Serikali iunganishe Dar na Pwani uwe mkoa mmoja uitwe Dar ili watu wazidi kusogea nje ya mji

wazo lako zuri ila kwanini TZ yote isiitwe Dar es salaam ili hao wanaorundikana wabaki hapo hapo Dar waliyopo wachangamkie fursa.

mfano; mtoa mada unakuwa Dar mtaa/wilaya/kata/kitongoji/kijiji cha Singinda, Tanga,Mtwara

hapo vipi??
 
Uko sahihi, ila kwa upande wangu naona ni bora kuchukua maeneo kadhaa ya mkoa wa Pwani kama vile Bagamoyo, Kibaha, Chalinze, kisarawe na kibiti hayo maeneo ndio yawe sehemu ya Dar mana mkoa wa pwani ni mkubwa sana (hvy kwa kufanya hvy itakuwa ni sawa na kugawa mkoa wa pwani kupata mikoa miwili)
 
Tena ni beach kabisa ila watu wanapadharau sana.
 
Basi kama mambo ni hivi, mtoa mada hoja yake inamashiko sana mamlaka wapokee wazo hili.
 
Wazo zuri. Muhimu serikali kabla ya kuunganisha iweke huduma za msingi kama barabara, shule,masoko,hospital, vituo vya mabasi, daladala, huduma za polisi karibu nk

Viwanja muhimu vipimwe, at least vianzie 30 x 20. Mitaa ta kueleweka.
 
We kilaza kweli kweli. Kata za Mkuranga ziende Lindi, wakati kutoka Mkuranga unapita wilaya za Kibiti na Rufiji ndio ufike Lind.😀😀😀
Mafia zamani huko ilikua mkoa wa Mtwara, walipoigawa Mtwara kutoa Lindi na Mzizima kutoa Dar basi automatically Mafia ikahamia Pwani.
 
Mwaka 1974 Serikali ya Tanzania ilianzisha mikoa mitatu kama ifuatavyo :-
1. Iligawa mkoa wa Pwani na kuzaliwa mkoa wa Dar es Salaam.
2. Iligawa mkoa wa Mtwara na kuzaliwa mkoa wa Lindi.
3. Ilimega Wilaya ya Mpanda kutoka mkoa wa Tabora na kumega Wilaya ya Sumbawanga kutoka mkoa wa Mbeya na kuunda mkoa wa Rukwa.

Hivyo basi, haiwezekani Tena Dar kuunganishwa na Pwani isipokuwa kwa kuwa mkoa wa Dar umejaa Cha kufanya ni kumega baadhi ya maeneo ya Pwani na kuyaingiza katika mkoa wa Dar. Nadhani nimeelewrka.
 
Nakubaliana na mtoa mada kwa 100%
 
Mbaya zaidi watu wa Dar wanaoenda kujenga huko na vikampuni uchwara vya viwanja vinakata viwanja vya 400sqm. Mwisho sehemu ambazo zingekuwa suburbs nzuri za Dar zinageuka kuwa slums flani hivi.
Mkuu kwa hili nami nakubaliana na wewe. Wizara ya ardhi itazame hii biashara ya viwanja vidogo vidogo kama visheti katika mkoa wa pwani hasa mkuranga, nk. Mkoa wa pwani utakuja kuwa kama mkoa wa mapokezi ya wakimbizi kutoka kwenye inchi zenye vita kwa mbanano utakaotokea siku za usoni. Serikali inafanya kosa lilelile la ujenzi holela alafu wanakuja na plan ya urasimishaji wa makazi.

Ukitaka kushangaa nchi hii uwe kwenye skyscrapers au usafiri wa angani alafu utazame chini utashangaa makazi ya watu yalivyokaa hovyo cha kushangaza serikali haina plani za miaka 70 au 100 ijayo.

Kama kuna watu wa ardhi humu waseme jambo kuhusu matumizi ya ardhi ya inchi hii.

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
Shida sio kuunganishwa kuwa mkoa. Mmoja wa jina, muhimu ni miundo mbinu, hakuna shida kuishi kisemvule kama tu kisemvule huduma zote muhimu zinapatikana, usafiri wa kuja huku mjini uwepo.

Changamoto ni miundo mbinu, waweke vitu sawa, mkuranga tu hapo kuna sehemu hakuna umeme, barabara mboovu kinooma, unadhani mtu anashawishika vipi kwemda kujificha huko.
Wakati nahamia kigamboni miaka ya 90, 2000 mwanzoni hakuna ndugu alikuwa anashawishika kuja kununua huku, ila baada ya miaka kwenda huduma muhimu kusogea, sasa pamepanda saana thamani kuna viwanja huna milioni 50 unaambiwa hupati,
serikali ijiongeze, kuna vitu vinawavutia na kuhamasisha watu kuhamia sehemu na kuishi.
 
We unaongelea watu kulundikana dar..
Watu hawasogei nje ya dar sio kwa sababu eti wanapapenda dar

Hiyo vikindu ni kama iko dar maana hakuna umbali wa kutisha.. watu hawasogei pwan
Sababu jografia ya pwani ilivyo

Hv unawezaje kuishi vikindu kisha ukihitaji huduma za kiserikali ngaz ya mkoa uende kibaha.. yaan unavuka mkoa mwingine kufata huduma za serikali mkoan kwako

Aligawa mkoa wa pwan ana akili za kiisrael kuigawa palestina kati kwa kati

Wanaotoka west bank wawe na pasport wakitaka kwenda south palestina
 
Mkuu wazo lako ni zuri lakini huoni kuunganisha mkoa wa Dsm na Pwani litakuwa ni eneo kubwa sana kiutawala?

Kwanza ukiuchukulia tu mkoa wa Pwani ulivyokaa tenge kijiografia (Kibaha, Chalinze, Bagamoyo, Kisarawe, Mkuranga, Kibiti, Rufiji na Mafia).

Cha muhimu sana ni kuboresha tu miundo mbinu kwa mkoa mzima wa Pwani, watu watasogea tu wenyewe.

Mkuranga kabla ya kuwa wilaya yote hiyo ilikuwa ni wilaya ya Kisarawe, lakini kwasasa inaikimbiza Kisarawe kutokana na kufunguka kwa barabara (Barabara kuu) iliyopelekea mwingiliano mkubwa wa watu.

Kisarawe imeishia kuendelea kwa upande wa Kiluvya pekee.
Sambamba na Kibaha na Chalinze.
Nafikiri mchawi ni miundo mbinu tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…