Ndugu yangu Idugunde
Sipendi kupinga wazo lako ila nimeona nichukue nafasi hii kutoa elimu kidogo kutofautisha baadhi ya mamboi.Watu wengi wamekupinga najua lakini kibinadamu hakuna mtu mwenye weledi wa kila jambo katika nyanza za taaluma mbali mbali basi inapotokea hivyo ni vizuri kuelimishana mfano mtaalamu wa umeme akifika hospitali anakuwa mpole anakutana na mtaalamu wa fani nyingine ya daktari ambayo yeye haijui.
Ni vyema busara kutumika kumuelewesha mwenzio kwa lugha ya staha bila kutumia maneno machafu na matusi.
Kwa kuanza tuanze na maana ya neno internet kwanza nitaweka kwa kiingereza.
Internet is the global system of interconnected computer networks that uses the
Internet protocol suite (TCP/IP) to communicate between networks and devices.
Ngoja nitoe maana rahisi Zaidi inayoeleweka internet ni sawa sawa na wewe chukulia uko juu angani unaichungulia dunia kwa chini unaiona yote halafu chini unaona barabara zote dunia nzima barabara kubwa zote na za mitaani,vitongoji na zote zimeunganishwa kwa pamoja zile kubwa na ndogo ndogo za mitaani kwa maana hiyo unaweza kutoka ya mtaani labda uko dar ukaenda barabara nyingine ya mtaani au kubwa iliyoko Marekani sasa hiyo ni sawa sawa na internet sasa katika masual ya mawasiliano na mengineyo.
Tuendelee sasa katika barabara hizo zilizounganishwa sasa unaona kila sehemu ilikopita kwenye vituo flani unaona na nyumba zote kabisa dunia nzima.Sasa hizo nyumba unazoona ni sawa sawa na tunavyosema websites yaani vituo.Sasa vile ni dunia nzima zile nyumba zinaitwa WWW yaani World Wide Web Web ni neno kwa Kiswahili utando wa buibui ulivyo kaa na hizo nyumba ziko hivyo.
Katika hizo barabara sasa utategemea lazima utaona magari yanapita na kurudi sehemu moja kwenda nyingine sasa hayo magari ndio mfano wa data wewe unazotuma kutoka kituo kimoja kwenda kingine.
Turudi kwenye zile web zetu au nyumba zetu.Humo ndani ya nyumba lazima utategemea kuna watu na vitu tuongelee vitu sasa kila nyumba inategemea kumewekwa vitu gani utakuta kuna makochi,vitanda,sufuria,vijiko,mapanya,nzi,mbu,meza n.k. Hivyo nilivotaja sasa tuvitafsiri ki electroni ndio unakuta kuna mitandao ya jamii Facebook,nyumba zingine utakuta instagram,whatsup,snapshot,linkeIn,jamii forum hii tunayotumia mimi na wewe sasa hizi ni mitandao ya kijamii sasa kuna mitandao ambayo mingine sio ya kijamii ni ki biashara mfano mambo ya bank CRDB,NMB,mawasiliano ya television,taarifa za usafiri wa anga,mambo ya masomo,taarifa za ki inteligensia na kijeshi ila hizi zina njia zake maalum zinalindwa nadhani imeeleweka sasa.
Ni muunganiko wa computer,simu na vingine kote duniani kwa kutumia njia maalum kuwasiliana na masuala mbali mbali.Kwa maana hiyo basi internet ni kitu kikubwa mno kuliko mtu anavyoweza kudhania wewe.Dunia ya sasa kila kitu ni internet wewe unapokwenda kuchukua hela kwenye ATM unatumia internet na ndio maana wakati mwingine ukienda unasikia leo ATM haitoi hela wanasema hakuna mtandao yaani hakuna mawasiliano na server ya DSM kama uko mikoani.
Unapoagiza gari lako wewe ukiwa umekaa nyumbani kwako kwenye kochi kutoka Japan au Singapore kwa kutumia simu yako au computer na ukaja kuletewa mlangoni kinachotumika hapo ni internet.Unapoangalia taarifa ya habari ya CNN au TBC1 kinachotumika ni internet.Unapotoa hela kutumia Simbanking hela ziko bank wewe unavuta kwenye simu hiyo ni internet unaweza kuwa umekaa kwenye bar ukavuta hela bank zikaja kwenye simu yako ukalipa bila kunyanyuka.Zamani huwezi chukulia hela tawi lingine hadi uchukulie kwenye tawi lako.Sasa unaweza chukua hela sehemu yeyote uliyoko hata nje ya nchi hiyo ni internernet.Unapoongea na mtu yuko Marekani hata kama ni landline ukweli ni kwamba internet kuna mahali inatumika kuwasiliana na satellites zilizo angani umbali wa hata km 10,000 kutoka duniani kukupelekea sauti yako.Satellite za angani zote ni internet.
