Serikali kitengo cha TEHAMA: Kwanini mifumo yenu mingi ya online/kimtandao inasumbua sana tatizo ni wataalam au vifaa duni?

polokwane

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2018
Posts
3,361
Reaction score
5,842
Mifumo mingi ya serikali ikisha pata watumiaji wengi tayari inasumbua sana tena sana na kuna wakati haipatikani kabisa tatizo ni nini? vifaa duni au wataalamu wenu mlio nao huko hawana uwezo?

Yani unaweza kukuta vi websites binafsi tu vinawatumiaji karibu milion lakin viko haraka sana lakini mifumo ya serikali unaweza subiri hadi unachoka mfumo haufunguki. Mfano wa kwanza NECTA, halafu kuna mifumo mingi sana ya ELIMU na AFYA, MIFUMO YA BILI ni matatizo makubwa sana tu.

Hebu wahusika pitieni hilo yawezekana mnauziwa savers zilizo chini kabisa ya kiwango kwa bei ghali.
 
Kama unauliza majibu vile. Kama mitandao inasumbua basi wataalamu hawana uwezo. Wawape Wahindi hizo kazi wafanye kama outsource kule Bangalore.
 
Watalamu wapo Shida ipo kwa mfumo wa kuajiri kulingana na ubobezi wa hio taluma ndio haupo.
 
Bajeti za serikali ni za kijinga.

Unawaambia wanunue server kila moja usd 9000 lakini kinachofata wana kwambia nunua ya usd 2000 iliyobaki wanakula wenyewe.

Bajeti za kuhudumia mitandao ni wagumu.nimefanya nao kazi !

Pili ma IT wao ni wale watoto wa ndugu zao na hakuna la maana.

JF kungekuwa kuna space ninge mwaga mchele wote kuhusu upuuzi sekta ya tehama serikali
 
Watalamu wapo Shida ipo kwa mfumo wa kuajiri kulingana na ubobezi wa hio taluma ndio haupo.
Hao wataalamu umeziona wapi kazi zao? Maana unaweza kuwa msomi mzuri lakini ukiwekwa kwenye kazi inakushinda.
 
Mifumo mingi ya serikali ikisha pata watumiaji wengi tayari inasumbua sana tena sana na kuna wakati haipatikani kabisa tatizo ni nini? vifaa duni au wataalamu wenu mlio nao huko hawana uwezo?

Yani unaweza kukuta vi websites binafsi tu vinawatumiaji karibu milion lakin viko haraka sana lakini mifumo ya serikali unaweza subiri hadi unachoka mfumo haufunguki. Mfano wa kwanza NECTA, halafu kuna mifumo mingi sana ya ELIMU na AFYA ,MIFUMO YA BILI ni matatizo makubwa sana tu.

hebu wahusika pitieni hilo yawezekana mnauziwa savers zilizo chini kabisa ya kiwango kwa bei ghali.
Kuna mtaalam mmoja aliniambia kuwa tatizo kubwa ni wataalam kuingiliwa na wanasiasa kimaamuzi. Mfano alisema wataalam wanapendekeza ununuliwe mtambo wa Milioni kumi, lakini anakuja mwanasiasa ili tu apate sifa kwa wananchi analazimisha mtambo ununuliwe wa bei rahisi labda nusu yake. hiyo husababisha wataalam waende kuweka oda ya mitambo ya bei rahisi ambayo huwa haina uimara na wala haidumu muda mrefu
 
Hao wataalamu umeziona wapi kazi zao? Maana unaweza kuwa msomi mzuri lakini ukiwekwa kwenye kazi inakushinda.
Mkuu fanya research utagundua zipo nying tu!.
Sikatai kuna kundi kubwa la wasomi Ila kazi zinawashinda Ila wapo wenye uwezo nzuri na uhakika na hilo.
 
Kuna ile system ya inatumiwa na kufanya clearance ya mizigo bandarini au border za nchi kavu ni balaa. Unaweza kuambiwa system iko down siku nzima mpaka ushangae.
 
Mifumo mingi ya serikali ikisha pata watumiaji wengi tayari inasumbua sana tena sana na kuna wakati haipatikani kabisa tatizo ni nini? vifaa duni au wataalamu wenu mlio nao huko hawana uwezo?

