ifahamike kwamba kila kigogo alie ofisini amefika hapo alipo pamoja na mambo mengine ni kufundishwa na walimu kuanzia chekechea hadi elimu aliyo ishia kigogo huyo. cha kushangaza mwalimu bado haheshimiwi, analipwa pesa kiduchu, hana nyumba, hana masurufu, anasomesha, anategemewa pamoja na matatizo chungunzima yanayo mkabili mwalimu. ningeomba serikali sikivu kama inavyo jiita, ikampa mwalimu posho ya kati kati ya mwezi yaani ration, ambayo iwe tofauti na mshahara kama ilivyo kwa maafande. hii itamsaidia mwl kulipia pango,umeme na maji, pia itapunguza ukali wa maisha kwa mwl hasa wa s/misingi na sekondari. vigogo wa elimu hasa waziri, katibu mkuu na kamishna wa elimu, uzi huu mki usoma ufanyieni kazi, sikuwa na njia muafaka ya kufikisha maombi yangu kwenu ila kupitia mtandao pendwa huu.