Serikali itenge fedha ya dharura kukabili changamoto za elimu bure

Modest84

New Member
Joined
Aug 3, 2022
Posts
2
Reaction score
1
FEDHA YA DHARURA ITENGWE HARAKA KUOKOA ELIMU NCHINI🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿

✍️Mwl. Modest Alphonce

(Mwandishi wa Makala hii ni mwalimu wa Sekondari, mwalimu wa Taaluma Mwandamizi na Mjumbe wa Kamati ya Shule ya Msingi iliyopo jijini Dsm)

Wakati shule wanazosoma watoto wa watunga Sera hapa nchini zikizidi kupanda gharaza za ada na michango kuongezeka ili kukidhi maboresho ya Elimu inayotolewa katika shule hizo, shule za Umma zimeondolewa ada katika ngazi zote za Elimu msingi (yaani Elimu ya lazima) huku shule hizi zikizidi kulemewa na changamoto lukuki zinazokwamisha utoaji wa Elimu kwa ufanisi kwa watoto wetu.

Utekelezaji wa Sera ya Elimu Bure hapa nchini umekuwa na changomoto sana kwa sababu serikali inashindwa kupeleka fedha za kutosha kwenye mashule ili kukabiliana na changamoto zilizopo. Wakati huo huo siasa za nchi yetu zimewajengea wazazi ukuta ambao unawatenga na mazingira ya shuleni kwa kuwaondolea wazazi wajibu wa kushiriki katika utatuzi wa changamoto za mashuleni.

Upigaji marufuku michango mashuleni na kuweka sheria ngumu za ushiriki wa wazazi katika uchangiaji fedha ili kutatua changamoto mashuleni zimezifanya shule kuwa na mazingira magumu sana ya kuweza kutoa Elimu Bora.

Hivi sasa shule nyingi sana za Umma zinakabiliwa na upungufu mkubwa sana wa madawati, mfano katika shule yangu ya sekondari tuna upungufu wa meza na viti kwa wanafunzi 100 jambo ambalo linatuwia vigumu tutekeleza majukumu yetu ya ufundishaji kwa ufanisi. Kazi huwa ngumu zaidi wakati wa ufanyaji mitihani jambo ambalo hutulazimu kuahirisha mitihani kwa baadhi ya madarasa ili kupisha baadhi waanze kwanza kufanya mitihani huku wengine wakisubiri zamu yao nje.

Shule ya msingi ambayo mimi ni mjumbe wa Kamati ya Shule kwa muda wa zaidi ya mitano sasa haina vyoo vya wanafunzi wa kiume huki ikiwalazimu watoto hao zaidi ya 700 kujisaidia katika shule ya jirani ambayo nayo ina matundu 4 tu huki ikiwa na watoto wa kiume zaidi ya 800. Vyoo vya wasichana vipo lakini havitoshelezi, matundu yaliyopo huweza kumudu nusu tu ya wasichana waliopo. Pamoja na uwepo wa vyoo vichache kwa baadhi ya shule bado mazingira na miundombinu ya vyoo hivyo ipo katika hatari kubwa sana kiafya kwani vingi havina kabisa miundombinu ya maji safi.

Vile vile licha ya shule hii kuwepo mjini lakini nayo inakabiliwa na upungufu mkubwa wa madawati huku sakafu za vyumba vingi vya madarasa vikiwa na mashimo makubwa.

Vile vile shule nyingi licha kuwa ni za muda mrefu lakini bado hazijaweza kuwa na majengo ya utawala yaani ofisi za walimu. Kuna shule zina zaidi ya miaka 10 hadi kumi 15 lakini hata ofisi ya Mwalimu Mkuu hazijafanikiwa kujengewa.

Kila mara juhudi za kuwashirikisha wananchi katika utatuzi wa changamoto hizi zinakwama kwa sababu ya vitisho vya siasa na dhana potofu ya Elimu Bure iliyojengwa vichwani mwa wazazi na wanasiasa watunga Sera ambao kimsingi athari za utekelezaji wa kile walichokitunga haziwagusi kwa namna yoyote ile.

