Serikali itunge sheria kuhusu uzazi wa mpango angalau watoto wawili kila familia maana kasi ya uzazi Tanzania inatisha

Na cheap labour yenye akili ya ubunifu sio ya kindezi kama sisi.
 
Mjini na vijijini ni wapi kuna maisha duni na chakula cha shida?
Unaongea kw takwimu rasmi au kwa story za vijiweni?
 
Kwa hizi akili za wanyonge zilizoharibiwa na mwendazake ni serikali gani itafanya hivyo ikaeleweka?😂😂
Itakua balaa
 
Kanda ipi hiyo, kanda ya ziwa?
 
Tz Bado watu hawana elimu ya kujua athari za popln kubwa! Kukiwa na mapori ndiyo sababu ya kuzaa kama mbwa twitu? Kanda ya ziwa mama 1 anazaa watoto 17 kweli ni haki/halali hiyo? Wa tz tuache kuzaa kama panya!
Unashauri tuzae wangapi?
 
Mtaji wa AFRICA Kwa sasa ni population kuwa kubwa, muda Si mrefu hao wa magharibi watakuja kununua labor kwetu. Mabinti zao wamegoma kuzaa.
Watakuja kununua wakati hivi sasa Waafrika wanafia baharini wakijaribu kwenda Ulaya? Tena wakifika wengi wanarudishwa, Nani anunue Waafrika?🤣🤣 Wakati maroboti yapo?
 
Tz Bado watu hawana elimu ya kujua athari za popln kubwa! Kukiwa na mapori ndiyo sababu ya kuzaa kama mbwa twitu? Kanda ya ziwa mama 1 anazaa watoto 17 kweli ni haki/halali hiyo? Wa tz tuache kuzaa kama panya!
Si bora uzae hivyo ukawa na uwezo pia. Lakini mtu anafyatua halafu watoto wanaishi in Hell world
 
Mbona kanda ya kusini nasikia ndio kuna wtoto wengi hawaendi shule, labda ndio inachangia madarasa kuwa na wanafunzi wachache kuliko kanda ya ziwa
Kanda ya Kaskazini ndio wanazaa kwa kiasi kutokana na uwezo wa familia matokeo yake wana familia zilizostawi vizuri sana.

Huku kwetu kusini ni majanga.

Wanashindana kuitiisha dunia lakini inaonekana Mungu kawakataa. Maisha magumu sana
 
Mi nimetokea kanda ya kaskazini,

Ukilinganisha na kipindi chetu tukiwa tunakua ambapo nyumba zilikuwa na watoto wengi na hata mkieda mtaani mnaunda timu kubwa ya kucheza mpira, kwa sasa hivi hali inatisha, hakuna watu, Nyumba zimebaki na wazee, vijana na watoto ni wa kuhesabu, na kuna nyumba nyingine hazina watu kabisa, actually miaka 15-20 ijayo nyumba nyingi zitakuwa zimebaki mahame maana wazee waliopo watakuwa wamekufa

unaweza ukakatokwa na machozi hasa ukikumbuka utotoni kulivyokuwa kumechangamka

Hii lakini inaweza kuwa na faida kimazingira maana kuna ukijani mwingi na vyanzo vya maji vimekuwa vikirudi, maana population kubwa inaua sana uoto na vyanzo vya maji

Yaani katika sensa ya mwaka huu nahisi Kilimanjaro itakokuwa na ongezeko hasi la watu
 
Huo ndio wastani wa Tanzania kwa sasa.
Wawili ina maana mkifa nyie wazazi wao wawili kuna watu wawili wanabaki duniani kuchukua nafasi yenu.
Kwa rate ya sasa ya uzaaji Tanzania inakadiriwa itakuwa na watu milion 130 miaka 30 mbeleni.
Dah!...fanya angalau 5
 
Kaskazini Thumbs up. Watu wengine wamebaki kuw ana wivu na nyinyi lakini wazee wenu walishtuka mapema sana.
 
Kaskazini Thumbs up. Watu wengine wamebaki kuw ana wivu na nyinyi lakini wazee wenu walishtuka mapema sana.
Mkuu population kupungua ni very depressing, ni jambo la fadhaa na huzuni

Mimi naunga mkono kuwa na population ambayo ni constant au inayokuwa kwa kasi ndogo, sio inayopungua. Inayoungua ni mbaya kama inayokuwa kwa kasi kubwa
 
Population constant au inayopungua ni jambo zuri kwa nchi maskini.
Mkuu population kupungua ni very depressing, ni jambo la fadhaa na huzuni

Mimi naunga mkono kuwa na population ambayo ni constant au inayokuwa kwa kasi ndogo, sio inayopungua. Inayoungua ni mbaya kama inayokuwa kwa kasi kubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…