Serikali iwahamasishe wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara kuwa na makazi bora

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Lindi na Mtwara ni miongoni mwa mikoa ambayo wananchi wake wana uhakika wa kupata fedha za pamoja tofauti na baadhi ya mikoa.

Kuna msimu wa ufuta, vijana hupata mamilioni, msimu wa korosho wazee pamoja na vijana hupata mamilioni, msimu wa mbaazi pia huwapa mamilioni wakulima baadhi. Ila makazi ya wananchi wengi kusini (home land) ni duni.

Kipaumbele chao ni pikipiki. Fahari yao ni kila mtu awe na pikipiki yake. Million 2.5-3 inayoweza kununua pikipiki Moja inaweza kumfanya mtu aanze ujenzi wa nyumba ya wastani kijijini na msimu unaofuata akamalizia nyumba yake vizuri.

Makazi bora ndio ustawi wa jamii yoyote. Kila msimu mtu akipata pesa kusini huko mtu hununua pikipiki mpya au gari. Baada ya muda anafulia. Serikali ina sauti kubwa, ihamasishe watu wajenge nyumba bora.
 
Umefika Dodoma, Singida, Tabora ukaona vinyumba vya flati vimechimbwa chini kama nyumba za nyegere?

Umewahi Kuona manyata ya wamasai licha ya kuwa na ng'ombe lukuki?
Maisha duni ya Dodoma, Singida na sehemu zingine isiwe sababu ya kuhalalisha ujinga unaofanywa sehemu nyingine.
Kusini ndio origin yangu .
98% ya ndugu wako Lindi .
Pesa zipo ila makazi daah
 
Maneno 'makazi bora' ni tata ndg!
Kwa msaada wa picha halisia, naomba utofaiutishe baina ya makazi bora na duni
 
Lindi na Mtwara ni miongoni mwa mikoa ambayo wananchi wake wana uhakika wa kupata fedha za pamoja tofauti na baadhi ya mikoa.

Kuna msimu wa ufuta, vijana hupata mamilioni, msimu wa korosho wazee pamoja na vijana hupata mamilioni, msimu wa mbaazi pia huwapa mamilioni wakulima baadhi. Ila makazi ya wananchi wengi kusini (home land) ni duni.

Kipaumbele chao ni pikipiki. Fahari yao ni kila mtu awe na pikipiki yake. Million 2.5-3 inayoweza kununua pikipiki Moja inaweza kumfanya mtu aanze ujenzi wa nyumba ya wastani kijijini na msimu unaofuata akamalizia nyumba yake vizuri.

Makazi bora ndio ustawi wa jamii yoyote. Kila msimu mtu akipata pesa kusini huko mtu hununua pikipiki mpya au gari. Baada ya muda anafulia. Serikali ina sauti kubwa, ihamasishe watu wajenge nyumba bora.
Umefika Tandahimba vijijini? Nenda halafu uje uandike tena. Pia,tambua kwamba kujenga au kuwa na vitu bora kunatokana na kiwango cha kipato/uchumi.
Ila ukizunguka maeneo mengi Tanzania hali ni ile ile kwa maeneo mengi.
 
Tandahimba kuko vizuri?
Sijafika.
Mtwara naijua city center, Masasi , Nanyumbu.
Lindi naijua Lindi municipal, Lindi vijijini, Liwale, Kilwa. Rwangwa siijui
 
Back
Top Bottom