Serikali iweke wazi orodha ya watumishi wanaostahili kupanda vyeo mwaka 2021

Oprah ukishaajaza huwa wanazitupia hapo chini hata hawashugulikia Chochote zikiihitajika tena wanakwambia upeleke , tena ili hali wao ndo wanazo halmashauri kuna kuna mafisa mtumishi ni vilaza sana
 
Mbona ili Jambo liko wazi ,labda katika Halmshauri yako Tu ,vyama vya wafanyakazi viko macho katika ili ,vinatembelea kila wiki Kwa maafsa Utumishi kuona zoezi linaendaje
Kabsaa mfano CWT Wana orodha ya majina kabsaa ya watumishi watakaopanda
 
Wakati mwengine kupanda cheo ni bahati tu.
Kunawatumishi nawafahamu wasiopungua watatu wanatumikia cheo chao cha sasa tangu January 2012.
Wazembe, mimi nikiwa chuo, kuna jamaa wao wanafundisha cha kushangaza nikapanda daraja mimi baada ya miaka minne, wao wakaachwa ingawa walinitangulia kuajiriwa. Huwezi Amin wale jamaa walipandishwa madaja Wizarani huko huko waligoma kufundisha wakaenda kueleza shida zao. Mwezi uliofuata wakapanda. Hii nchi usipojihanagikia mwenyewe unakufa masikini
 
Kiukweli hoja yako ina mashiko Sana. Kuna idara ya afya hapa sengerema imeacha kuwaweka kwenye orodha zaid ya watumishi 50 wa kada ya afya kupanda daraja mwaka huu. Kiukweli nimefuatilia nikaona mwenye tatizo ni katibu wa afya mwenye jukumu la kuchambua hayo majina. Ikitokea ana chuki na mtumishi yeyote lazima kadhia hiyo uipitie.
 
Hii nchi ngumu sana ndugu yangu. Hata hili nililoshauri walipaswa wao wenyewe wawe wameshalifanya. Kwa sasa wanasubiri malalamiko yaanze ndio wachukue hatua badala ya kuwa na mikakati ya kuzuia mambo kama haya yasotokee

Yaani wako reactive badala ya kuwa proactive.
 
Huku maofisini ukiwa mtu wa kuhoji vitu, ukiwa mtu wa kutaka haki utaitwa mkorofi na hutapewa kazi za za michongo ya hela hasa ukiwa na boss asiyejiamini
 
Mbona ili Jambo liko wazi ,labda katika Halmshauri yako Tu ,vyama vya wafanyakazi viko macho katika ili ,vinatembelea kila wiki Kwa maafsa Utumishi kuona zoezi linaendaje
Hivyo vyama vinasubiri hadi utemwe kwenye orodha uwafate ndio wanaanza kushughulikia usijidanganye kuwa wanafuatilia kila kitu. Mimi yalinikuta
 
Huku maofisini ukiwa mtu wa kuhoji vitu, ukiwa mtu wa kutaka haki utaitwa mkorofi na hutapewa kazi za za michongo ya hela hasa ukiwa na boss asiyejiamini
Umeongea ukweli mtupu. Yaani utachukiwa na kuonekana unajifanya mjuaji.
 
Huku maofisini ukiwa mtu wa kuhoji vitu, ukiwa mtu wa kutaka haki utaitwa mkorofi na hutapewa kazi za za michongo ya hela hasa ukiwa na boss asiyejiamini
True umesema yote wao hawataki watu wa Kuwa challenge
 
Aisee hili la opras Ni Bomu .Tumeandika opras Hadi tukataka kugemea ,,
 
Hakuna Haki bila Wajibu dogo. Kama unataka Daraja, JAZA OPRAS.
 
Maswala ya kitumishi ni siri.

Kama kuna mtumishi ataachwa ipo nafasi ya malalamiko.

Na kila mtumishi anajua kama anastahili kupanda ama la.
 

Ni taratibu za kitumishi miaka yote, wala hakuanza mwendazake.
Kama hukuwa na sifa njema kwenye opras usimlaumu mama.
 
Hizo opras mbona kila mwaka watumishi wanajaza? Sasa nini ambacho wanakitaka tena?Ukiona hivyo, ujue visngizio ndio vinaanza kama ilivyokuwa wakati wa Mwendazake alipokuja na kisingizio cha uhakika kabla ya kupandisha mishahara.

CCM ni shida!

Hakuna kisingizo

Opras ipo miaka yote
 
I strongly support you. Kuna takataka nyingi serikalini kitengo chs HR
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…