Serikali kuja na kifurushi cha gesi ya kupikia cha Sh 500 au 1,000 ili Mtanzania anunue gesi badala ya mkaa na kuni

Serikali kuja na kifurushi cha gesi ya kupikia cha Sh 500 au 1,000 ili Mtanzania anunue gesi badala ya mkaa na kuni

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Katika kuhamasisha matumizi ya gesi ya kupikia, serikali yetu itakuja na utaratibu wa kumruhusu mteja kuinunua gesi kwa bei ndogo kulingana na mahitaji yake.

Kwa sasa wengi wanashindwa kumudu kutokana na gharama kubwa zilizopo, hivyo mchakato wa kuzipunguza unaelekea mwishoni ili kulifanyia mapinduzi suala hilo.

Moja ya vikwazo kwa Watanzania kutumia gesi ni kwamba lazima uwe na fedha nyingi kwa mkupuo. Teknolojia inayoruhusu mtu kununua gesi ya Sh500 au Sh 1,000 ipo na inamwezesha mtu kununua gesi kama anavyonunua kopo la mkaa au fungu la kuni.

Kwa sasa gesi inayouzwa kwa mtungi wa kuanzia kilo sita, ni wastani wa Sh25,000 hivyo kuwa juu ya mahitaji ya baadhi ya wanaohitaji kiasi kidogo kwa matumizi yao au wasio na uwezo wa kifedha kumudu bei ya mtungi huo.

Teknolojia hiyo itakuwa mkombozi kwa Watanzania na itapunguza matumizi ya kuni na mkaa kupikia hasa kwa wananchi wa vijijini. Mazingira yetu yanafanana na India kwa kiasi kikubwa lakini wao asilimia 98 wanapika kwa kutumia gesi.

Kiuhalisia bei ya gesi ni rahisi kuliko mkaa na kuni, lakini wananchi wamezoea kununua kuni na mkaa katika vipande vidogovidogo ndio maana haionekani kuwaumiza wengi hivyo gesi inahitaji ubunifu wa kibiashara ili kuendana na uwezo na mahitaji ya Watanzania.

Chanzo: Mwananchi
 

Attachments

  • images (19).jpeg
    images (19).jpeg
    41 KB · Views: 34
Serikali ina mipango mingi Sana isiyokuwa na cohesion..

STAMICO na Jafo wanasema wamegindua mkaa rafiki wa mazingira serikali haifanyi kitu..

Makamba anasema anazindua gas ya kupima.sasa kipi hasa ni uelekeo wa serikali?
Vyote vina umuhimu boss, tunatakiwa kuchanganya vyanzo vya nishati lakini bila kuharibu misitu na miti yetu.
 
Serikali ina mipango mingi Sana isiyokuwa na cohesion..

STAMICO na Jafo wanasema wamegindua mkaa rafiki wa mazingira serikali haifanyi kitu..

Makamba anasema anazindua gas ya kupima.sasa kipi hasa ni uelekeo wa serikali?
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Suleiman Jafo amelitaka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kuongeza uzalishaji na usambazaji wa mkaa mbadala unaotokana na makaa ya mawe ili kuokoa mazingira.

Soma hapo kwa umakini ili upate kujua ni mkaa wa namna gani unazungumziwa hapo.

Na lengo la kutumia huo mkaa mbadala na kifurushi cha gesi ya kupikia ni ili kuokoa mazingira yetu.
 
Back
Top Bottom