Unataka wakose afutatu za kubrashia?
Gari za masafa marefu(Dar -Mwanza, Mbeya, Kagera, Mara, Tunduma n.k) kila siku lazima zipoteze sio chini ya 30k kwa kuwalipa matrafiki.
Hili nimeliona mara kadhaa baada kukaa kwenye kigodoro nikipanda gari hizo. Konda kila akiona anakaribia kijiwe cha hao jamaa, anakunja elfu 5 kwenye kikaratasi, akifika anashuka fasta anasalimiana naye chini mbele ya gari, sekunde 5 tu gari inasepa.
Kuna trafiki pale Mtumbatu kuelekea Gairo walikuwa wanawake 3, bila aibu ya kike wakachukua buku 5 wakiwa wamekaza sura kabisa.
Rushwa haiwezi kuisha nchi hii hata kama sheria ngumu na kali kiasi gani zitungwe hii ni kutokana na wasimamizi wa sheria ndio vinara wa Rushwa