kiu ya haki
Senior Member
- Jul 17, 2015
- 103
- 55
Natanguliza salamu ya Amani na upendo wangu kwenu wote pia nawasalimu kwa jina la jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Baadhi ya viongozi wamekuwa wakisema vijana waliosoma wachangamkie fursa za kujiajiri kwa kulima ,kufuga kuku,kuuza machungwa na biashara nyinginezo ili waweze kujiajiri na kujikimu kimaisha kuliko kuihitaji serikali kuwaajili.
Tunashukuru kwa kumpata mama ambaye katika hutuba zake amejichanganua kuumizwa na swala la ukosefu wa ajira kwa vijana na kuumizwa na kauli za baadhi ya watu wanaosema vijana wajiajiri hali yakuwa kujiajiri kuna mchakato mgumu kwa vijana walio maliza chuo ,najua kuna watu wanaweza kusema “tumia elimu yako kujikwamua”.
Taasisi nyingi za Serikali zina utaratibu wa kuwapa vijana nafazi za mafunzo kwa njia za vittendo(Internship) ambazo zimekuwa na ushindani mkubwa sana kwani unaweza kukuta kada moja wametangaza nafasi moja au mbili lakini waombaji wake wakafika hata mia nane au elfu moja.
Tasisi kama TRA,TRC,TASAC,TPA,TAA ,TBS na kadhalika wanautaratibu huo ambao kwa kweli ni mzuri katika kuwaandaa vijana wetu kujijengea uzoefu wa kazi na ujuzi.
Mimi kama mdau wa maendeleo ya watu katika zama hizi ambazo raisi kajipambanua kuwasaidia vijana katika swala la ajira naomba serikali ipite katika taasisi hizo na kuhakikisha hawa vijana wanaajiriwa pindi wanapomaliza mafunzo yao kwa sababu zifuatazo.
1.Wamepita katika usaili wenye ushindani mkubwa katika kupata nafasi hizo.
2. Wanasifa na haki zote zinazostahili kuajiriwa.
3. Wana uzoefu na shughuli za taasisi husika hivyo hata wakiajiriwa hawatahitaji msaada sana wa kuelekezwa majukumu ya kufanya tofauti na mtu ambaye hajawahi kushughulika na majukumu ya sehemu hiyo.
4. Japo ni utaratibu wa kutoa fursa kwa wengine ili wajifunze bado haiathiri kuwaajiri waliomaliza mafunzo yao kwani wanaopewa fursa hizo ni 1 2,au 3 katika mamia na maelfu.
Naiomba serikali katika mchakato wao wa kuwaangalia vijana wawape vipaumbele hawa vijana na pia wengine wapewe fursa za ajira na tuepukane na kupigia upatu kujiajiri hali ya kuwa wewe unaesema hivyo umeajiriwa na hata ukiambiwa umpishe mwingine wewe ukajiajiri kama kujiajiri ni dili hauko tayari kufanya hivyo.
Nb: Sipingi suala la watu kujiajiri.