Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Msajili wa Hazina Mheshimiwa Nehemia Mchechu, amesema ya kuwa wapo katika hatua za Mwisho katika kukamilisha mfumo maalumu utakaosaidia na kuiwezesha mamlaka ya uteuzi kufanya maamuzi sahihi katika uteuzi wa viongozi mbalimbali wa mashirika na taasisi za Umma.
Ameyasema hayo katika uwasilishaji wa Gawio na michango kutoka katika mashirika na taasisi mbalimbali za umma mbele ya Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.
Amesema kuwa mfumo huo utakuwa na kazi na wajibu au jukumu la kutoa taarifa za kiutendaji kwa kila kiongozi kwa usahihi,kwa uaminifu na kwa wakati kwa mamlaka za uteuzi, Ili kusaidia mamlaka ya uteuzi kufanya maamuzi sahihi.
Akatolea mfano kuwa kuna wakati kuna kiongozi aliondolewa katika nafasi yake na baadaye kurudishwa tena baada ya Mwenyekiti wake kutoa maelezo mazuri yaliyoonesha kuwa mhusika alikuwa amefanya kazi nzuri katika nafasi yake.
Mheshimiwa Nehemia Mchechu ameomba radhi Kwa Mheshimiwa Rais kuwa wao kama hazina walimuangusha Mheshimiwa Rais, na ndio maana wameamua kujisahihisha kwa kuja na mfumo huo utakao kuwa muarobaini na msaada kwa mamlaka ya uteuzi kufanya uteuzi na maamuzi sahihi ,kwa kuangalia na kusoma taarifa zenye ukweli na usahihi juu ya utendaji kazi wa viongozi mbalimbali wa taasisi na mashirika ya umma.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa. Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.