Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Selous hifadhi ya pori tengefu au pori la akiba kwasasa ndilo pori linalotegemewa sana na TAWA.
Kama kawaida ya binadamu hakosi alternative pale anapozidiwa njaa au shida.
Vijana wanaingia kwenye hifadhi mbalimbali kutafuta chochote kitu ili wapate kujinasua aidha kwenye njaa au wajinasue kwenye ufukara.
Sasa vijana wanaoshikwa huko Selous lango la Liwale wanauwawa kama paka mwitu tu.
Nisiandike sana haya ila kama serikali hii inapenda haki basi ikachunguze suala hili. Waende wilaya ya Liwale wapo vijana ambao walishuhudia wenzao wakikatwa miguu porini, kupigwa risasi na mateso mengine.
Ni unyama sana. Ukifika wilaya ya Liwale hata mtoto mdogo anajua kuwa askari wa hifadhi ya Selous wameua wananchi. Serikali hii kama itapuuzia haki, nasema katika Roho, haitasimama.
Nilisema wakati wa serikali ya Magufuli na ninasema wakati huu. Serikali hii ikipuuzia haki haitasimama. Itaanguka soon.
Sibariki vitendo vya kijangiri, kukata miti au kuchimba madini kwenye hifadhi ila mtu akivunja sheria Askari sio hakimu.