Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Labda ungemuuliza DED, pengine atakuwa na majibu.Tangu 01/11/2022 hadi sasa (28/12/2022) takribani miezi miwili serikali imeshindwa kupeleka fedha mashuleni kwa ajili ya ruzuku, na hakuna tamko lolote kutoka katika mamlaka husika.
Kushindwa kupeleka fedha hizo kwa wakati mashuleni kuna sababisha walimu kushindwa kupatiwa vifaa vya maandalizi ya kufundishia na kujifunzia shuleni.
Aidha adha hii pia inasababisha shule nyingi kuwa na mrundikano wa madeni kwa wazabuni kwani baadhi ya shule hukopa vifaa na kushindwa kulipa kwa wakati kutokana na kutoingizwa fedha hizo kwa wakati!
Rai yangu ninaishauri serikali itoe tamko ili kuondoa sintofahamu iliyopo kwa sasa kwani kukaa kimya kunazua tafsiri hasi hususani kwa wadau was Elimu.