Serikali itunge Sheria ili mahojiano kati ya trafiki na dereva yafanyike huku abiria wakisikia Kila kitu. Kama inataka kufuta rushwa Kwa trafiki

magari mengi hayakosi makosa madogo madogo, sasa ipi Nafuu, umpe buku ya kubrashia viatu uondoke zako au ukatiwe mkeka wa elf 30 uje utoe povu huku na unajua kabisa una makosa
 
Kwa nadharia inawezekana ila si kwa vitendo na si kwa askari tu mambo mengi waliokua wanaamua viongozi wetu mengi kwa nadharia ya darasani yana wezekana ila c ku'apply uswahilini! Kifupi haiwezekani
 
Unawazo nzuri lakini kabla hatujafikia huko ujue matrafiki wenyewe wanawahurumia hapo madereva na makondakta angalao nao wapate mboga ya watoto. Ok Sasa traffic anyooshe ruler mbele ya abiria,, kosa la kwanza mbona umesimamisha abiria hapo Kuna faini mjue, mbona hujavaa uniform, speed, uchakavu wa gari( iwe kioo cha mbele kina alama ya mpasuko tu ukumbuke ni kosa, tairi lishanza ukipara ni kosa), na Mambo mengine mengi tu. Madereva sio wajinga kuunga umoja nao.
 
Trafiki wamekuwa wasumbufu na wababaishaji sana. Na mbaya wanaonea sana watu. Mpaka nashangaa kuna nini kinaendelea.
Hawana wanalofanya. Mbona ajari zinaendelea kuongezeka? Bora hata walivyopotea
 
kila nimuonapo polisi huwa naamini nimemuona binadamu asiye na akili timamu. pigia mstari akili timamu
 
tutawaua njaa ma-trafic wetu na kazi wataiona chungu; tuwaache maana maisha yatakuwa magumu kwao - 1.2m kwa mwezi una familia ya watu 6 home utakimbia mji. 😀
Kwa hiyo turuhusu rushwa Kwa polis? Waalimu je? Manesi na daktari je? Watumishi wengine wengi wanaolipwa kima cha chini je?
 
Hii mbinu imesaidia kweli?
 
Mimi nlijuwa mleta mada,anaomba serikali itambue rushwa rasmi [emoji1]

Traffic wenyewe wanatumwa na wakubwa zao kukusanya hela

Ova
Hebu jaribu kutoa mfano wa maisha ambayo rushwa imerasimishwa yanaweza kuwaje
 
magari mengi hayakosi makosa madogo madogo, sasa ipi Nafuu, umpe buku ya kubrashia viatu uondoke zako au ukatiwe mkeka wa elf 30 uje utoe povu huku na unajua kabisa una makosa
Ninachotaka mimi Sheria zifuatwe gari likiwa na dosari lisiruhusiwe kutembea barabarani. Maana vigezo vya gari kuwa complete viliwekwa ili kuwalinda watu na madhara yatokanayo na hayo mapungufu.
Kuleta huruma kwenye mambo ya kitaalamu ni kujihatarisha kinachotakiwa ni kuizuia rushwa
 
Kawaida gari ya abiria inaposimamishwa na polisi, anatakiwa aingie ndani , asalimie abiria na aeleze sababu za kusimamisha gari. Mf. Kama dereva hana leseni abiria wajulishwe!
 
Kawaida gari ya abiria inaposimamishwa na polisi, anatakiwa aingie ndani , asalimie abiria na aeleze sababu za kusimamisha gari. Mf. Kama dereva hana leseni abiria wajulishwe!
Asante sana Kwa ufafanuzi mzuri mbona sasa traffic wetu hawafanyi hivyo kabisa? Nani wa kuwawajibisha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…