Yani unaweza kukuta vi websites binafsi tu vinawatumiaji karibu milion lakin viko haraka sana lakini mifumo ya serikali unaweza subiri hadi unachoka mfumo haufunguki. Mfano wa kwanza NECTA, halafu kuna mifumo mingi sana ya ELIMU na AFYA ,MIFUMO YA BILI ni matatizo makubwa sana tu.

hebu wahusika pitieni hilo yawezekana mnauziwa savers zilizo chini kabisa ya kiwango kwa bei ghali.
Kweli tupu
 
bajeti za serikali ni za kijinga.
unawaambia wanunue server kila moja usd 9000 lakini kinachofata wana kwambia nunua ya usd 2000 iliyobaki wanakula wenyewe.

bajeti za kuhudumia mitandao ni wagumu.nimefanya nao kazi !

pili ma IT wao ni wale watoto wa ndugu zao na hakuna la maana.

JF kungekuwa kuna space ninge mwaga mchele wote kuhusu upuuzi sekta ya tehama serikali
Mwaga mchele mkuu space ipo ili wajirekebishe
 
Mtu akisha ajiriwa serikalini anakuwa mungu mtu. Anaweza kuacha kutatua tatizo ndani ya muda akaenda kunywa chai. Hakuna uwajibikaji
 
Watu wameagizwa wapige,huo muda wa kuhangaika na utopolo wa mifumo watapata wapi?🐒🐒🐒
 
Mtu akisha ajiriwa serikalini anakuwa mungu mtu. Anaweza kuacha kutatua tatizo ndani ya muda akaenda kunywa chai. Hakuna uwajibikaji
Pia conservatives wengi makazini hawataki kuakosolewa ukijidai mjuaji wanapita nawew unasubili muda wako ufike
 
Kazi nyingi za serikali zinafanywa kwa mazoea na siyo weredi. Unachosomea ni tofauti na unachokutana nacho. Mara nyingi unachokutana nacho si cha kitaalamu sanasana ni Cha mazoea. Kazi nyingi ndani ya serikali yetu unweza kujifunzia palepale na hazina uhusiano na kisomo chako. Ukileta usomi wako unafanyiwa zengwe unafukuzwa
 
Mifumo mingi ya serikali ikisha pata watumiaji wengi tayari inasumbua sana tena sana na kuna wakati haipatikani kabisa tatizo ni nini? vifaa duni au wataalamu wenu mlio nao huko hawana uwezo?
Kuna Kitu huwa kinatakiwa kifanyike kabla ya Ku-Launch mifumo kwenda "LIVE" kutoka "UAT" hiyo process inaitwa Stress Testing, mifumo mingi ya huko bongo huwa haifanyiwi hii kitu nimekaa huko kwenya mbaadhi ya sekta mfumo ukishatengenezwa kabla hata ya Quality testing tayari uko Live.

Stress testing inasaidia sana hasa kwenye kufahamu Kama kutakuwa na Concurrent connection 20 thousand wahat will happen.

Lakini stress testing huwa inafanyika kisasa pia.
 
Yaani wanatia kinyaaa mifumo yao ya hovyo sana halafu wanataka kwenda Kitehama

Huvi muhusika mkuu wa hii sekta ninani na ipo chini ya nani ? Huyi ni NAPE huyu uzuri yupo humu afanyie kazi

Kuna mifumo mingi wameianzisha ni mizuri lakini perfomance ya hiyo mifumo utachoka.
 
Udhaifu na mapungufu katika mifumo ya TEHAMA ni manufaa kwa wapigaji na wazee wa michongo.
 
Serikali inajua kukamua maziwa na sio kulisha ng'ombe
 
Udhaifu na mapungufu katika mifumo ya TEHAMA ni manufaa kwa wapigaji na wazee wa michongo.
Hata ikiwa imara still inapigwa tu wabongo sio mbuzi wachungike.
Hakuna kitu cha hovyo cha kupigia kama mifumo.Mifumo yote wanapigia kwenye madhaifu yake.
 
Back
Top Bottom