SULUHISHO

Sera ya Elimu Bure kwa maana halisi ya Elimu Bure ni jambo jema kwa ustawi wa nchi yetu hasa kwa wananchi wa hali ya chini lakini kwa hali hii iliyopo katika shule zetu Elimu Bure inakuwa haina maana wakati tuna akili na nguvu za kifedha sisi kama jamii kuweza kuboresha mazingira na miuondombinu ya mazingira ya shule kwa ajili ya Elimu ya watoto wetu.

Aidha Serikali itenge haraka fedha ya dharura kwa ajili ya kuzikabili changamoto hizi za Elimu ikiwa ni pamoja na kuanzisha kambi maalumu za upasuaji mbao na kutengeneza madawa, meza na viti vya kutosha kwa kuzingatia sera na mpango wa Maendeleo Endelevu, na kutumia njia zingine mwafaka kutokana na mapendekezo ya wataalamu

Au, sisi wananchi tupewe dhamana na mamlaka ya kuendesha shule zetu kwa ngazi ya jamii ili kwa maamuzi ya pamoja tuzishughulikie changamoto hizo kwa kipindi kifupi sana, PESA TUNAZO, NIA, UTASHI NA UWEZO wa kusimamia utekelezaji wa haya yote.

#ModestAlphonce
0747792984
 
Attachments

  • FB_IMG_1659788458647.jpg
    FB_IMG_1659788458647.jpg
    34.5 KB · Views: 8
Nchi hii ngumu sana ndugu yangu na hii inasababishwa na Wananchi wenyewe ambao hawajielewi wala kujitambua, hawajui wajibu wao wala haki zao ilimradi tu wanapata ugali wao basii. Hivyo wewe kuwasemea ni kujichosha bure tu.

Aliyesema michango holela mashuleni marufuku, Yeye anamlipia mtoto wake 12M shule binafsi. Ili aje kuwaongoza hawa st kayumba kidumu na fagio, matundu 4 ya vyoo watoto 800 ambao wazazi wao walifurahi sana kusikia maneno Yale.

Inauma ila hakuna namna labla tusubiri miaka 50 ijayo ndio tutapata kizazi kama kile cha marekani.

Mwisho ila sio kwa umuhimu, mashuleni huko kuna shida nyingi mno VYOO, MADAWATI, WALIMU, MAJENGO NK, sio kwamba hawajui wanajua ila HAIWADHURU KWA CHOCHOTE KILE
 
FEDHA YA DHARURA ITENGWE HARAKA KUOKOA ELIMU NCHINI[emoji1241][emoji1241][emoji1241][emoji1241][emoji1241]

[emoji3578]Mwl. Modest Alphonce

(Mwandishi wa Makala hii ni mwalimu wa Sekondari, mwalimu wa Taaluma Mwandamizi na Mjumbe wa Kamati ya Shule ya Msingi iliyopo jijini Dsm)

Wakati shule wanazosoma watoto wa watunga Sera hapa nchini zikizidi kupanda gharaza za ada na michango kuongezeka ili kukidhi maboresho ya Elimu inayotolewa katika shule hizo, shule za Umma zimeondolewa ada katika ngazi zote za Elimu msingi (yaani Elimu ya lazima) huku shule hizi zikizidi kulemewa na changamoto lukuki zinazokwamisha utoaji wa Elimu kwa ufanisi kwa watoto wetu.

Utekelezaji wa Sera ya Elimu Bure hapa nchini umekuwa na changomoto sana kwa sababu serikali inashindwa kupeleka fedha za kutosha kwenye mashule ili kukabiliana na changamoto zilizopo. Wakati huo huo siasa za nchi yetu zimewajengea wazazi ukuta ambao unawatenga na mazingira ya shuleni kwa kuwaondolea wazazi wajibu wa kushiriki katika utatuzi wa changamoto za mashuleni.

