Serikali itoe pesa za kujikimu kwa Walimu wapya

Serikali itoe pesa za kujikimu kwa Walimu wapya

Komando tamimy

Senior Member
Joined
Nov 18, 2020
Posts
108
Reaction score
121
Serikali itoe pesa za kujikimu kwa walimu kwani mlolongo umekuwa mrefu sana haijulikani ni lini pesa hiyo itatolewa. Nakumbuka siku katibu mkuu tamisemi anatangaza halmashauri zitakazowapokea walimu ziwe zimejiandaaa katika mapokezi ya wafanyakazi hao wapya.

Lakini cha ajabu karibia hslmashauri nyingi hazijawapa pesa za kujikimu waaalimu. Mfano mtwara mjini na mbinga mji ni baadhi ya maeneo waalimu hawajapata pesa ya kujikimu.

Maeneo ni mengi hatujui tatizo nini watuambie ukweli basi turudi nyumbani mpaka hapo watakapo jipanga kulala kwenye godauni za korosho na store za mahindi ni aibu kwa serikali pia ni aibu kwa mtumidhi wa umma.

Serikali itoepesa pesa ya kujikimu tukapange basi kama imeshindwa iwaingize kwenye mfumo wa malipo (payroll).
 
Hoja ya kuajiri walimu ilikuwa ya Mhe. Lissu wakati wa kampeni. Kwa aibu, serikali ikaidandia wakati haimo kwenye ilani ya ccm na haikujipanga kwa mwaka huu 2020/2021. Matokeo yake kila kitu ni hovyoo tangu mchakato wa kuwapata walimu wapya mpaka kupokelewa vituoni.
 
Wengi wamerudi makwao..sasa mkipewa fedha za kujikim pamoja na mshahara mnaeza msirudi mashulen mkafanya hizo hela ni mtaji.
 
Hoja ya kuajiri walimu ilikuwa ya Mhe. Lissu wakati wa kampeni. Kwa aibu, serikali ikaidandia wakati haimo kwenye ilani ya ccm na haikujipanga kwa mwaka
huu. Matokeo yake kila kitu ni hovyoo tangu mchakato wa kuwapata walimu wapya mpaka kupokelewa vituoni.
Ni vizuri lakini ingesema lini pesa za kujikimu zitakuwa tayari ili watu warudi mtu ametoka songea ameripoti bukoba mtu hyu hawezi kurudi nyumbani lazima asubiri mpaka wafungue wakati anasubiri anaishije ndani ya mwezi huu.kupata kazi ni furaha lakini wakati mwingine huwa inageuka na kuwa mateso
 
Ndio tatizo la watanzania nikuombeana matatizo nimechoka kulala store
Walimu ndio mnaliangamiza sana hili taifa, MCC inawatumia sana walimu kipind cha uchaguz
Nyie inabidi muisome namba za kila aina. Na hakuna rangi mtaacha kuziona
 
Ngoja wamalize kula K zao zilizoajiriwa kupitia mgongo wa shida wakishiba akina Paulo na silla mtaiona neema.
 
Pesa inajenga SGR na Kigongo -Busisi huko ndio muhimu zaidi kwasasa, nyie endeleeni tu kulala kwenye magodown ya korosho kwa miaka mitatu ijayo hiyo miradi itakuwa imeshakamilika.

Anyway, kuna zile posho za uchaguzi ukifika, 2025 mtapewa.
 
Tunakusanya pesa kwanza, tukiwa tayari tutaangalia kipi cha kuanza nacho...

Cc: mahondaw
 
Nadhani kuna mtazamo sio sahihi tunasema fedha (money)

Mtazamo yetu ifike mahali tuone na tupembue haya

Money as an outcome

Money as an output and,

Money as a product

Hela sio kila kitu kama wengi tunavyoaamini
 
Serikali itoe pesa za kujikimu kwa walimu kwani mlolongo umekuwa mrefu sana haijulikani ni lini pesa hiyo itatolewa. Nakumbuka siku katibu mkuu tamisemi anatangaza halmashauri zitakazowapokea walimu ziwe zimejiandaaa katika mapokezi ya wafanyakazi hao wapya.

Lakini cha ajabu karibia hslmashauri nyingi hazijawapa pesa za kujikimu waaalimu. Mfano mtwara mjini na mbinga mji ni baadhi ya maeneo waalimu hawajapata pesa ya kujikimu.

Maeneo ni mengi hatujui tatizo nini watuambie ukweli basi turudi nyumbani mpaka hapo watakapo jipanga kulala kwenye godauni za korosho na store za mahindi ni aibu kwa serikali pia ni aibu kwa mtumidhi wa umma.

Serikali itoepesa pesa ya kujikimu tukapange basi kama imeshindwa iwaingize kwenye mfumo wa malipo (payroll).
Kuna wakati unajuta kupata ajira maana si kwa mateso haya tunayopitia. yaani ni shida mtu unakaa hata hujui lini utapata mshahara Wala pesa ya kujikimu Ni mwezi Sasa watu tunakomaa lakini hakuna hata dalili za kupata pesa.
 
Back
Top Bottom