Serikali itunge sheria kuhusu uzazi wa mpango angalau watoto wawili kila familia maana kasi ya uzazi Tanzania inatisha

Serikali isiingilie suala la uzazi lakini Vilevile watu wajitambue...

Kuna watu wanawaza ardhi tu, Je una resources za kustahimili population hio yote! Milioni 60 yenyewe hali ngumu, tukifika milioni 100 sitamani kuona itakuaje
 
Watu ni moja ya mitaji mikubwa sana katika ukuaji wa uchumi wa nchi. Tanzania bado tunahitaji watu wengi zaidi ili kuweza kuzitumia rasilimali tulizonazo kwa ukamilifu. Tatizo tulilonalo ni ukosefu wa viongozi bora na siasa safi!

Tanzania kama Taifa tunapaswa kuwekeza zaidi katika rasilimali watu.
 
Hili ni jambo linatakiwa kuangaliwa vizuri sana, tuwe na uwezo wa kupima kasi ya ukuaji wa idadi ya raia na kasi ya kuijaza hiyo ardhi tuliyo nayo tuone tutaimaliza lini, halafu je ikiisha kuwa imejaa ni kwamba hatutahitaji mapori tena?

Jambo lingine muhimu Serikali inayo kasi inayoendana na kasi ya ukuaji wa idadi ya raia katika kutoa huduma muhimu? Elimu, Maji safi, Huduma ya Afya, miundombinu ya kutosha, Umeme nk. nk.

Tunahitaji taifa lenye raia walio na afya bora na elimu nzuri inayokidhi mahitaji yetu, hilo litakuwa taifa lenye nguvu.
Waliandika kitambo wahenga kwamba ili nchi iendelee inahitaji a). Watu b). Ardhi c). Siasa safi na d). Uongozi Bora.

Sifa ya b), c), na d) vipo wazi ila walisahau a). Watu wa aina gani? Ni wazi tunahitaji Taifa lenye Afya na lililo Elimika.
 
Hicho ulichovuta leo achana nacho. Kama unaona Bongo michosho chukua Uraia wa Australia!
 
Kama hauna mbegu za kuzalisha wapishe wenye nazo tafadhali, kwani umeombwa msaada wa kuwasaidia hao wenye watoto wengi?
 

Watu wanazaa kama kuku, na maisha yenyewe ndo haya. Serikali iamrishe mwisho watoto wawili kama china. Zaidi ya hapo faini. Maana hata watoto wa mitaani wataisha kabisa na kazi zitakua nyingi kulingana na idadi ya watu waliomo
 
Iwe watoto wawili kwa kila mwanamke au kila mwanamme?
 
Utafiti usio rasmi unaonesha mataifa yenye population kubwa ndio matajiri . Eg USA, China, Canada, India, Russia, Germany, Nigeria, South Africa etc.... So acha watu waendelee kufyatua
 
Nimepitia hiyo mistari sijaona mahali walipotajwa ndugu wa damu wa Yesu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kirumbiu umesema ukweli kabisa, mimi ni shahidi yako kwa yote uliyo yasema.
 
Umeongea ukweli pale mula kuna shule wanafunzi wachache
Lemira nayo
Kyuu
Mboshwa
Mafeto nkwansira
Watu wazaeee hadi watoto kumi
Angalau tufikie million 300
 
Umeongea ukweli pale mula kuna shule wanafunzi wachache
Lemira nayo
Kyuu
Mboshwa
Mafeto nkwansira
Watu wazaeee hadi watoto kumi
Angalau tufikie million 300
Walio jitahidi kidogo eneo la Machame ni eneo la Mwowe karibu yote. Hasa huku Mwowe msikitini wamejitahidi.
 
Rasilimali hata zikiwa nyingi kuna vitu ambavyo ni adimu kwa mfano maji safi. Watu bilioni moja maji safi watayatoa wapi? Chakula cha kulisha watu bilioni moja kitatoka wapi? Hicho chakula kitalimwa na kufugwa wapi? Na hata tukisema tutaagiza maji na chakula kutoka nje, nchi zingine nazo wanaanza kuwa makini na maji yao na vyakula vyao. Zamani bahari zetu zilijaa samaki. Wavuvi hawaendi mbali wanarudi na samaki kibao. Siku hizi wavuvi mpaka waende mbali inamaanisha samaki wanaadimika na mpaka tunaagiza samaki. Nchi haiwezi tuu kuongeza watu hata kama ina utajiri wa rasilimali bila kufikiria mazingira.
 
Kama huwezi kuzalisha tulia usaidiwe. Mjinga mmoja wewe watu wanatekeleza agizo la Mwenyezi Mungu la zalieni mkajaze dunia wewe unaleta uhanithi wako hapa.
 
Hakuna viwanda vya maana ambavyo watu wangefanya hata shift za usiku!
Watanzania karibia asilimia 70% ikifika SAA mbili usiku wamejifungia ndani wanalala!! Kazi ni moja tu, "kuunganisha" viungo vya uzazi! Na bado kila mtaa utakuwa na shule yake!
 
 
watu wanazaa kama kuku, na maisha yenyewe ndo haya. Serikali iamrishe mwisho watoto wawili kama china. Zaidi ya hapo faini. Maana hata watoto wa mitaani wataisha kabisa na kazi zitakua nyingi kulingana na idadi ya watu waliomo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…