DOKEZO Serikali itupie macho viwanda vya wahindi, kuna unyonyaji mkubwa dhidi ya wafanyakazi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

JMWAKA

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2012
Posts
739
Reaction score
652
Sio siri viwanda ambavyo kuna Wahindi kuna unyonyaji mkubwa sana. Nabaki kushangaa jinsi ambavyo hawa Wahindi kwanza ni wageni katika nchi yetu lakini wanawanyanyasa sana watz mishahara midogo sana.

Unamlipaje mtu kutwa elfu 7 yaani atoke asubuhi mpaka jioni saa 11 unampa elfu 7?
Hakuna mkataba.
Hakuna NSSF.
Hakuna kitu.
Humo humo nauli, chakula juu yake.
Vyama vya wafanyakazi kimnya.
Vyama vya siasa kimnya.
Au sababu hawa jamaa ni watoaji rushwa wazuri.

Wenyewe wanalipana mishaharaa mizuri, plus usafiri plus nyumba ya kuishi
Huku watz wenzetu wakifanya kazi ngumu kwa malipo kiduchu nenda pale kiwanda cha patel mikocheni.

Hili serikali yetu inamtumikia nani kama wananchi wake wanateswa na wageni.
 
Viwanda vingi viliacha kutumia wafanyakazi wanatumia vibarua, na Kibarua haajiriwi na kiwanda bali kampuni husika.

Kwa Tanzania Viwandani minimum wage ni 5770 kwa siku, so mtu anaelipwa 7000 analipwa above minimum wage na hakuna kosa Kisheria.

Source
 
Hizo sheria zinazotungwa na watu ambao wapo katika viyoyozi wasiojali hali za watu wa tabaka la chini
Sheria inayokandamiza mwananchi wake
Watu wanakuja wanawake fortune nchini na nchi inabariki
 
Hizo sheria zinazotungwa na watu ambao wapo katika viyoyozi wasiojali hali za watu wa tabaka la chini
Sheria inayokandamiza mwananchi wake
Watu wanakuja wanawake fortune nchini na nchi inabariki
Kuna kazi nyingi sana zina lipa ovyo zaidi kuliko viwanda, 7000 kwa siku wala haipo kwenye kazi inayo lipa kidogo, nikukumbushe tu mshahara kidogo kabisa ni 60,000 kwa mwezi.
 
Dah! Aiseee inafikirishana 🤔🤔🤔 ivi mfano kuna uwakika wa maisha ya baadae kwa wao wajiriwa au ndy ile Mungu ataweka mkono wake mbeleni kwa waja wake
 
Bado hujaambiwa kuwa na wanalazimishwa kufanya kazi usiku tena kwa kufungiwa?.....na polisi wakiambiwa huwa wanafika mpaka viwandani usiku huo na kuondoka na bahasha huku wafanyakazi mkiwa mmefungiwa kufanya kazi?.....
 
Poleni sana
 
Kuna kazi nyingi sana zina lipa ovyo zaidi kuliko viwanda, 7000 kwa siku wala haipo kwenye kazi inayo lipa kidogo, nikukumbushe tu mshahara kidogo kabisa ni 60,000 kwa mwezi.

Hapo mtu anaishije kodi labda 30 000 kwa mwezi. Nauli 40,000 kwa mwezi. Chakula 60,000 kwa mwezi. Na ukute huyu mtu ana familia.
 
Wangeongeza hadi kufika at least 10,000 kwa mwezi. Sababu buku inaisjia kwenye nauli na chakula cha mchana tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…