Deadline hiyo imetangazwa na Waziri wa Mazingira Suleimani Jafo.
Baada ya January 31, 2024 taasisi zote za Umma na Binafsi ni marufuku kupikia kwa kutumia mkaa na kuni.
Aidha Serikali imesema inataka kufikia 2030 Asilimia 80% ya Watanzania wote wawe wanatumia Nishati safi ya kupikia.
====
"Taasisi zote za Umma na Binafsi zinazopika chakula cha zaidi ya watu 100 itakapofika Januari 31,2024 taasisi hizo zinatakiwa kusititisha matumizi ya kuni na mkaa kwa ajili ya kupikia, lakini taasisi zile ambazo zina watu zaidi ya 300 itakapofika Januari 31, 2025 zisitishe matumizi ya kuni na mkaa watumie nishati mbadala" - Dkt. Selemani Jafo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).