... nimeona lile tangazo la serikali lililosainiwa na Prof. Makubi, mganga mkuu wa serikali. Limejaribu kueleza hatua za kuchukua katika maeneo mbalimbali yenye misongamano ili kukabiliana na Uviko-19. Lakini ama kwa makusudi, kusahau, au kutokujua halijagusia chochote kuhusu misongomano mashuleni na vyuoni walau kutaja Shule na Vyuo halikufanya hivyo!
... Kama kuna maeneo yenye misongamano ya UHAKIKA basi ni shuleni na vyuoni! Madarasa ni machache, wanafunzi ni wengi! Mabwenini na hostels huko misongamano ipo ya kutosha! Je, wale watoa huduma (walimu) sehemu hizo wamekuwa sacrificed? Athari za Uviko-19 kwa watoto na vijana angalau ni ndogo japo haimaanishi hawaambukizwi. Badala yake hawa wanakuwa carrier au vector; wanaambukizana mashuleni na vyuoni jioni wanawapelekea wazazi nyumbani!
.... Ilitegemewa tangazo lingeelimisha jamii juu ya hili na namna ya kujikinga! Kwa mfano, wangesema wazazi epukeni kuwakumbatia watoto wenu watokapo shule na nyumbani mkae mbali nao maana ni hatari! Badala yake kimya!