Serikali iwatambue madalali na kuweka mazingira sahihi ya wao kufanya biashara, ongezeko la vijana wenye tatizo la afya ya akili ni kubwa

Serikali iwatambue madalali na kuweka mazingira sahihi ya wao kufanya biashara, ongezeko la vijana wenye tatizo la afya ya akili ni kubwa

Tsh

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2021
Posts
17,022
Reaction score
36,936
Kuna Kijana kwenye page yake kapost gari na specifications zote, kaweka bei na maelekezo kuwa punguzo lipo.

Kapigiwa simu na mtu anayelihitaji gari akatoa maelekezo kuwa gari ni la mtu wake wa karibu anamsaidia kuuza hivyo afuatwe eneo alipo waende kwenye gari likaguliwe likipendwa yeye ataongea na mmiliki ili biashara ifanyike, watu wakamfata.

Walipofika kijana kumbe anatafuta riziki kwa kufanya udalali, akampigia mwenzake anamuuliza gari lilipo, mwenzake naye akatoa maelekezo wapi pa kumkuta ili waende kwenye gari.

Kijana akaulizwa hili gari unalifahamu? Akasema gari kali balaa, nalijua nje ndani pale ukinunua umepata gari. Akaulizwa sasa mbona hujui hata lilipo unampigia simu mwingine akuelekeze akajibu mm hii wiki nilibanwa kidogo hivyo gari kuna mtu tulimpa atafute mteja na funguo anazo yeye sasa naye tangu saa mbili namwambia awe karibu lakini shida naye mambo meengi hatulii mara yupo huku mara kule, watu wakaridhika na majibu wakamfuata huyo mtu.

Walipofika na yeye akawa hana gari, akaulizwa gari lipo wapi akasema ngoja kuna mtu anakuja hapa chap tunalifata muwe na subira lilienda kwa mteja anakuja chap........

Dakika zikapita hakuna mtu, masaa yakapita hakuna mtu na mtu aliyekuwa anapigiwa ili gari lionekane akawa hapatikani tena.....

Ikabidi wanunuzi wajitambulishe kuwa wao ni Askari polisi na hilo gari linatafutwa lina kesi na watalazimika kwenda kituoni kutoa maelezo, hapo ndo kijana anaanza kulia lia kuwa yeye ni dalali tu halijui hilo gari, hizo picha kaziokota kwenye group maelezo mengiii akaambiwa usiongee sana utajitetea sana tu kwa afisa upelelezi yeye na mwenzie wakatiwa pingu tayari kwa safari ambayo kutoka kunategemeana na upelelezi utakaporuhusu kuwa hawahusiki na jinai iliyohusisha hilo gari wanalouza.

Sasa hoja yangu hapa ni kijana wa miaka 35 na kuendelea unapost vipi chombo cha mtu mwingine mitandaoni kuwa kinauzwa, unapigiwa simu unasema unafahamu kila kitu kuhusu hicho chombo ilihali hujui lolote na wala mmiliki humfahamu? Angalau si ujihakikishie tu kuwa kile unachofanya na ulichokitangaza kwa identity yako ni sahihi na salama?

Halafu hata kama kusingekuwa na jinai unaruhusu vipi mteja akufikie ulipo kabla wewe hujajihakikishia kuwa una access na alichokifata mteja?

Mteja anafika unaanza kuzunguka nae kumtafuta mwenzako ambaye naye anawaunga mkono kwa kumtafuta anayejua gari lilipo badala mngepeana taarifa ndipo mteja ukamruhusu akufuate. Kama sio kuchanganyikiwa ni nn?.

Kama taifa serikali inabidi ipitie hizi ajira zisizo rasmi zirasimishwe kinyume na hapo taifa litakuwa na vijana wa ajabu.
 
NAOMBA NIPEWE TOFAUTI KATI YA DALALI NA TAPELI
Nafikiri Dalali ni mtu anayeuza information na tapeli ni mwizi asiyetumia silaha au nguvu badala yake anakulaghai.
Ila kwa hawa madalali wetu wanavyofanya nadhani ni mix ya utapeli na udalali.
 
Back
Top Bottom