Serikali iwachukulie hatua hawa Maaskofu wa KKKT kwa kuleta fujo katika Jamii ya waumini

Haya ni masuala ya dini ndio maana serikali inakuwaga makini ktk kuingilia na ktk kumbukumbu zako ni lini serikali iliingilia migogoro ya dini ili kuisuluhisha
Migogoro ya kanisa ni kweli haiingiliwi na serikali ila jinai inashujulikiwa polisi.

Umesema kuna ubadhirifu wa fedha eh?
 
Huo unadhirifu ndio unaosababisha migogoro kokote kule unaposikia kanisa lipo katika conflict na hakuna polisi wala serikali itakayoingilia hiyo sintofahamu mpk kanisa lenyewe litakaposolve matatizo yake
 
Mkuu ngoja wakatane mapanga , mundu na ngumi kavu kavu, ndo serikali itaamka toka usingizini.
 
Huo unadhirifu ndio unaosababisha migogoro kokote kule unaposikia kanisa lipo katika conflict na hakuna polisi wala serikali itakayoingilia hiyo sintofahamu mpk kanisa lenyewe litakaposolve matatizo yake
Basi kama chanzo ni ubadhirifu tudeal na chanzo na sio matokeo.
 
Bagonza ana exposure gani zaidi ya kubwabwaja kila uchao.
Na ana scandal ya kuwa na watoto wawili nje ya ndoa yake na kuwatelekeza watoto.
Huyo ndio role model kimaadili kwako!

You are entitled to your opinion kuwa unaamini kuwa Askofu Bagonza anabwabwaja!! Lakini heshima aliyokuwa nayo kwa wananchi wa Tanzania wanaojitambua ni kubwa sana; hata mheshimiwa Rais anatambua mchango wake kwani huwa anajumuishwa kwenye majadiliano mengi na serikali.
Hayo ya kuwa na watoto wa nje ni suala ambalo kama lingekuwa la ukweli lingemshushia heshima na kutokukubalika na waumini wake kitu ambacho hakipo!! Askofu Bagonza ni kiongozi wa mfano ambaye ni jasiri tofauti na viongozi wa huko kwenu wasokile ambao wanasifika kwa ubinafsi, na wametumia nafasi za uongozi walizopewa kujilimbikizia mali kwa ufisadi uliokithiri!! Kiwanja cha ndege cha SONGWE kimetengewa fedha nyingi sana over the years lakini hali ya kiwanja hailingani na fedha serikali iliyopeleka kukijenga hicho kiwanja!! Jiwe aliligundua hilo na ndiyo maana hakuwakubali viongozi wa kutoka huko kutokana na unafiki!!!
 
BARAZA la Vijana wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT, Dayosisi ya Konde, limemtupia lawama Mkuu wa kanisa hilo nchini, Askofu Dk. Fredrick Shoo, likidai kuongoza mkutano wa kumwondoa Askofu wa dayosisi hiyo, Dk. Edward Mwaikali, badala ya kutafuta njia sahihi ya kumaliza mgogoro ....

[https://res]

unaofukuta.

Akisoma taarifa ya msimamo wa vijana wa dayosisi hiyo jana, Marko Mahenge, alidai Askofu Dk. Shoo amekuwa sehemu ya kukuza mgogoro huo badala ya kutafuta njia sahihi ya kujadili namna ya kushughulika na jambo hilo ambalo linaendelea kuyumbisha Dayosisi ya Konde.

Alisema kwa muda mrefu vijana walikuwa kimya wakifuatilia mwenendo ya mgogoro huo huku wakitarajia kufanyika kwa hekima na busara katika kushughulikia maridhiano ya kuhamisha makao makuu ya dayosisi hiyo kutoka mjini Tukuyu katika Wilaya ya Rungwe na kupelekwa Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

“Sisi vijana wa Jimbo hili la Mbeya na maeneo mengine ya dayosisi hii tunapinga vikali uamuzi wa Mkuu wa Kanisa kumwondoa Askofu Mwaikali kwenye kiti chake kwa sababu mkutano uliofanyika Machi 22, katika Ushirika wa Uyole ulikuwa batili, tunamtambua Dk. Mwaikali kuwa ndiye askofu wetu na hapa jimboni haondoka wala mchungaji au Mkuu wa Jimbo,” alisema Mahenge.

Aidha, Mahenge aliliomba Baraza la Maaskofu wa kanisa hilo nchini kuingilia kati mgogoro huo kwa kuiita halmashauri kuu ya dayosisi na viongozi wengine ili kukubaliana mambo ya kufanya.

Akizungumza wakati wa ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Ruanda, yalipo makao makuu ya Dayosisi ya Konde, Mkuu wa Jimbo, Mchungaji Nyibuko Mwambola, alisema Halmashauri Kuu haitambui mkutano ulioitishwa na Askofu Dk. Fredrick Shoo kwa madai kuwa ulikuwa batili.