Upigaji marufuku michango mashuleni na kuweka sheria ngumu za ushiriki wa wazazi katika uchangiaji fedha ili kutatua changamoto mashuleni zimezifanya shule kuwa na mazingira magumu sana ya kuweza kutoa Elimu Bora.

Hivi sasa shule nyingi sana za Umma zinakabiliwa na upungufu mkubwa sana wa madawati, mfano katika shule yangu ya sekondari tuna upungufu wa meza na viti kwa wanafunzi 100 jambo ambalo linatuwia vigumu tutekeleza majukumu yetu ya ufundishaji kwa ufanisi. Kazi huwa ngumu zaidi wakati wa ufanyaji mitihani jambo ambalo hutulazimu kuahirisha mitihani kwa baadhi ya madarasa ili kupisha baadhi waanze kwanza kufanya mitihani huku wengine wakisubiri zamu yao nje.

Shule ya msingi ambayo mimi ni mjumbe wa Kamati ya Shule kwa muda wa zaidi ya mitano sasa haina vyoo vya wanafunzi wa kiume huki ikiwalazimu watoto hao zaidi ya 700 kujisaidia katika shule ya jirani ambayo nayo ina matundu 4 tu huki ikiwa na watoto wa kiume zaidi ya 800. Vyoo vya wasichana vipo lakini havitoshelezi, matundu yaliyopo huweza kumudu nusu tu ya wasichana waliopo. Pamoja na uwepo wa vyoo vichache kwa baadhi ya shule bado mazingira na miundombinu ya vyoo hivyo ipo katika hatari kubwa sana kiafya kwani vingi havina kabisa miundombinu ya maji safi.

Vile vile licha ya shule hii kuwepo mjini lakini nayo inakabiliwa na upungufu mkubwa wa madawati huku sakafu za vyumba vingi vya madarasa vikiwa na mashimo makubwa.

Vile vile shule nyingi licha kuwa ni za muda mrefu lakini bado hazijaweza kuwa na majengo ya utawala yaani ofisi za walimu. Kuna shule zina zaidi ya miaka 10 hadi kumi 15 lakini hata ofisi ya Mwalimu Mkuu hazijafanikiwa kujengewa.

Kila mara juhudi za kuwashirikisha wananchi katika utatuzi wa changamoto hizi zinakwama kwa sababu ya vitisho vya siasa na dhana potofu ya Elimu Bure iliyojengwa vichwani mwa wazazi na wanasiasa watunga Sera ambao kimsingi athari za utekelezaji wa kile walichokitunga haziwagusi kwa namna yoyote ile.

SULUHISHO

Sera ya Elimu Bure kwa maana halisi ya Elimu Bure ni jambo jema kwa ustawi wa nchi yetu hasa kwa wananchi wa hali ya chini lakini kwa hali hii iliyopo katika shule zetu Elimu Bure inakuwa haina maana wakati tuna akili na nguvu za kifedha sisi kama jamii kuweza kuboresha mazingira na miuondombinu ya mazingira ya shule kwa ajili ya Elimu ya watoto wetu.

Aidha Serikali itenge haraka fedha ya dharura kwa ajili ya kuzikabili changamoto hizi za Elimu ikiwa ni pamoja na kuanzisha kambi maalumu za upasuaji mbao na kutengeneza madawa, meza na viti vya kutosha kwa kuzingatia sera na mpango wa Maendeleo Endelevu, na kutumia njia zingine mwafaka kutokana na mapendekezo ya wataalamu

Au, sisi wananchi tupewe dhamana na mamlaka ya kuendesha shule zetu kwa ngazi ya jamii ili kwa maamuzi ya pamoja tuzishughulikie changamoto hizo kwa kipindi kifupi sana, PESA TUNAZO, NIA, UTASHI NA UWEZO wa kusimamia utekelezaji wa haya yote.

#ModestAlphonce
0747792984
Mwalimu umeeleweka, Sasa namba ya simu ya kazi gani!
 
Back
Top Bottom