Serikali: Kuna ongezeko la watu wenye homa, kukohoa, mafua, maumivu ya mwili

Dah imenipiga wiki nzima sema nimepona sasa maana sio poa.
 
Limeongezeka wimbi la Mafua makali hv karibuni. Mzigo Kama umerudi au ndo mambo ya vita?
Ukiumwa wewe na washikaji kadhaa dhaifu usihisi ni kila mtu anapata hizo tabu
 
Aisee.. watu wanahofia mafua
Hata mimi zamani nilikuwa mjinga kama wewe sikuelewa flue ni nini na kwa nini flue inawasumbuwa sana wazungu.

Mjinga yeyote anapaswa kuelimishwa, ni kwamba mafuwa au flu huwa yanaleta homa kali na uchovu pia, ni bora hata ya maralia.
 
Hata mimi namshukuru sana MUUMBA kwa kunipa Afya iliyo bora na njema pia.

Kwa kweli sikumbuki mara ya mwisho ni lini nilipata homa, na huwa sina kawaida ya kusumbuliwa na Mafua, au hata viungo kuuma.

Asikudanganye mtu Mazoezi ni dawa tosha.

Asilimia kubwa ya Maisha yangu ni Mazoezi
 
Kwahiyo wewe unafanya mazoezi kumzidi marehemu Mac vivian foe?
 
Na si kila mtu anaweza kuambukizwa ukimwi hili ulijuwe pia.
Nasikia ni wachache sana.
Ila hili la kuona au kuambizana mitaani, makazi au popote na ukakuta unachokiumwa wewe nao wanaumwa tuache kuleta mastory ya ajabu

Miwatu mingi siku hizi ni nyoronyoro tu yani tunatembea na maradhi ukipitiwa kavumbi tu shida, ukinywa maji ambayo hayajachemshwa utahara hadi kesho kutwa n.k sasa hii si kila mtu inampata watu strong ni wengi mno
 
Kwa miaka mitatu mfululizo hili tatizo lipo, halina uhusiano na unachokiamini.

Ni kama tetekuwanga ikiingia kwenye itawapata wote lakini utakuta mtu mwingine haimpati, hakuna swala la mazoezi hapo.
 
Limeongezeka wimbi la Mafua makali hv karibuni. Mzigo Kama umerudi au ndo mambo ya vita?
Yote hiyo ni madhara ya vita ya urusi na ukraine. Hivyo Mwili unajiweka sawa kukabiliana na ongezeko la bei.

Leo tu ewura watapandisha bei ya petrol hadi 3500 kwa lita. Mbona mtakufa mmesimama
 
Kwahiyo wewe unafanya mazoezi kumzidi marehemu Mac vivian foe?
Utanishindanisha vipi na Mtu ambae alishafariki!

Nimezungumzia mimi kama mimi, sijazungumza kwa niaba ya Foe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…