Alimtupia lawama Askofu Dk. Shoo kama mkuu wa kanisa kwa kushindwa kusuluhisha mgogoro huo na kuwa sehemu ya kuchochea hali ambayo alidai inazidi kuongeza chuki na mfarakano.

Kadhalika, alisema baada ya mkutano wa kumchagua askofu mwingine, Geofrey Mwakihaba, Askofu Dk. Shoo alituma waraka kwa taasisi zote za kifedha kufunga akaunti za dayosisi.

Alisema hatua hiyo imewasababishia kushindwa kufanya malipo yoyote ikiwamo mishahara ya wachungaji na watumishi wengine wa dayosisi hiyo.

Vile vile, alidai kuwa Dk. Shoo amewatumia barua wachungaji wote wa Dayosisi ya Konde kuhudhuria kikao kinachofanyika kesho jijini Dodoma, bila kumpa taarifa Askofu wa Jimbo Dk. Mwaikali, na kwamba Halmashauri Kuu imesema naye atashiriki kikao hicho.

“Mkuu wa Kanisa ameonyesha dhahiri upande alipo kwa sababu ameshindwa kutukutanisha pamoja viongozi wa dayosisi na kujadili pamoja namna bora ya kumaliza huu mgogoro badala yake ameonesha wazi kushindwa kusimamia jambo hilo na kuchangia kuchochea suala hili, sisi tunamtambua bado Askofu Mwaikali ndiyo anasimamia dayosisi yetu ya Konde,” alisisitiza.

“Haiwezekani Mkuu wa Kanisa aitishe mkutano na kufanya uchaguzi wa kumchagua askofu mwingine, tena kwa siku moja, inaonyesha dhahiri kuna chuki binafsi na sio suala la kuhamisha makao mkuu ya dayosisi.”

Machi 22 mwaka huu Mkuu wa Kanisa la KKKT nchini, Askofu Dk Fredrick Shoo, pamoja na wajumbe 201 walifanya mkutano katika Usharika wa Uyole jijini Mbeya kwa lengo la kumaliza mgogoro huo ambapo liliibuka suala la wajumbe kutokuwa na imani na Askofu Dk. Edward Mwaikali.

Katika mkutano huo ambao uliendeshwa na Askofu Dk. Shoo na kudumu kwa saa 10, ulitumika kumchagua Askofu mwingine Mchungaji Geofrey Mwakihaba, ambaye alitangazwa mbele ya wajumbe wa mkutano.

Kutokana na uamuzi huo baadhi ya vijana wa KKKT mkoani Mbeya walieleza kuwa mchakato uliotumika kuwa ulikuwa batili.

Hata hivyo, Askofu Dk. Shoo alipotafutwa na Nipashe kwa simu jana, muda wote hakupatikana kuzungumzia suala hilo.

Mgogoro wa kwanini yahamishwe makao makuu ya dayosisi kutoka mjini Tukuyu katika Wilaya ya Rungwe na kwenda Halmashauri ya Jiji la Mbeya, ulianza kufukuta tangu mwaka 2017 hadi sasa.

Hii sasa ni hatari kwa mustakabali wa amani nchini.

Inavyoonekana kuna kikundi cha Maaskofu ambao wameamua kuleta ufarakano ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Tanzania-KKKT.

Hili kundi yumo Askofu Bagonza wa Karagwe
Askofu Mwaipopo wa Jimbo La Ziwa Tanganyika, Sumbawanga
Na sasa amengia hilo kundi Askofu aliyetimuliwa Dr Mwaikali aliyekuwa Konde
Askofu mstaafu Isaya Mengele wa Kusini Njombe

Serikali ikilifumbia macho suala hili yatatokea yale ya KKKT Meru na Jimbo la Kaskazini miaka ya 90, ambapo watu waliuwawa.

Kuna Maaskofu wamelifanya Kanisa, hasa Dayosisi kuwa mali zao na familia zao, na kuteteana hata kama maovu ya dhahiri yanaonekana.

Serikali isiogope kutumia maguvu yake pale inapoonekana kuwa hali ya amani inataka kutoweka

Mbona kwa vyama vya siasa serikali inachukua hatua haraka?

View attachment 2163812

View attachment 2163814

View attachment 2163817

View attachment 2163821
 
BARAZA la Vijana wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT, Dayosisi ya Konde, limemtupia lawama Mkuu wa kanisa hilo nchini, Askofu Dk. Fredrick Shoo, likidai kuongoza mkutano wa kumwondoa Askofu wa dayosisi hiyo, Dk. Edward Mwaikali, badala ya kutafuta njia sahihi ya kumaliza mgogoro ....

[https://res]

unaofukuta.

