BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Nimetazama video hii ya Habarika24 TV ikanikumbusha nilipowahi kufika kwenye hiki Kijiji cha Madaha Wilayani Chemba Mkoani Dodoma na vingine kadhaa vya jirani nilipoenda kwa ajili ya shughuli zangu binafsi.
Nilikuwa na mwenyeji wangu ambaye alinieleza kuwa changamoto hiyo ni ya kawaida kwao, kwa kweli Wananachi wa vijiji vya huko wana hali ngumu na Serikali inatakiwa kuwajibika kwani wanaoteseka kwa asilimia kubwa ni Wana wake na Watoto ambao wanateseka kutafuta maji.
Wengi wao wanasema kuwa maji wanayapata porini ambapo kukutana na Wanyama mbalimbali ni jambo la kawaida kitu ambacho ni hatari kwa usalama wao, pia kukosa maji salama kiafya si salama.