Unaweza ukafanya teleconference yaani mkafanya mkutano au kikao cha harusi na watu walioko Marekani hata kundi la watu kumi kwa kutumia computer bila kuonana hiyo ni internet.Unaweza ukapata elimu inaitwa Online mwalimu akiwa Marekani wewe uko nchi nyingine uka sikiliza anavotoa lecture wewe siku ya kufanya mtihani ukaenda tu kituo kilicho karibu ukafanya mtihani ukafaulu ukapata shahada yako.Unaweza ukafanya e-commerce ukiwa nyumbani kwako.Tunakoelekea na tayari kwenye simu zetu kuna application hizo simu yako ina uwezo wa kukupima joto la mwili wako hata na pressure itafika mahali hata damu ikagundua una malaria au kisukari ukawa huna haja ya kwenda hospitali ukajibiwa tu utumie dawa gani.Kuna operation ilifanyika hivi karibuni India daktari alimfanyia upasuaji mgonjwa bila kumgusa kwa kutumia mtandao huu huu wa internet.Computer yako inaweza kuingiwa virusi au ikaharibika software sio hardware mtu aliyeko Marekani ukampa access zako akaingia au akakuambia zip hilo file nitumie ukamtumia akali fanyia repair akakurudishia computer ikawa sawa.Ticket ya ndege huna haja ya kwenda kukata unakatia kwenye simu wewe unakwenda tu airport kusafiri.Mifumo yote ya kwenda anga za juu na usafiri duniani zinaongozwa na internet.Kuna baadhi ya simu zina kitu kinaitwa Infrared camera yaani camera yenye uwezo wa kumpiga picha mtu akiwa gizani.mfano mnamfukuza mwizi kajificha kichakani wewe una uwezo wa kumuona.Siku hizi ukienda kanisani padre sio lazima abebe biblia anakuwa na tablet anasoma anachotaka kwenye screen.Siku hizi sio lazima uende maktaba unaweza ukaagiza kitabu flani kiko marekani ukurasa flani ukakujia ukausoma ilimradi tu ujue ISBN—Internationa System Book Number unafuata maelekezo utaona hicho kitabu unaweza ku request usome wapi nadhani kuna malipo masuala kama haya.
Mfano kama una google hapo fungua andika maneno haya ISBN 978-92-5-105411-6 kisha enter utakuwa umefungua kitabu cha FAO Shirika la Chakula Duniani catalogue ya mwaka huu March 2020. Ukisoma Zaidi kuna mahali wanaongelea sheria na kanuni za kimataifa za namna ya usambazaji wa madawa ya kuulia wadudu bila kumdhuru binadamu.
Unaonaaaa!!!!!???? Internet ni dude kubwa mno na pana na vigumu kuliepuka.Wenzetu wakikimbia walau kama hatuwezi angalau tutembee sio tusimame hatuwezi kusema kuwa mambo haya hapana tutakuwa tunarudi kwenye ule ujima wa kuwasha moto kwa kusugua sugua vijiti badala ya kutumia kibiriti.
Sasa tuje upande mwingine wa shillingi mitandao ya kijamii.Ijulikane mitandao ya kijamii imebebwa na Internet iko ndani ya zile nyumba nilizosema awali kama nilivyo toa mifano hapo juu.Sasa mitandao hii ina faida zake na pia kuna matumizi mabaya yake
What are the dangerous of social media?
Cyberbullying (bullying using digital technology) invasion of privacy. identity theft. your child seeing offensive images and messages.
Sitatafsiri hapo najua kila anayesoma hiyo pamoja na wewe mnajua lugha ila naongezea mimi kitu kimoja kumchafulia mtu jina,kuweka habari za uongo ambazo zinaweza leta uchochezi au uvunjifu wa Amani katika sehemu flani kitaifa au kimataifa kuharibu watoto wadogo kuangalia picha za ngono.
Hapo juu nilisema kwenye zile nyumba za ile mitaa ndani kuna vitu mbali mbali nimevitaja kuna mahali nimetamka neno mapanya hapa mapanya namanisha katika hizo web Sites zingine zinakuwa hazitumiwi ipasavyo hazitumiki kwa manufaa ya jamii au kimataifa na hao mapanya sasa wako ndani ya hizo website.Inapofikia hatua hatarishi ndio sasa mamlaka husikia zinaweza kuamua kuingilia kati aidha kuzifunga kwa muda flani au moja kwa moja au ndio maana kila nchi ikaweka chombo maalum cha kufuatilia vitu kama hivyo kulingana na dunia inavyokwenda kasi ki teknolojia.
Serikali kiukweli zina uwezo wa kufunga yote niliyotaja ila kusema kufunga internet moja kwa moja inajua madhara yake hata kwa upande wake yenyewe.Watu wengi wanafikiria internet ni email peke yake au mitandao ya kijamii mitando ya kijamii iko ndani ya internet.Serikali ina uwezo wa kudhibiti baadhi ya mambo inayoona hatarishi kama internet zilifungwa mbona mabenki hela zilikuwa zinatoka?.Serikali na sio serikali tu hata katika organization walio na intranet hapa sijasema internet mfano chukulia kampuni kubwa kama ya Mohamed Enterprises anaweza akawa na intranet kwa ajili ya kampuni yake tu na akawa na server yake kubwa kwa ajili ya kampuni yake tu sasa anao uwezo pia
View attachment 1621449 kudhibiti matumizi kwenye computer za kampuni yake watu wasifungue kitu flani au mfano ukitaka kutuma attachment ya file au picha labda lisizidi ukubwa flani mfano mwisho 4MB ikitokea hivo file haliendi au likienda likikutana na server iliyowekewa restrictions kule linakofikie lisifunguke kwa muda huo labda baadae.Ila hiyo server yake lazima na yenyewe inapitia kwenye server husika kubwa.
Angalia picha nilivyoambatisha ya internet kidunia uone sio jambo dogo.Hivyo kama vitaa ndio zile nyumba nilizosema hiyo mistari ndio internet yenyewe sasa muunganiko dunia nzima vinavopita kwenye hiyo mistari au barabara ndio data unazotuma wewe sasa zinaposafiri humo kweye vitaa au nyumba ndio websites zilipo mbali mbali na mitandao ya kijamii na taarifa zako mfano za crdb