Serikali: Kuna kundi kubwa la watoto wenye jinsia mbili, lakini wanafichwa na wazazi na kushindwa kupatiwa matibabu

Serikali: Kuna kundi kubwa la watoto wenye jinsia mbili, lakini wanafichwa na wazazi na kushindwa kupatiwa matibabu

Shida ni kuwa ukimuacha akakua akaja kuchagua mwenyewe akibalehe ni kwamba kama alilelewa kama wakike halafu akikua achague kuwa wa kiume huoni hapo ndipo jamii itataharuki?na unyanyapaa utaanzia hapohapo,ni bora atambuliwe mapema ili aishi na alelewe kufuatana na jinsia yake.
alelewe kwa jinsia gani wakati anazo mbili mkuu ?
 
Na nyie watu wa maabara mmejuaje kama ni Kundi kubwa?mmefanya utafiti au kwa sababu mmeletewa kesi mbili tatu kwenu mmeamua kuropoka?

Uwasilishaji ujumbe kwa kiswahili kimempiga chenga.

Pengine angesema kuwa Katika Watoto Wanaozalia Wenye Jinsia Zote Mbili, Idadi Yao Kubwa Hufichwa.

Kichwa hiki cha habari cha uzi huu kinaashiria hata hapa Jamiiforums wengi wamezaliwa wakiwa na jinsia zote mbili na tumefichwa.
 
Wakizaliwa hospitali basi wawafanyie uparesheni ya mapema ili ibaki wanatoitaka hata hivyo litakua zoezi gumu kugundua ni jinsia ipi iliyokusudiwa wakati wa uumbaji.
 
Wasomi, msaada tutani; mwana baiolojia si lazima awe daktari sio?

Hakuna jinsi ya kuwaacha mpaka wakaja kuchagua wenyewe, tena baada ya balehe? Sawa, kwamba kitaalamu watathibitisha kuwa jinsi inayotawala ni x, ila kwa huku kwetu, ni bora ikajithibitisha yenyewe kuliko kupasuliwa kichwa ilhali ugonjwa uko gotini.
Unamlea kiume akakua anataka kuwa demu utafanyaje hapo bora wamrekebishe mapema hakuna aliyewahi chagua jinsi.

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Kuna familia ilikuwa na wadada sita wazuri hatari ila wanajinsia mbili duh na waligoma kutoa matokeo wamezeeka na uzuri wao.
Wapi hiyo? Mzazi unapata mtoto kwanza, wa pili bila kujiuliza mpaka sita? Hapana huo no uzembe kiwango cha lami.

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Kwa kuwa watoto wengi wanazaliwa hospitali, ingetengenezwa sheria kwamba ikitokea mtoto kazaliwa na jinsia mbili awekwe chini ya uangalizi maalumu kama ilivyo kwa watoto njiti.
Hii itasaidia sana .
 
Nilisoma na mmoja wao O-level tulikuwa nae bweni moja...baadae kipindi namaliza kidato cha 4 ndio nikaanza kuambia huyu mtu ana jinsia mbili...nilivyoenda kutembelea huko kwa hivi karibu nikamkuta ni mwanamke ila ndo hawa ma tomboy aise!! Nilipagawa
 
Sasa nyeti zao zinakaa wapi kati ama
Niliwahi kumuona mtoto mmoja alikuwa na miezi kama minne pale kwa juu inaanza uke kwa chini unakuja uume na pumb. inakuwa ndogo sana kuiona mpaka uichungulie Sana.Mama mtu alikuwa hana hata hela ya kula lakini madaktari wa wilayani walikuwa wanamuambia aende hospitali kubwa ya rufaa.

Alishindwa akawa anapita mitaani kuomba msaada.Wengi siyo wanawaficha ila hawana fedha za kwenda hospitali,hasa wanaotoka vijijini.
 
Back
Top Bottom