Serikali iwaangalie Walimu wanaojitolea iwasaidie hata kwa chochote

Serikali iwaangalie Walimu wanaojitolea iwasaidie hata kwa chochote

muafi

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2015
Posts
2,557
Reaction score
6,128
Kuna Walimu wanamiaka miwili wengine zaidi wanajitolea kwenye shule za umma, wamepewa mpaka vipindi kabisa na wanafanya kazi hawana tofauti na waajiriwa.
 
Kwanini ujitolee tu,ulipwe 20 hadi 50?
Umeambiwa usipoenda kujitolea watoto hawatasoma?
Mnaojitolea,hamuoni wenzenu wa kada ya afya,wanalipwa walau laki kadhaa?
Acheni mambo ya unyonge,eti mnawinda ajira kwa kivuli cha kujitolea,wakati kuajiri wanaajiri wa 2020-21,acheni hizo,mara kuchukua kadi za chama,acheni hizo,kama ajira zitakuja tu.
 
Mkuu kujitolea kwa lengo la kubembeleza ajira ni ujijnga, kama kweli unaithamini elimu yako uliyoisotea miaka mingi huwezi kufundisha for free huku ukitegemea huruma ya wanasiasa. Huu ni mwaka wa nne toka nimalize chuo nipo kitaa napambana hakuna kazi sijawahi fanya, nimejifunza mengi huku mtaani. Katika maisha yangu siwezi kuidhalilisha taaluma yangu kwa kujitolea. Jichanganye na watu and learn how to make money out of interaction.
 
Achana na kujitolea,kafanye shughuli zingine za kujipatia kipato.
Anzisha hata kijiwe cha kuchoma mishikaki au biashara zingine ndogondogo.
Wengi waliojitolea hawakuajiriwa,shtuka.
 
Nilisikia kijana mwenye nguvu na akili timamu anajitolea kufundisha kwa kubembelezaa aajiriwe hua nahofia future ya taifa hili itakua ya watu wa aina gani aisee.
 
Kuna Walimu wanamiaka miwili wengine zaidi wanajitolea kwenye shule za umma, wamepewa mpaka vipindi kabisa na wanafanya kazi hawana tofauti na waajiriwa.

Walimu hawa wanasaidia sana kupunguza tatizo la uhaba haswa kule vijijini wanapewa mpaka kazi nyingi sana ili wawape hata elfu 20 ya sabuni.

Rais waangalie watu hawa wazalendo wamefanya kazi zaidi ya mwaka kwa malipo ya elfu 20 mpk 50 bila kuchoka lakini wanasaidia sana kutoa elimu kwa vijana.

Wape ajira Jamani hata kwa huruma yako tu! na wala sio wengi hata 2000 wanaweza wasifike!

Wahurumie sana wamejitahidi kuwa wazalendo sana.
Huu ni upumbafu sn, ajira kwa watanzania hazitakiwi kuwa huruma au hisani ya mtu inatakiwa iwe ni kipaumbele cha taifa
 
Nilisikia kijana mwenye nguvu na akili timamu anajitolea kufundisha kwa kubembelezaa aajiriwe hua nahofia future ya taifa hili itakua ya watu wa aina gani aisee.
Ni taifa la watu wajinga, eti ajira iwe ni huruma
 
Wakitoka hapo walalamike wanazo kadi za chama Chao na wamehudhuria mikutano ya chama[emoji23][emoji23][emoji23][emoji2365] hivyo wapate ajira, walimu ni wengi nchini lakini ndio kundi lenye matatizo lukuki licha ya kuwa na vyama lukuki vya utetezi kwao.

Waandae proposal wakakope pesa waanzishe biashara, au wasubiri ajira zikitangazwa basi waambatanishe majina kwa Katibu wa CCM kwenda wizarani kuwaombea nafasi[emoji847]
 
Back
Top Bottom