Akisoma taarifa ya msimamo wa vijana wa dayosisi hiyo jana, Marko Mahenge, alidai Askofu Dk. Shoo amekuwa sehemu ya kukuza mgogoro huo badala ya kutafuta njia sahihi ya kujadili namna ya kushughulika na jambo hilo ambalo linaendelea kuyumbisha Dayosisi ya Konde.

Alisema kwa muda mrefu vijana walikuwa kimya wakifuatilia mwenendo ya mgogoro huo huku wakitarajia kufanyika kwa hekima na busara katika kushughulikia maridhiano ya kuhamisha makao makuu ya dayosisi hiyo kutoka mjini Tukuyu katika Wilaya ya Rungwe na kupelekwa Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

“Sisi vijana wa Jimbo hili la Mbeya na maeneo mengine ya dayosisi hii tunapinga vikali uamuzi wa Mkuu wa Kanisa kumwondoa Askofu Mwaikali kwenye kiti chake kwa sababu mkutano uliofanyika Machi 22, katika Ushirika wa Uyole ulikuwa batili, tunamtambua Dk. Mwaikali kuwa ndiye askofu wetu na hapa jimboni haondoka wala mchungaji au Mkuu wa Jimbo,” alisema Mahenge.

Aidha, Mahenge aliliomba Baraza la Maaskofu wa kanisa hilo nchini kuingilia kati mgogoro huo kwa kuiita halmashauri kuu ya dayosisi na viongozi wengine ili kukubaliana mambo ya kufanya.

Akizungumza wakati wa ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Ruanda, yalipo makao makuu ya Dayosisi ya Konde, Mkuu wa Jimbo, Mchungaji Nyibuko Mwambola, alisema Halmashauri Kuu haitambui mkutano ulioitishwa na Askofu Dk. Fredrick Shoo kwa madai kuwa ulikuwa batili.

Alimtupia lawama Askofu Dk. Shoo kama mkuu wa kanisa kwa kushindwa kusuluhisha mgogoro huo na kuwa sehemu ya kuchochea hali ambayo alidai inazidi kuongeza chuki na mfarakano.

Kadhalika, alisema baada ya mkutano wa kumchagua askofu mwingine, Geofrey Mwakihaba, Askofu Dk. Shoo alituma waraka kwa taasisi zote za kifedha kufunga akaunti za dayosisi.

Alisema hatua hiyo imewasababishia kushindwa kufanya malipo yoyote ikiwamo mishahara ya wachungaji na watumishi wengine wa dayosisi hiyo.

Vile vile, alidai kuwa Dk. Shoo amewatumia barua wachungaji wote wa Dayosisi ya Konde kuhudhuria kikao kinachofanyika kesho jijini Dodoma, bila kumpa taarifa Askofu wa Jimbo Dk. Mwaikali, na kwamba Halmashauri Kuu imesema naye atashiriki kikao hicho.

“Mkuu wa Kanisa ameonyesha dhahiri upande alipo kwa sababu ameshindwa kutukutanisha pamoja viongozi wa dayosisi na kujadili pamoja namna bora ya kumaliza huu mgogoro badala yake ameonesha wazi kushindwa kusimamia jambo hilo na kuchangia kuchochea suala hili, sisi tunamtambua bado Askofu Mwaikali ndiyo anasimamia dayosisi yetu ya Konde,” alisisitiza.

“Haiwezekani Mkuu wa Kanisa aitishe mkutano na kufanya uchaguzi wa kumchagua askofu mwingine, tena kwa siku moja, inaonyesha dhahiri kuna chuki binafsi na sio suala la kuhamisha makao mkuu ya dayosisi.”

Machi 22 mwaka huu Mkuu wa Kanisa la KKKT nchini, Askofu Dk Fredrick Shoo, pamoja na wajumbe 201 walifanya mkutano katika Usharika wa Uyole jijini Mbeya kwa lengo la kumaliza mgogoro huo ambapo liliibuka suala la wajumbe kutokuwa na imani na Askofu Dk. Edward Mwaikali.

Katika mkutano huo ambao uliendeshwa na Askofu Dk. Shoo na kudumu kwa saa 10, ulitumika kumchagua Askofu mwingine Mchungaji Geofrey Mwakihaba, ambaye alitangazwa mbele ya wajumbe wa mkutano.

Kutokana na uamuzi huo baadhi ya vijana wa KKKT mkoani Mbeya walieleza kuwa mchakato uliotumika kuwa ulikuwa batili.

Hata hivyo, Askofu Dk. Shoo alipotafutwa na Nipashe kwa simu jana, muda wote hakupatikana kuzungumzia suala hilo.

Mgogoro wa kwanini yahamishwe makao makuu ya dayosisi kutoka mjini Tukuyu katika Wilaya ya Rungwe na kwenda Halmashauri ya Jiji la Mbeya, ulianza kufukuta tangu mwaka 2017 hadi sasa.
Mkutano huo ulifanyika wapi?
 
Back
Top Bottom