Serikali kujenga vituo 3 vya michezo

Serikali kujenga vituo 3 vya michezo

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2020
Posts
9,034
Reaction score
6,913
Hii ni mpya.

Serikali imesema itajenga vituo 3 vya michezo kwenye mikoa ya Geita, Dodoma na Dar es Salaam ambapo kila kituo kitagharimu bil.3.

Aidha Serikali itajenga kituo cha umahili wa michezo kwenye chuo cha michezo Malya kitakachoghadia kiasi cha 1.5 bln.

Binafsi sina tatizo na vituo hivyo ila nina tatizo na malengo ya hivyo vituo ni yapi.

Nachojua sports centre ni complex ambayo inatakiwa kuwa na facilities na viwanja vya michezo aina zote tena vyenye ubora kuanzia viwanja vya mpira wa miguu,kuogelea hadi golf na tennis.

Sasa unajiuliza bil.3 ndio zitafanya hayo yote? Huu ni utani na upotezaji wa fedha za walipa kodi.Vipaji gani vitakuzwa kwa staili hii?

Ni afadhari kujenga complex zenye hadhi kila Kanda na hizo pesa zingewekwa kwenye kituo kimoja Ili kuwe na tija badala ya kutapanya afu mwisho wa siku hakuna kitakachofanyika.

Serikali itazame upya mpango wake huu,mbaya zaidi wameenda kujenga kwenye mikoa ambayo hata haina uzito kwenye michezo.Geita na Dodoma michezo wapi na wapi?
 
Ni maamuzi yenye utashi wa kisiasa zaidi kuliko wa kimichezo

Ati Geita😂😂 kama mwendakuzimu angekuwa hai wangesema Chattletown kabisa
Sasa hapa tunapoteza pesa kwa nn hawa wapuuzi wa huko Serikalini wanafanya mambo ya kijinga? Kuna wadau wa michezo ,tff nk Kwa nini wasiwaulize au wasijifunze kwa wengine?

Hizi akili sijui huwa wanazitoa wapi Hawa watu
 
Binafsi napenda serikali ishirikiane na tff wajenge sports complex za maana za michezo kwa ajili ya michezo mbalimbali Ili si TU zitumike kukuza vipaji bali ziweze kuja kutumika kuandaa mashindano mbalimbali ya Africa kama all African games,afcon nk sio upuuzi wanaotaka kufanya huo.
 
Kigoma wameiachaje?
Swala sio mkoa gani kujengwa bali complexity ya facility husika,sasa bil.3 si ni kiwanja tuu cha mpira cha kawaida hapo ndio sports complex ya kuendelea vipaji?

Hii nchi haijielewi kabisa inachofanya,hamuoni aibu ya kuambulia patupu kila mwaka kwenye mashindano ya kimataifa?
 
Back
Top Bottom