KERO Serikali itufikirie Wahandisi wa Halmashauri tunalipwa mishahara midogo tofauti na kada nyingine

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kwa huu uandishi huwezi kuwa mhandisi. Itaje hiyo engineering yako unayoiona ni bora kuliko Civil.
Petrology Engineering - Combination of Petroleum & Geological Engineering ....hii haitolewi Bongo Mkuu
 
Sensitive ya taasisi ina matter pia,

It's about what you bring to the table

Mhandisi yupo Ewura Kwenye regulatory body ambayo ethics ni muhimu Sana unamlipaje hela Sawa na Consumer wa halimshauri?
 
Petrology Engineering - Combination of Petroleum & Geological Engineering ....hii haitolewi Bongo Mkuu
Kwa hiyo Geology unalinganisha na Civil engineering?. Civil engineering is about designing and building infrastructure(barabara,majengo,madaraja,water supply n.k). Haya hiyo engineering yako inahusika na nini?
 

Ukweli ni kwamba, kuna departure kubwa sana kwenye mishahara kwa kada moja katika maeneo mbali mbali serikali. Kwa ujumla, watumishi wa serikali kuu na serikali za mitaa ndio wenye mishahara midogo kuliko wengine walioko kwenye taasisi. Tena hapo mleta mada hujachungulia engineers walipo kwenye neema kama TPDC, TCRA, REA etc.

Hawa wa serikali kuu kwa maana ya mawizara wao advantage yao ni angalu kuna posho na safari hapa na pale na miradi mingi ya wafadhili huwa inaanzia wizarani kwa hiyo wao pamoja na mishara midogo ila bado wanakua wako vizuri.

Serikali imejaribu mara kadhaa kufanyia kazi suala hili la kuwianisha mishahara ila nadhani changamoto zimekua nyingi ikiwemo limitation kwenye wage bill ya serikali na pia tija inatofautiana.

Swali ni je, serikali ikiamua kuwianisha mishahara kwa kuwapunguzia mishahara wahandisi waliopo kwenye taasisi ili ilingane na wale wa Halmashauri, itakusaidiaje mkuu kuendesha maisha yako ya kila siku?​
 
Magufuli alishindwa kabisa hilo suala ...Kikubwa jamaa atafute transfer kwenda huko kwenye mishahara mikubwa .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…