Askofu Mwaikali kihistoria aliheshimika kwa misimamo mikali na ni mtu asiye yumbishwa. Nakumbuka wakati Nikiwa muumini betheri sae alichaguliwa hapo hapo uyole alipovuliwa katika uchaguzi uliochukuliwa na wengi kama ushindi kwa kanisa. Hata hivi alibadilika sana baada ya uaskofu.... akawa mtu mnyenyekevu mno na misimamo ya chini chini Nadhani ndio busara za kiaskofu.
Ni vyema pia ni vyema ukamfahamu hasimu wake mwanafalsafa Askofu mteule daktari msomi mwakihaba... Huyu alihudumu kama askofu msaidizi tangu nyakati za askofu mwakyolike. Warutheri humuheshimu sana kwa uhodari wake wa mahubiri. Nilimfahamu kama mtu mtulivu sana maana hata baaada ya kukikosa kiti cha u askofu Aliendelea kuhudumu kwa nafasi ya usaidizi kwa askofu Mwaikali.
Mpasuko Ulianza baada ya askofu Mwaikali kuisimamia kidete agenda ngumu iliyokwama kwa miaka mingi ya kuhamishia dayosisi Jiji kutokea Tukuyu. Alipata uungwaji mkono mkubwa mbeya jiji na kyela huku akipingwa na watu wa Tukuyu. Hapo ndipo Mwanafalsafa mbobezi mwakihaba alipotumia nafasi hiyo kujishikiza upande wa Tukuyu na kujitoa mamlakani, Askofu mwaikali asiyeyumbishwa alichagua msaidizi wake na kazi ya kuhamia jiji iliendelea....
Kilichoendelea hapo ilikuwa mpasuko. Mwaikali aliungwa mkono na watu wa mbeya jiji na kyela huku Mwakihaba akipata uungwaji mkono kwa badhi ya sharia za jiji na kyela . Mpaka hitimisho Mwaikali anavuliwa madaraka na maaskofu wenzie wawili Malasusa na Dr Shoo....
Mgogoro huu unapanda na kushuka nyingi ila naomba nizungumzie mambo machache yaliyogusiwa na mtoa maada
(I) kuna orodha ya maaskofu wanaotajwa kuichafua KKKT
Ukitazama hiyo orodha sawa inamtu asiyemtulivu Askofu Mengele wa kusini, ila kuwashutumu watu makini kama askofu bagonza na Prf Hance Mwakabana ambaye ni Mnyeti wa kanisa la kirutheri ni jambo linalo zua hofu. Nashauri maaskofu hawa na wengineo wahukumiwe kwa wallchart kisema na sio tuu kuwaona maadui kwakuwa walionekana kumbeba Mwaikali.
(ii) Iwapo maamuzi ya kumtoa mwaikali yalikuwa sahihi
Hilo ni swali linguine tunapaswa kujiuliza. Kwanza inatakiwa utambue kuwa kanisa la kirutheri ni Muunganiko wa makanisa 1963 hivyo anayetajwa kama askofu mkuu huwa ni Celebrate na hana mamlaka ya kinidhamu kwa maaskofu. Warutheri mtakumbuka mgogoro wa Askofu mdegela na Mchungaji Mtatifikola wakati huo Askofu Malasusa alishindwa kabisa kumuadhibu Mdegela licha ya makosa ya wazi sana lakini leo Malasusa huyo huyo anampotosha Dr Shoo kumpindua Mwaikali.
Ni nani Anae mpa nguvu Dr Shoo?
Binafsi naona ni mwaikali mwenyewe
Kwanza, aliwahi kukariliwa kusema kuwa atakuwa tayari kuyafuata maamuzi ya mkuu wa kanisa.
Pili,Ameshindwa kujimilikisha kanisa kama walivyofanya kina mdegela na Malasusa even Bagonza... Alidhani kuongoza KKKT ni mambo ya kiroho tuu kumbe hitaji pia ucheze siasa tena siasa za mbeya ni chafu
Hatma ya kanisa
Kwanza watu wa Konde hatuelewi namna gani tutaingia katika madhabahu inayoongozwa na Mwakihaba aliye mpindua Mwenzie. Pili muunganiko wa konde hauwezekaniki labda kugawa Diocis na Mwisho Dr Shoo awe makini Sana na Malasusa....
Malasusa ni Rafiki yangu nikiwa usharika wa kiluvya DMP. Kuna machafu Mengi niliyowahi kuyasikia dhidi yake ila sikutaka kuamini, ila sasa nyanza kuwa na hofu kubwa kuwa huenda kweli ni Nyoka wa makengeza mtu mjanja mjanja.
Ni toe ushauri kwa watu wanao mshauri Mwaikali, hawezi kurudi madarakani, azidi kuwa mtu wa maombi na unyenyekevu kama Hance Mwakabana. Asipende masuala ya mahakamani, amuachie Dr Shoo na Malasusa ambao wamefikia hatua ya kutinga na wanasheria kwenye video vya kikanisa. Kwetu wanakonde kukubali kumfuasa Mwakihaba ni jambo linalohitaji kusubiri amani ya Roho na si kwa wakati huu.
KKKT ijaribu kutizama uratibu wa miradi yake kama shule na Hospitali, kwani miradi yake imefanya diocis kuwa na mapesa ya kumwaga.... sharika zinazidi kunyonywa huku viongozi wakipambana kuongoza Diosis aidha miradi ya kanisa imeendelea kufanya vibaya kadri muda unavyozidi kwenda.
Poleni kwa Gazeti ndimi mrutheri halisi.
Christine1
Jidu La Mabambasi