#COVID19 Serikali: Kuanzia Julai 26, 2021 kila anayetumia usafiri wa umma avae barakoa

NDUGU ZANGU WAHANGAIKAJI TUNAOTEGEMEA KUTOKA NDIO TUPATE MAHITAJI YETU YA KILA SIKU, HAKIKA TUTAPOTEZA AJIRA NA MAZINGIRA YA BIASHARA YATAKUA MAGUMU SANA.
Tumeyataka wenyewe!! Pesa ya mabeberu pamoja na kwamba ni mkopo ambao utarudishwa na riba lakini wanakuwekea masharti hadi basi!! I'm very sorry for poor africans!!
 
Ulishawahi kutumia Public transport tangu hizi Porojo za Corona zianze?
 
Dah kweli ukila pesa za watu unakuwa kama zombie kila utakaloambiwa utafanya tu haki huyu mama Mungu anamuona anapotupeleka
 
Madhara ya kukiri udhaifu... Mbona tulikuwa tunaishi kawaida tu.. kwanini sasahivi?

Tunapeana hofu tu, korona ndio ipo ila naona kama tunatishana sana
 
Uganda mpaka walikua wanazika majeneza matupu ili kuonesha watu wanakufa sana,kumbe hakuna lolote.
Hichi kitu hakuna ni propaganda tu.
 
NDUGU ZANGU WAHANGAIKAJI TUNAOTEGEMEA KUTOKA NDIO TUPATE MAHITAJI YETU YA KILA SIKU, HAKIKA TUTAPOTEZA AJIRA NA MAZINGIRA YA BIASHARA YATAKUA MAGUMU SANA.
Mnaenda kupigwa lockdown muda sio mrefu
 
Atakumbukwa kwa kuwaachia watanzania wafe kama kuku wenye kideri bila kuchukuwa hatua mapema.mpaka yeye mwenyewe ikamuua.
Hoja yako hasa ipi maana kuhusu watu kufa hao wazungu wamekufa na wanaendelea kufa pamoja na kuchukua hatua, sasa huko kufa kama kuku ni kupi hebu eleza?
 
Unajua issue ya matumizi sahihi ya barakoa inapuuzwa kabisa, mkiulizwa wavaaji wa barakoa ni wangapi mnakumbuka kunawa mikono kabla ya kuvaa na kuvua barakoa ni wazi wachache tu huwa wanakumbuka hilo suala. Sasa kama watu wanashindwa kujua matumizi sahihi ya barakoa sijui ni vp barakoa itakuwa msaada wa kuzuia maambukizi? watu hawajui hata baada ya kuvua barakoa afanye nini
 
Umesahau nyumba za ibada, makanisa na misikiti.
 
Serikali kupitia msaada wa nje, washone barakoa wazigawe bure,ni rahisi ku implement kuliko kusisitiza disposable face mask, my opinion, I stand to be corrected
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…