Serikali iwe makini, isikurupuke kurudisha mtandao wa intaneti

Serikali iwe makini, isikurupuke kurudisha mtandao wa intaneti

Hii nchi ina maadui wengi sana wa kiuchumi na kisiasa ambao hawaitakii mema. Hivyo serikali iwe makini...
Kikulacho, ki nguoni mwako.....haoa wasaliti ni wana harakati wetu fake pamoja na kina Lissu, Zitto, na wapuuzi wengine. Serikali isiwafumbie macho hawa watu.
 
Nampa mfano mmoja huyo mjinga, mimi niko inje ya Tanzania hununua bidhaa zangu kaliako kwa oline. Yaani wenye maduka Wanarusha mizigo kwenye whatsaap unachagua anakupa bei unamtumia hera kwenye mpesa anakutumia mzigo, mpaka sasa hivi hatuwapati huoni hiyo ni hasara.
 
Mpaka Naamini Meza Ya Duara Ni Muhimu Kuliko Kuzima Internet, Watu Mpaka Sasa Hivi Wameshaamka Muda Wanatumia Internet Bila Kujari Wamezima!

Hii Technology Inatisha Mno, Maana Huyu Jamaa UFO VPN Basic Ndiyo Tishio Kila Mtu Anayo
 
Hii nchi ina maadui wengi sana wa kiuchumi na kisiasa ambao hawaitakii mema. Hivyo serikali iwe makini...

Wanaoumia sasa hivi sio serikali, ni wananchi ambao biashara zinategemea mitandao. Muda ambao internet imefungwa imeshacost wananchi mabilioni ya pesa.

Kama hujui udukuzi unavyofanyika usijifanye mtaalamu, kaa pembeni kabisa

Shenzi mwingine. Next
 
Hanijui, uzalendo na mapenzi kwa taifa langu ndio maana nasema ukweli.

Mkuu, sio lazima uwe kilaza ili kuonekana ni mzalendo. Hao maadui mnaopigana nao ni nadharia tu! Kiuhalisia hakuna adui mnapigana nae. Mmeshindwa kushindana nao sasa mnawaita maadui huku mkisibiria misaada na mikopo nk!

Uzalendo si kuwa mjinga au kuikumbatia kale. Sasa hivi nchi haiwezi kuendeshwa kama miaka ya 1980!

Muda wa “work harder” umekwisha, sasa ni “work smarter” na kwa kuwa hamko smart mnadhani watu smart ni maadui!
 
Tanganyika ipi unaisema? Adui wa kwanza ni wewe kibaraka wa mabeberu.
Biashara za kuuza kupitia mtandao bongo? Nyumba hazijapangiliwa na hao ndio huwa wa kwanza huko uswahilini kuuana kwa kusiliza uongo wa kwenye mitandao.

Kusoma kwa kutumia internet ni uvivu wa kusoma vitabu ndio maana ubongo wako unawaza uharo
Pathetic
 
Dah Tanzania yaani mpaka vijana wa leo anakuja na propaganda zile zile za 70's na 80's eti tuna rasimali nyingi tunaonewa wivu. Hizo rasimali nyingi zinetusaidia nini mpaka sasa hivi? Vijana tubadilike aisee... kwa mwendo huu si ajabu na wajukuu zetu wakakuta ngonjera hizi hizi na maendeleo hakuna.
 
[emoji26] maskini nchi yangu!
Inazidi kuzalisha vijana wabinafsi, wajinga na wapumbavu
Mtoa maada ungekua kwenye ukoo wetu tungekutandika viboko na tungechana vyeti vyako urudi kijijini.
 
Umesahau kuwa leseni nyingi zilifutwa na kuanzia 2017 ilitungwa sharia mpya ya madini? Hujui kampuni nyingi ziliondoka na sasa ndio zinakuja kivingine.

Unajua una maswali kama mtu ambae hata hajui kusoma na kuandika hawezi kuuliza. Unajua Usa wana reserve ya gold kiasi gani na kwa nini?

Leseni nyingine ndio ngapi? Narudia tena wanaochimba sasa hivi sio wazungu? Acha sababu za kulazimisha kwa uzalendo uchwara.
 
Mtoa mada hauoni Kama hii kuzima mitandao itaendelea kuua sector binafsi hasa makampuni ya simu ie Vodacom, Airtel etc.alafu ikifika muda wa kupeleka gawio wakisema wamepata hasara hamuwasikilizi
 
Kipi bora hiyo hasara ya vijisenti vyenu au usalama wa nchi?
Usalama upi unaoukusudia kama kweli hawo mnaowaita mabeberu wanashida na hayo unayoyazungumzia ya Internet wasiweze kuyafanikisha wakati shina liko kwao na wewe unatawi tu.?

Wakiamua hawanashida ya kumtumia mtu hata mmoja wakati kila kitu kikokwao watafanya tu. Au unaona hawawezi?
 
Biashara za kuuza kupitia mtandao bongo? Nyumba hazijapangiliwa na hao ndio huwa wa kwanza huko uswahilini kuuana kwa kusiliza uongo wa kwenye mitandao.

Kusoma kwa kutumia internet ni uvivu wa kusoma vitabu ndio maana ubongo wako unawaza uharo
Kama hujiwezi kufanya miamala online usidhani wote ni pompoma kama wewe. Unashabikia kufungwa mitandao lkn nakuona hapa upo bize na VPN. Watu matatizo gani kichwani lkn??
 
Sheria inasemaje?
Serikali inakubalia na hilo kwasababu ni sheria tayari.View attachment 1621302
IMG_20201018_161556.jpg
 
Back
Top Bottom