KERO Serikali itufikirie Wahandisi wa Halmashauri tunalipwa mishahara midogo tofauti na kada nyingine

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kwa tanzania huo ni mshahara mkubwa sana.. wtz wachache sanaaaaa wanaweza kutengeneza mil 3 ndani ya mwez mmoja.
Mjifunze kuwa na shukrani
Hapo huo mshahara PAYE yake nizaidi ya laki 8, bado NSSF, bado bima ya afya hapo hujaweka bodi ya mkopo kwa wanaodaiwa. Take home hapo nipungufu ya mil 2.1, tungesema iyo pesa ni nyingi kama hio 3 or 3.5 ingekua baada ya makato lkn kama ni kabla ya makato bado ni ndogo.
 
1. Nakushauri uwe na taarifa sahihi kabla ya kuweka maoni yako kwenye hilo eneo.

2. Kodi au hiyo PAYE haifiki hata laki 4
3. Kama anadaiwa na bodi ya mikopo unatakiwa kuelewa deni lake litakuwa linazidi kupungua kadri anavyolipa.

4. Watumishi wa umma hawachangii kupitia NSSF bali PSSSF. NSSF ni kwa walio sekta binafsi.
 
Kabisa ,watu wanaona figure tu mshahara gross 2.3m kumbe wakilima makato anabakiwa na net ya 1.5m ,Engineers wa Sector binafsi wanakula wengine hadi 8m net kwa hao juniors ila kwa maseniors wanacheza hadi 20m.

Faida ya kufanya kazi serikalini ni moja tu mikopo ya uhakika ,kusoma ,safari ,warsha ,makongamano ,semina ,perdiem na uhakika wa kazi hadi unastaafu ila kwenye salary ni "PENENGE".
 
Mshahara unaozidi TZS 1,000,000: Unakatwa TZS 128,000 jumlisha asilimia 30 ya kiasi kinachozidi TZS 1,000,000.

Haifiki vipi laki nne mkuu PAYE?.
 
Mm kama mtanganyika nasema hapana kuongeza salary kwenu na pia hao agency wapunguze salary zao. Kwa hoja ya Ujenzi n usimamizi wenu kwenye barabara na majengo ni ovyo kama sio takataka bombei.
Yani unakutana na barabara imejengwa mwaka huo huo na kufa mwaka huo huo. Na bado mnataka kulipwa kwa kushindana na sio kushindana kwa kazi nzr. Hii inakela mno kwa wananchi mpk hv kweli kuna mainginia uko halimashauri?. Au nyie amuoni?Kuna mkuu w mkoa mmoja alikua anazindua shule cku iyo iyo kitasa kinakatika. Kweli!!
Kazi ni kipimo cha utu
 
Mganga mkuu wa wilaya[DMO],Afisa elimu wilaya msingi,Afisa elimu wilaya Sec,Afisa kilimo wilaya,Afisa mifugo wilaya,Afisa Ardhi wilaya,Afisa Utumishi wilaya...wengine siwakumbuki vizuri..Hao ndo wanalamba Leaders salary scale[LSS]
Aisee
 
Hao ndo wakuu wa Idara mzee,DMO ni Boss kule idara ya Afya..anasimamia masuala yote ya Afya kuanzia Hosp ya wilaya,vituo vya Afya Mpaka zahanati..

Hao wakuu wa Idara,wanateuliwa na Tamisemi...so mnaletewa tu kama ilivyo kwa wakuu wa wilaya..isipo kuwa wakuu wa Idara wao wana elimu husika ya Idara anayo simamia. Mfano DMO ni Medical Doctor by profession.
 
Mganga mkuu wa wilaya[DMO],Afisa elimu wilaya msingi,Afisa elimu wilaya Sec,Afisa kilimo wilaya,Afisa mifugo wilaya,Afisa Ardhi wilaya,Afisa Utumishi wilaya...wengine siwakumbuki vizuri..Hao ndo wanalamba Leaders salary scale[LSS]
Bado salary Ndogo, wanazidiwa na Senior engineer I wa Tarura
 
Mganga mkuu wa wilaya[DMO],Afisa elimu wilaya msingi,Afisa elimu wilaya Sec,Afisa kilimo wilaya,Afisa mifugo wilaya,Afisa Ardhi wilaya,Afisa Utumishi wilaya...wengine siwakumbuki vizuri..Hao ndo wanalamba Leaders salary scale[LSS]
Afisa biashara wilaya
Afisa michezo wilaya
Afisa usalama wilaya
Afisa ugavi wilaya
Afisa tehama wilaya
Afisa afisa afisa
 
Ni haki yenu kulipwa hiyo Mishahara mkuu, sisi wahandisi huwa tunafungua Makampuni yetu ya kihandisi

Kama umesoma ule uhandisi urahisi wa Civil Engineering - huu tunaoiita Uhandisi wa Kimama ambao ndiyo rahisi kuliko zote Duniani unastahili mshahara huo, toshekeni na mishahara yenu

Karibu kwenye Uhandisi niliousomea tupige hela, Miradi kama yote
 
Kwa huu uandishi huwezi kuwa mhandisi. Itaje hiyo engineering yako unayoiona ni bora kuliko Civil.
 
Engineer. wa halmashauri jau; kwenye mipango miji/mitaa mnatuangusha sana,hasa kwenye kukabiliaba na tatizo la wamachinga na vibanda/meza/mikeka ya biashara kando ya barabara kuu mijini.
Fanyeni ubunifu ndio niwatetee kuhusu kuongezwa mishahara, vinginevyo mpunguziwe hata hiyo mnayopata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…