Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 7,899
- 10,415
Katika kuhamasisha matumizi ya gesi ya kupikia, serikali yetu itakuja na utaratibu wa kumruhusu mteja kuinunua gesi kwa bei ndogo kulingana na mahitaji yake.
Kwa sasa wengi wanashindwa kumudu kutokana na gharama kubwa zilizopo, hivyo mchakato wa kuzipunguza unaelekea mwishoni ili kulifanyia mapinduzi suala hilo.
Moja ya vikwazo kwa Watanzania kutumia gesi ni kwamba lazima uwe na fedha nyingi kwa mkupuo. Teknolojia inayoruhusu mtu kununua gesi ya Sh500 au Sh 1,000 ipo na inamwezesha mtu kununua gesi kama anavyonunua kopo la mkaa au fungu la kuni.
Kwa sasa gesi inayouzwa kwa mtungi wa kuanzia kilo sita, ni wastani wa Sh25,000 hivyo kuwa juu ya mahitaji ya baadhi ya wanaohitaji kiasi kidogo kwa matumizi yao au wasio na uwezo wa kifedha kumudu bei ya mtungi huo.
Teknolojia hiyo itakuwa mkombozi kwa Watanzania na itapunguza matumizi ya kuni na mkaa kupikia hasa kwa wananchi wa vijijini. Mazingira yetu yanafanana na India kwa kiasi kikubwa lakini wao asilimia 98 wanapika kwa kutumia gesi.
Kiuhalisia bei ya gesi ni rahisi kuliko mkaa na kuni, lakini wananchi wamezoea kununua kuni na mkaa katika vipande vidogovidogo ndio maana haionekani kuwaumiza wengi hivyo gesi inahitaji ubunifu wa kibiashara ili kuendana na uwezo na mahitaji ya Watanzania.
Chanzo: Mwananchi