Kamwe sukari isiwe mojawapo.wa bidhaa ambayo inabidi.itoke.nje ndio bei iwe.ndogo.
Huo ni ukiritimba wa mawazo .
Kwa hiyo unataka kutuaminisha kwamba viwanda vyetu vimezalisha sukari ya kutosha wafanyabiasha tu Kwa tamaa yao wameamua kupandisha bei ili wapate faida.
Wakati viwandani sukari ipo ya kutosha
Ukiritimba wa mawazo ni kusema serikali ndiyo inajua kila kitu, kila bidhaa lazima tuzalishe sisi. Ni kuacha kutumia mazuri ya free-market.
Kwenye uchumi kuna kitu kinaitwa "competitive advantage". Kama hatuna competitive advantage kwenye kitu, tuagize kutoka nje tu if it makes economic sense.
Utafanya protectionism kwenye sukari mpaka lini wakati viwanda havikui na wafanyabiashara wa sukari wanatumia fursa hiyo kupandisha bei na kupiga hela tu?
Ukiritimba ni the opposite of free-market. Wewe ndiye unahubiri ukiritimba kwa kukataa free-market.
Wafanyabiashara hawazalishi sukari ya kutosha makusudi ili sukari iwe chache.
Sukari ikiwa chache bei inapanda juu, kwa hivyo wafanyabiashara wanaweza kutengeneza faida ile ile au kubwa zaidi kwa kuzalisha sukari chache ukilinganisha na kuzalisha sukari nyingi. Kwa kucheza na bei tu.
Kwa mfano.
Ikiwa unazalisha kilo 50 za sukari, na kilo ni shilingi 6,000, hapo unapata shilingi 300,000.
Sasa, ukijua kwamba ukizalisha kilo 100, bei itashuka mpaka shilingi 3,000 (more supply, fall in price per laws of demand and supply ceteris paribus), ambayo itakurudisha kwenye mapato yaleyale ya shilingi 300,000, kwa nini uzalishe kilo 100 wakati unaweza kuzalisha kilo 50 na kupata mapato yaleyale ya kilo 100 kwa kuzidisha bei tu?
Ndicho wanachofanya wafanyabishara wa sukari.
Dawa yao ni kuruhusu sukari ya nje, itakayokuja kuuzwa kwa shilingi 3,000.
Watu wakizoea kununua sukari ya nje kwa shilingi 3,000, wafanyabiashara wa ndani nao watalazimika kuuza sukari yao kwa shilingi 3,000, bila kujali wamezalisha kilo 50 au 100.
*Bei na namba ni za kufikirika tu zimetumika kwa mfano, hazina uhalisi kabisa zaidi ya kuonesha mfano.