Serikali itoe maelekezo ya fedha za uchaguzi zilizobaki kwenye Halmashauri, naona huku vimeanza

Serikali itoe maelekezo ya fedha za uchaguzi zilizobaki kwenye Halmashauri, naona huku vimeanza

ibesa mau

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2015
Posts
2,109
Reaction score
1,707
Kwanza nawashukuru wananchi na wasimamizi kwa namna moja au nyingine walioshiriki kuokoa fedha hizi. Nitakuwa mchoyo wa fadhira nisiposema asante

Halmashauri zilipokea fedha nyingi kwa ajiri ya uendeshaji wa uchaguzi, karibu halmashauri zote zimetumia nusu tu ya fedha zilizopelekwa, kwa sababu kati ya shughuri 6 zilipangwa kufanywa na OR_TAMISEMI ni shughuri tatu tu ndio zilizofanyika ambazo ni uandikishaji wa wapiga kura , uteuzi na mafunzo kwa maafisa waandikishaji na uteuzi wa wagombea. Na shughuri ambazo zilikuwa bado kufanyika ni kampeni za uchaguzi, uteuzi na mafunzo kwa wasimamizi wa vituo, upigaji wa kura na utoaji wa matokeo.

Halmashauri nyingi zimebaki na fedha zaidi ya milioni mia na halmashauri zenye idadi kubwa ya vituo vya kupigia kura wamebaki na zaidi ya milioni 300 hadi mia 400 na kuendelea.

Nashauri tamisemi fedha hizi itoe tamko na ibadilishe matumizi kwa kuelekeza kwenye miradi ya maendeleo iliyopo kwenye Halmashauri au izichukue na kuzipeleka kwenye mfuko mkuu wa serikali ikafadhiri miradi mikubwa inayoendelea kama ujenzi wa hospitali, vituo vya Afya, majengo ya utawala kwenye halmashauri mpya na zile zilizo hamishwa juzi kwenye maeneo yao ya utawala,SGR n.k

Nimetoa wazo hilo kwa sababu ya uzoefu wa hizo LGAs wataanza vikao vya usiku vya wakurugenzi na wasimamizi wa uchaguzi waback date shughuri na kuanza kulipana posho wakidai hizo kazi zilifanyika huko nyuma kumbe ni uongo na uwizi tu. Watu watajifanya walishandaa ballot paper kumbe ni mbinu tu za kutoa ela kwa wazabuni.

Nimetoa hilo wazo mamlaka zinazohusika zifanye maamuzi kwa sababu wapo viongozi ambao hawaogopi fedha za umma na kwa sababu karibu halmashauri zote zimeshatangaza waombaji wa nafasi mbalimbali kuwa ni washindi wa nafasi walizoomba. Hivyo hakuna shughuri yoyote itakayofanyika kuanzia kesho na kuendelea.

Mzalendo niliyebakia
 
Back
Top Bottom