akawafia njiani mkoani Morogoro! Hiki kitendo ni cha kijinga sana.
We ulishawahi panda hiyo ndege,ndege sio bajaj
 
Ndio utajua tulivyo wabinafsi.
Hao waliomsafirisha yawezakawa walitoa ushauri mkubwa tu juu ya jambo husika ila bila kujali watu wakajipangia cha kufanya.

Wewe ingia kwa Cruiser..huyo atafika tu kwa mipango ya Mungu Muhimbili.

Siwezi kuwalaumu hao waliokuwa kwa Ambulance kumsafirisha.

Nani alihusika kutoa maamuzi ya kubahatisha kiasi hicho?
Kwa muda waliotumia hao ,je nini kilishindikana kwenda Bugando na kama lengo lilikuwa uhai.Hao Madaktari Bingwa walishindwa kusafirishwa kwa dhararua kuokoa uhai wa Mtoto?

Ubinafsi na mawazo mgando kwa baadhi ya watu wenye nyazifa huko kwenye maamuzi.

Waliohusika kufanya maamuzi wana la kujibu mioyoni mwao.
 
Back
Top Bottom