Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Kwa kumbukumbu zangu, katika barua yake kwa wizara, idara na taasisi za serikali, Katibu Mkuu Utumishi aliwagiza wahusika kuwa ifikapo June 10 mwaka huu, wawe wamewassilisha serikalini orodha ya watumishi wanaostahili kupanda vyeo katika mwaka huu wa 2021.
Hivyo, ili kuwapa watumishi fursa ya kuhakiki orodha hiyo ili kuondoa uwezekano wa baadhi ya watumishi kusahaulika, kurukuwa na hata kufanyiwa mizengwe, nashauri serikali iweke wazi hiyo orodha na itoe nafasi kwa watumishi kuwasilisha malalamiko iwapo wapo watakaona majina yao hayapo ingawa sifa wanazo.
Ukweli ni kwamba, haya yalipaswa kufanywa na idara na taasisi husika kabla ya kuwasilisha orodha hiyo Utumishi, ila sidhani kama jambo hili limefanyika na hata kama limefanyika limefanywa na kila idara na taasisi ya serikali.
Nashauri hivi ili kuondoa uwezekano wa kuja kuibuka malalamiko kutoka kwa watumishi wakilalamika kutopandishwa vyeo ili hali sifa walikuwa nazo na wakaishia kupewa majibu kama maswala yenu yanashughulikiwa au ni tatizo la system au ni matatizo tu ya kibinadamu, n.k, ila tunashgulikua.
Mambo ya serikalini tunayajua kwani ukikosa hii nafasi, unaweza kusubiri miaka mingine miwili, mitatu na hata zaidi ndio tatizo liwe limepatiwa ufumbuzi ingawa pia linaweza tatuliwa mapema (probability).
Tukumbuke watumishi hawa wamekaa miaka karibu sita bila kupata hizo promotion, sasa haitakuwa vyema mtu kukosa tena hii fursa.
Hivyo, ili kuepuka yote haya, ni bora hiyo orodha iwekwe wazi na serikali au serikali iziagize idara na taasisi zake kuweka wazi orodha hiyo kwa watumishi wake ili watumishi wahakiki majina yao kabla ya mchakato haujafika mwisho.
Lingine la msingi ni serikali au idara zake kuweka wazi sifa ambazo mtumishi anastahili ili aweze kupandishwa cheo. Hii ni kwasababu sifa hizi zimekuwa zikiorodheshwa tu ila pasipo kuwa na ufafanuzi wa kutosha, hivyo kuna uwezekano wa baadhi ya watumishi kutoelewa ni zipi hasa hizo sifa wanazostahili kuwa nazo ili wapande vyeo na matokeo yake watashindwa kudai haki zao..
Kwa mfano,hivi sasa mtumishi ili kupanda cheo, sifa mojawapo ni awe amekaa katika cheo kimoja kwa miaka minne.Sasa swali litakuja; je, ni miaka minne mfululizo au mradi itimie miaka minne bila kujali kuna kipindi mtumishi hakuwa kazini mfano alikuwa masomoni?
Wahusika tunaonba haya myafanyie kazi mapema iwezekanavyo ili kuwaondolea watumishi adha zisizo za lazima na pia ili kutowachanganisha watumishi na serikali yao.
CHADEMA,ACT na vyama vingine vya upinzani, baada ya serikali kutamka kuwa itawapandisha vyeo watumishi, nyinyi mnapaswa kubeba agenda hiyo kwa kuongelea mambo haya kama ambayo mimi nimeongea hapa au kwa namna mtavyoona inafaa kwani mna nguvu na ndio kazi yenu na ndio siasa yenyewe.