tatizo kubwa la watumishi wa umaa wanapigana "PINI" wao kwa wao, chuki,wivu, majungu na fitina kibao, mnaharibiana sana, hawapendani wao kwa wao, wanachongena ubenya sana!!
sasa mbaya zaidi ukikuta boss naye chaumbeya basi hapo huna chako utabaki kula vumbi labda itokee miujiza ya Mungu.
na katika hili viongozi kuanzia Mhe. waziri, naibu waziri, katibu mkuu na watendaji wote wa wizara ya Utumishi wa Umma wawe makini sana tena sana,
kuna uonevu mkubwa unao endelea ndani kwa ndani, , kuna baadhi yabwatumishinwamepigwa PINI za maksudi tu ili mtu asisogee mbele lkn ukimchunguza mtumishi huge utakuta ni mchapa kazi na muadilifu lkn zengwe limeundwa IPO kumpiga PINI asipande.
chunguzeni tatueni kero haswa kwa wale wasio kuwa na mtu wa kuwasaidia yaani godfather, sioni kama tabia ya kuwa na godfather ni jambo la kuachiliwa liendelee ktk mifumo yetu, hapa! watu wato watumishi wote watendewe haki sawa. kamwe kusiwe na matabaka ktk utumishi wa umma, kwa kufanya hivyo mtajenga imani kwa wananchi.
hakikisheni anayestahili anapewa haki yake bila kuwekewe pini au zengwe.
Upatikanaji wa haki za wananchi unaanzia kwa watumishi wao kwa wao kutendeana Haki ndipo na sisi wananchi tutapata haki, kinyume chake hakuna haki.
Rais wetu Mpendwa mama Samia anataka kuona Haki ikitamalaki, hataki kuona UONEVU/UNYANYASAJI na upendeleo au kujuana.
acheni kutoa kadi nyekudu ovyo ovya, waleeni watumishi walio chini yenu badala ya kuwagawa, wajengeeni uwezo badala ya kuwaharibu.
wapo viongozi wenye roho mbaya sana ambao wanapenda kuwaharibia kazi walio chini yao kwa maksudi tu au chuki binafsi, mizengwe mizengwe mizengwe na chuki
uonevu, uonevu, uonevu ndicho huwa kinatendaka ndani kwa ndani, viongozi wana waonea sana watumishi walio chini yao, kiongozi anaweza kuamua tu kwa hila kumharibia aliye chini yake hiyo ndio tabia iliyo kithiri ndani kwa ndani na bahati mbaya hakuna wa kuwatetea.
Waziri Mchengelwa safisha tabia hiyo ya uonevu mkubwa iliyo kithiri ndani ya utumishi wa umma.