Ukweli ni kwamba, kuna departure kubwa sana kwenye mishahara kwa kada moja katika maeneo mbali mbali serikali. Kwa ujumla, watumishi wa serikali kuu na serikali za mitaa ndio wenye mishahara midogo kuliko wengine walioko kwenye taasisi. Tena hapo mleta mada hujachungulia engineers walipo kwenye neema kama TPDC, TCRA, REA etc.
Hawa wa serikali kuu kwa maana ya mawizara wao advantage yao ni angalu kuna posho na safari hapa na pale na miradi mingi ya wafadhili huwa inaanzia wizarani kwa hiyo wao pamoja na mishara midogo ila bado wanakua wako vizuri.
Serikali imejaribu mara kadhaa kufanyia kazi suala hili la kuwianisha mishahara ila nadhani changamoto zimekua nyingi ikiwemo limitation kwenye wage bill ya serikali na pia tija inatofautiana.
Swali ni je, serikali ikiamua kuwianisha mishahara kwa kuwapunguzia mishahara wahandisi waliopo kwenye taasisi ili ilingane na wale wa Halmashauri, itakusaidiaje mkuu kuendesha maisha yako ya kila siku?