Serikali iweke ration kwa walimu pia

Serikali iweke ration kwa walimu pia

NJALI

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2014
Posts
1,534
Reaction score
1,090
ifahamike kwamba kila kigogo alie ofisini amefika hapo alipo pamoja na mambo mengine ni kufundishwa na walimu kuanzia chekechea hadi elimu aliyo ishia kigogo huyo. cha kushangaza mwalimu bado haheshimiwi, analipwa pesa kiduchu, hana nyumba, hana masurufu, anasomesha, anategemewa pamoja na matatizo chungunzima yanayo mkabili mwalimu. ningeomba serikali sikivu kama inavyo jiita, ikampa mwalimu posho ya kati kati ya mwezi yaani ration, ambayo iwe tofauti na mshahara kama ilivyo kwa maafande. hii itamsaidia mwl kulipia pango,umeme na maji, pia itapunguza ukali wa maisha kwa mwl hasa wa s/misingi na sekondari. vigogo wa elimu hasa waziri, katibu mkuu na kamishna wa elimu, uzi huu mki usoma ufanyieni kazi, sikuwa na njia muafaka ya kufikisha maombi yangu kwenu ila kupitia mtandao pendwa huu.
 
Wanasikia Ila wanaishia hapo hapo kwenye kusikia, kutenda ni zero
 
kwani afande anaripwa sh.ngapi na mwalimu sh.ngapi? Lets say wote ni wa bachelor mwlm ana degree yake ya education na afande ana degree ya law enforcement?.
 
Mkuu wala usipate tabu kuwambia haya, oluochi amewambia haya bungeni wameishia kumzomea, sisi tunachokifanya saiz ni kuandaa bomu, siku tukilipua wataomba poo
 
Ila inauma, walimu liangalie hili swala kwa mtazamo wa kina, mkiamua haya yanawezeka.
Mwalimu ana uwezo wa kufanya taifa liwe sikivu ama kinyume chake mbele ya serikali pia anaweza kuandaa kizazi kinachotaka kujenga au kubomoa na kuharibu kabisa taifa, Serikali ikiwa na malengo ya muda mrefu kuna haja ya kulitilia maanani suala la walimu lakin kama kila mtu atajali familia yake ipo siku kila familia itakua serikali na mwenye mabavu ndiye atakayedumu Tanzaniani!!!!
 
kinacho jadiliwa hapa ni hoja kwamba walimu hawana allowance kama kazi zingine mfano TRA,BANK,SUMATRA,POLICE,JWTZ n.k. walimu wapewe posho japo laki moja katikati ya mwezi ili kuwapunguzia ukali wa maisha. vijiwe vikavu wauze chaki ?wauze mitihani ?wauze vitabu au samani za ofisi na madawati?
 
Tumewasikia,ila lileteni swala lenu ofisin kwetu kwa maandishi.over
 
Kazi kama hailipi unaachana nayo na kusoma unayodhani inalipa.

Kuanzia sasa hivi nimefuta rasmi cheti chako cha chekechea na matokeo ya muhula wa pili wa darasa la kwanza, utarudia ngazi uliyofutiwa cheti na kila ukibeba biskut nitakunyang'anya nampa kuku wangu kwasababu sijazalisha bado. Ukome kuchezea waliokufundisha adabu ya kula na kuamkia na kuimba hadi leo unajiona una haki ya kuandika ushenzi hapa.
 
Tumewasikia,ila lileteni swala lenu ofisin kwetu kwa maandishi.over

Huna sifa ya kujibu huu uzi, kwasababu wenye uwezo saa ulizopost wanakuwa baa wanaangalia vimini na kutusahau wachapakazi. Kaa pembeni usinitie hasira nina mamlaka ya kufuta matokeo ya chekechea na ya mihula maana ndiyo nayashughulikia.
 
-WALIMU watu wenye madeni mitaani,madukani,kwenye vilabu vya mataputapu,
-WALIMU watumishi wa umma wenye mikopo kila taasisi ya kifedha
-WALIMU walevi wa bia kwa siku 5 za mwanzo wa mwezi baadae wanarudia mataputapu
-WALIMU watu wasiojitambua
IT BE CONTINUED
 
Na mshahara wake atafanyia nini?
Sasa wa mwanajeshi anafanyia nini? Ushawahi kuwauliza wanajeshi hilo swali? Acheni unafiki kwa kazi za wenzenu. Kazi ile ni ngmu na isitoshe wewe si mwalimu. Wanajeshi wana panda magari bure, wana supermarkets zao wananunua vitu kwa bei nafuu kabisa, mikopo riba nafuu sana na isitoshe hawalipi mkopo wa elimu ya juu kama kada zingine, wake zao na watoto wao wanapewa posho kila mwezi. Je, mwalimu akipewa ration tu kwako ni nongwa?
 
-WALIMU watu wenye madeni mitaani,madukani,kwenye vilabu vya mataputapu,
-WALIMU watumishi wa umma wenye mikopo kila taasisi ya kifedha
-WALIMU walevi wa bia kwa siku 5 za mwanzo wa mwezi baadae wanarudia mataputapu
-WALIMU watu wasiojitambua
IT BE CONTINUED
Also a JF GT
 
Siku zote hua naumia vile walimu wanakuwa treated..hawana posho na madaraja yao yanacheleweshwa sana na kwa mfano leo kigoma vijjn walimu wamefunga ofisi ya mkurugenzi wao kisa madaraja na yapo mengi sana ambayo walimu wanafanyiwa ndvyo sivyo lkn wako kimya...
 
Sasa wa mwanajeshi anafanyia nini? Ushawahi kuwauliza wanajeshi hilo swali? Acheni unafiki kwa kazi za wenzenu. Kazi ile ni ngmu na isitoshe wewe si mwalimu. Wanajeshi wana panda magari bure, wana supermarkets zao wananunua vitu kwa bei nafuu kabisa, mikopo riba nafuu sana na isitoshe hawalipi mkopo wa elimu ya juu kama kada zingine, wake zao na watoto wao wanapewa posho kila mwezi. Je, mwalimu akipewa ration tu kwako ni nongwa?

just relax my friend, wanajeshi na wafanyakazi wengine terms zao ni tofauti sana. wanajeshi wako "enrolled" na walimu wameajiriwa. na potential risk ni tofauti
 
Back
Top Bottom