Serikali Kuja na Mfumo Maalumu wa Kusaidia mamlaka ya Uteuzi kufanya uteuzi kwa Usahihi

Kuna utaratibu unafanyika kabla ya kufanya uteuzi wa Mwisho.ikiwa ni pamoja na kupitia wasifu wa mhusika na uwezo wake wa kiuongozi na historia yake ya kiutumishi na kiutendaji katika maeneo ambayo amewahi kufanya kazi
Achana na huo upuuzi watu waombe washindanishwe Kwa CV na interview

Sema utaratibu umeshaanza kwenye kuchagua wakurugenzi wa bodi Sasa hivi zinatangazwa na interview zonafanyika inaonyesha uko nyuma ya wakati Iko outdated wanachoongelea ni ku extend mchakakato watu waombe waweke CV wafanye Interview wapewe post badala ya kuteua tu waimba kwaya za kusifu na kuabudu anayeteua ambao hamna kitu kichwani zaidi ya nyimbo za kusifu na kuabudu Kiongozi mteuaji

Kwa wakurugenzi wa bodi tayari mchakato ulishakamilika Bado hayo maeneo mengine yanakuja
 
Utasimamiwa na watanzania wazalendo ambao watawajibika kutoa taarifa za ukweli,sahihi na kwa uaminifu mkubwa sana kwa mamlaka ya uteuzi.
Mungu ajalie wawepo hao watu, ila mi nimekata tamaa na watanzania. Wabinafsi sana kiasi wanatesa watanzania wenzao maskini.
 
Umesahau kuweka namba ya simu
 
Mungu ajalie wawepo hao watu, ila mi nimekata tamaa na watanzania. Wabinafsi sana kiasi wanatesa watanzania wenzao maskini.
Ni dhambi kukata tamaa .naomba usikate tamaa bali uwe na imani na matumaini makubwa sana kwa Mheshimiwa Rais na serikali yake
 
Mfumo sahihi ni kuondoa jukumu la uteuzi kwa Rais.
Badala yake nafasi zitangazwe watu wachuane kupata nafasi!
 
Duniani kwote zipo nafasi ambazo ni lazima zifanyiwe uteuzi na Rais.
Hilo sijakataa... Duniani huko wanafanya vizuri zaidi kuliko huko ccm.
Duniani inapobidi Rais kuteua still bado kuna mamlaka nyingine inawachuja!
 
Mifumo ya kujipendekeza kwa rais haiwezi kuwa na tija yoyote, zaidi ya kuwatafutia makada wa ccm ulaji wakiukosa mahali pengine. Kama hii iliyopo haina tija, huo mwingine utapata wapi tija zaidi ya kuongezea wananchi mzigo Ili kuwalipa Wala kodi?
 
MaRC,MaDc na Maded pia huu mfumo ungesaidia kuwapata .
Mfumo wa sasa ni janga la Taifa
 
Hahaha ha!....hebu kwenda huko!
 
I strongly recommend that any transformation starts with articulating organisation’s vision, mission, and core values. Once that’s done, Boards should map out a strategic roadmap that outlines specific milestones, timelines, and success metrics. With this foundation, Government entities and parastatals will have a unified purpose that fuels their efforts and keeps them on successful track hence contributes heavily in our treasury and sustainable development .
 
CCM hawajawahi kufanya kitu cha maana zaidi ya kuiba kura, na kulazimisha kutawala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…