Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Serikali imesema itasasimamia na kugharamia taratibu zote za mazishi ya Wanafunzi wanne wa Shule ya Msingi Kagera iliyopo Manispaa ya Kigoma Ujiji waliofariki kwa kuzama kwenye Mto baada ya mtumbwi kupinduka wakati wakielekea Shule.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye amesema hayo baada kufika kaika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma ya Maweni kuaga miili ya Wanafunzi wawili waliopatikana leo kadokando ya Mto huo unaomwaga maji katika Ziwa Tanganyika.
"Kwa niaba ya Serikali ya awamu ya sita naomba niwafikishie salamu za pole kwa msiba mkubwa uliozikumba Familia hizi, tumepokea kwa mshituko na masikitiko makubwa na tunaungana na Familia pamoja na Ndugu katika masikitiko haya makubwa tunajua hakuna mwenye uwezo wa kurejesha uhai uliotoweka ila tunaomba tuungane kwenye huzuni hii"
"Na serikali kwa upande wake itajitahidi kila inavyoweza ili kuwapumzisha kwa heshima Watoto wetu hawa ambao wamefariki, tutafanya tunavyoweza kuungana na Familia kuhudumia msiba ili tuweze kuwapumzisha wapendwa wetu vizuri, Serikali itaondoa changamoto hiyo kwa kutengeneza Daraja katika Mto huo"
Miili miwili iliyopatikana leo ya Wanafunzi hao ni mwili wa Tatu Sanaari na Ramadhani Nkwila(12) wa darasa la tano na wote wanazikwa leo, miili ambayo haijapatikana hadi sasa ni ya Watoto wawili Ashura Haruna wa darasa la kwanza na Zabibu, juhudi za utafutaji zinaendelea kufanywa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kutoka Kigoma.
Pia soma: Kigoma: Wanafunzi 4 wazama mto Luiche wakivuka kwenda shule. Miili 2 yapatikana kati ya watoto 4 waliozama