Serikali iwaangalie Walimu wanaojitolea iwasaidie hata kwa chochote

muafi

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2015
Posts
2,557
Reaction score
6,128
Kuna Walimu wanamiaka miwili wengine zaidi wanajitolea kwenye shule za umma, wamepewa mpaka vipindi kabisa na wanafanya kazi hawana tofauti na waajiriwa.
 
Kwanini ujitolee tu,ulipwe 20 hadi 50?
Umeambiwa usipoenda kujitolea watoto hawatasoma?
Mnaojitolea,hamuoni wenzenu wa kada ya afya,wanalipwa walau laki kadhaa?
Acheni mambo ya unyonge,eti mnawinda ajira kwa kivuli cha kujitolea,wakati kuajiri wanaajiri wa 2020-21,acheni hizo,mara kuchukua kadi za chama,acheni hizo,kama ajira zitakuja tu.
 
Mkuu kujitolea kwa lengo la kubembeleza ajira ni ujijnga, kama kweli unaithamini elimu yako uliyoisotea miaka mingi huwezi kufundisha for free huku ukitegemea huruma ya wanasiasa. Huu ni mwaka wa nne toka nimalize chuo nipo kitaa napambana hakuna kazi sijawahi fanya, nimejifunza mengi huku mtaani. Katika maisha yangu siwezi kuidhalilisha taaluma yangu kwa kujitolea. Jichanganye na watu and learn how to make money out of interaction.
 
Achana na kujitolea,kafanye shughuli zingine za kujipatia kipato.
Anzisha hata kijiwe cha kuchoma mishikaki au biashara zingine ndogondogo.
Wengi waliojitolea hawakuajiriwa,shtuka.
 
Nilisikia kijana mwenye nguvu na akili timamu anajitolea kufundisha kwa kubembelezaa aajiriwe hua nahofia future ya taifa hili itakua ya watu wa aina gani aisee.
 
Huu ni upumbafu sn, ajira kwa watanzania hazitakiwi kuwa huruma au hisani ya mtu inatakiwa iwe ni kipaumbele cha taifa
 
Nilisikia kijana mwenye nguvu na akili timamu anajitolea kufundisha kwa kubembelezaa aajiriwe hua nahofia future ya taifa hili itakua ya watu wa aina gani aisee.
Ni taifa la watu wajinga, eti ajira iwe ni huruma
 
Wakitoka hapo walalamike wanazo kadi za chama Chao na wamehudhuria mikutano ya chama[emoji23][emoji23][emoji23][emoji2365] hivyo wapate ajira, walimu ni wengi nchini lakini ndio kundi lenye matatizo lukuki licha ya kuwa na vyama lukuki vya utetezi kwao.

Waandae proposal wakakope pesa waanzishe biashara, au wasubiri ajira zikitangazwa basi waambatanishe majina kwa Katibu wa CCM kwenda wizarani kuwaombea nafasi[emoji847]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…