Serikali kuajiri Zaidi ya walimu 35,000

Serikali kuajiri Zaidi ya walimu 35,000

Mnyakyegi

Member
Joined
Sep 12, 2014
Posts
81
Reaction score
21
Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Peter Pinda,amesema serikali imepanga mwaka huu kuajiri walimu zaidi ya 35,000 kwa ajili ya shule za sekondari ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa walimu nchini.

Ametoa kauli hiyo Jana (Alhamis) Tarehe 19 February 2015 wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Kiwere, mara baada ya kukagua ujenzi wa maabara na kuzindua nyumba nne za walimu kwenye shule ya Sekondari Kiwere, tarafa ya Kalenga wilaya ya Iringa.

Alisema pia walimu hao watasambazwa kulingana na mahitaji ya maeneo husika Lengo ni kuhakikisha kuwa uhaba wa walimu unapungua kutokana na kufahamika kuwa baadhi ya maeneo kuna uhaba mkubwa wa walimu hasa vijijini.

N.B: Ondoeni wazo la kusema ajira hakuna.

Source: Radio One



FRIDAY, FEBRUARY 20, 2015 SERIKALI KUAJIRI WALIMU 35,000 - WAZIRI MKUU WAZIRI MKUU

Mizengo Pinda amesema Serikali imepanga kuajiri walimu zaidi ya 35,000 kwa ajili ya shule za sekondari ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa walimu nchini.

Ametoa kauli hiyo jana jioni (Alhamisi, Februari 19, 2015) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa kata ya Kiwere, mara baada ya kukagua ujenzi wa maabara na kuzindua nyumba nne za walimu kwenye shule ya sekondari ya Kiwere, tarafa ya Kalenga, wilayani Iringa.

Waziri Mkuu alisema walimu hao watagawanywa kwenye shule kulingana na mahitaji yaliyokwishawasilishwa na kwamba watakapopata mgao wao hawana budi kuziangalia kwanza shule zenye miundombinu iliyokamilika kama ilivyo kwa shule hiyo. Akifafanua kuhusu kasi ya ujenzi wa maabara Waziri Mkuu alisema:

"Mkoa mzima wa Iringa unahitaji kuwa na maabara 318 na zilizo tayari mpaka sasa ni 108. Lakini kuna nyingine 141 ambazo zimekwishaanza kujengwa na zimefikia hatua nzuri. Nimeambiwa katika muda mfupi ujao kutakuwa na maabara 249 zilizokamilika," alisema. "

RC inabidi uwasukume watu wako ili hizi 69 ambazo bado hazijaanza kujengwa zikamilike kabla ya Juni mwaka huu kama ambavyo Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete alikuwa ameelekeza. Alisema hataongeza tena muda wa ujenzi," aliongeza.

Alisema elimu ni sekta ya msingi ambayo Serikali imeamua kuipa umuhimu wa kipekee na kuiweka katika moja ya maeneo sita muhimu ya kipaumbele chini ya Mpango wa Matokeo Makubwa ya Haraka (BRN).

Waziri Mkuu aliwataka wanafunzi wa shule hiyo wasome kwa bidii na wawe wasikivu ili waweze kufanya vizuri zaidi kwenye masomo yao.

Mapema, akitoa taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Afisa Elimu wa Wilaya ya Iringa, Bw. Leonard Msigwa alisema ujenzi wa nyumba hizo nne ambazo zina pande mbili (four duplex houses) umegharimu sh. milioni 323.2.

Alisema nyumba hizo zenye vyumba vitatu vya kulala, sebule na jiko, zina uwezo wa kubeba familia nane. Bw. Msigwa alisema ujenzi wa nyumba ulifanywa shirika la DESWOS la Ujerumani kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa pamoja na wananchi.

Pia walisaidiwa kujengewa tenki la maji na mabweni mawili yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 112 kila moja kwa ajili ya wasichana.

Akifafanua kuhusu hali ya ujenzi wa maabara, Afisa Elimu huyo alisema hadi sasa wamekamilisha ujenzi wa vyumba viwili vya Kemia na Baiolojia lakini bado viko kwenye hatua ya kupaka rangi. Alisema mfumo wa gesi na maji umekwishafungwa ndani ya vyumba vya maabara.

"Ujenzi wa maabara hadi sasa umekwishagharimu sh. milioni 52.8/- na katika kipindi cha Februari 2015, tumefanikiwa kutengeneza baadhi ya samani za maabara yaani meza 24 na stuli 96 zenye thamani ya sh. 8,940,000/-," alisema.

FRIDAY, FEBRUARY 20, 2015 ~ COPYRIGHT: MICHUZI BLOG ~ Pia waweza tafuta Magazeti ya Leo jumamosi 21/2/2015 MTANZANIA HALISI NA HABARI LEO YAMECHAPISHA HABARI HIII!!



 
Acha wasiwasi kijana. Unadhani tukiacha kukuajiri mwaka huu na jinsi ulivyopigika mtaani, utatupa kura yako kweli!
Wewe andaa nauli!
 
Ni kweli ajira za walimu wapya zimetokaa?
 
Sehemu yenye uitaji wa walimu ni vijijini so ukipelekwa uko uturie uijenge Tanzania
 
HAPA NAMNUKUU MHESHIMIWIWA KATIBU.


Walimu wa masomo ya Historia, Kiswahili, Civics, Geography wamejazana mashuleni. Serikali tumeamua kusitisha kuajiri walimu wa masomo haya kwa mwaka wa ajira 2015/16 ili kuweza kupunguza gharama za uendeshaji wa elimu hususan kwa kuwa ada ya elimu ya secondary imefutwa ambapo haitalipwa tena kuanzia mwakani.


SOURCE: UHAKIKA

Wewe kweli............ Huoni hats aibu kucoment, ngoja nikuulize ivi katibu mkuu na Waziri mkuu nani mwenye mamlaka, halafu huyo katibu mkuu ulimsikia wewe peke yako?

Pinda amezungumza akiwa katika shule ya sekondari Kiwere navyombo vya habari hususani magazeti ya Leo karibia yote yameandika iyo habari, wewe uyo katibu mkuu alikuwa akizungumzia wapi?

navyombo gani vya habari viliandika au alikwambia peke yako.Ndugu kabla ya kucoment uwe unafikiria sababu umetuonyesha ni jinsi gani ulivyo na uwezo mdogo Wa kufikiri
 
Back
Top Bottom