DOKEZO Serikali itupie macho viwanda vya wahindi, kuna unyonyaji mkubwa dhidi ya wafanyakazi

DOKEZO Serikali itupie macho viwanda vya wahindi, kuna unyonyaji mkubwa dhidi ya wafanyakazi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Sawa bro ila hiyo dunia ina utawala pia sasa viongozi wanawatumikia kina nani kama citizen wanasuffer
Sometimes usioneshe umwamba kwenye serious ishu bro tuna serikali inayopaswa kuwajibika kwa watu wake
And vise versa, kwa hapa serikali haiwatumikii wananchi, bali wananchi wanaitumikia serikali,
Unafanya kazi kwa taabu na mateso, unatungiwa na sheria ngumu na kandamizi na serikali yako hiyo hiyo,
Serikali inaamua ulipwe mshahara kiduchu kabisa, halafu kwenye hiyo kiduchu nayo inakudai kodi.

Halafu yule anayetumiwa na serikali akunyonye anailipa serikali kodi kiduchu ili serikali impe uhalali wa kuendelea kukunyonya,
Nb>ukileta ujuaji polisi wanaitwa, wanakutandika bila huruma wala akili,
Solution ni moja tu--------!!!
 
Mbona hata Walimu hua wanalalamika mishahara yao mpaka leo?
Ni kada gani isiyolalamikia mishahara yao?

Dunia inahitaji kupambana na sio kutafuta huruma,huu ndio ukweli mchungu nakuambia,
Ukiona Viwandani ni mateso,rudi Kijijini kwenu,maisha sio rahisi kama unavyofikiria,

Unalalamika humu kuhusu viwanda vya wahindi,nimekuuliza,viwanda vya wabongo wao wanalipaje?
Ila naona umelikwepa swali langu.
Wewe utakuwa ni nyapara kwa muhindi, umewazidi wenzako mshahara, badala ya 7000 wewe unapewa 10,000 kwa siku ili uwakandamize wenzako, umesomeka
 
Wewe utakuwa ni nyapara kwa muhindi, umewazidi wenzako mshahara, badala ya 7000 wewe unapewa 10,000 kwa siku ili uwakandamize wenzako, umesomeka
Wewe ni punguani usiyetumia akili,
Jikite kwenye mada,huko unapoelekea nina uhakika hupawezi ila kama unajiamini endelea kuleta hizo kashfa ili upate unachokitafuta.
 
Mkuu tutake radhi elf 7 ina uhalali gani kishera gharama ya maisha ni kubwa sana wao wanaingiza pesa nyinyi kwa siku tungelipwa elfu kumi kwa siku ingekuwa afadhali tunaitaji utetezi kwa wanasiasa na raisi kwa ujumla
Unaweza uka jenga hoja haitoshi kimaisha, ila Kisheria ni halali minimum wage Viwandani kwa siku ni 5000, sio mimi niliopanga hio hela ni sheria.

Wao pia hawaingizi hela nyingi kama unavyofikiria, ikipanda hadi 10,000 watahitaji na wao kuongeza bei ya bidhaa.
 
Akili ikikaa sawa tutaacha biashara za uchuuzi na kuanzisha viwanda vyetu wenyewe kupunguza ukubwa wa tatizo. Serikali haikwepi lawama kwenye hili. Kwa sheria zilizopo bora kuagiza China kuliko kufungua kiwanda chako. Gharama za kuendesha kiwanda ni kubwa mno na lazima ukutane na mamlaka kibao za udhibiti. Bunge likae chini na kufanya marekebisho ya sheria za hovyo.
 
Back
Top Bottom