Hatua gani!?..kupeleka miswada maana yake kishaandaa,hawatishi
Kama kaandaa muswada hadi kuupeleka bungeni sijui mwezi wa sita, kuna muda zaidi ya miezi mitatu ambayo inatosha kabisa kuwa compromised.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hatua gani!?..kupeleka miswada maana yake kishaandaa,hawatishi
Mbona. Uko negative, una shida gani!?kama kaandaa muswada hadi kuupelekwa bungeni sijui mwezi wa sita, kuna muda zaidi ya miezi mitatu ambayo inatosha kabisa kuwa compromised
Kunaweza kuwa na ka ukweli hapa, kwamba Big Boys asiyekuwepo anatwishwa gunia la misumari kumbe mchawi dola, hakuna dolare za kuagiza sukari nje!Asitafutwe mchawi, ni sera mbovu za serikali ya CCM katika masuala ya kiuchumi na kibiashara. Asitishie kivuli cha ruhani asiyekuwepo ambaye amebatizwa jina la kiruhani Big Boys, CCM itazidi kuaibika
Anasema anapeleka muswada bungeni kuruhusu sukari ya nje kwenye soko.
Sasa, wewe huna haki ya kumtuhumu hilo unalomtuhumu mpaka akishindwa kupeleka huo muswada bungeni.
Mfanyie haki ya kumpa muda kwanza akosee, ashindwe anachosema atafanya, akikosea, akishindwa, hapo utakuwa na haki ya kumsakama na kusema alitaka kidau kipande tu.
Ukimsakama kabla hajapeleka muswada bungeni, utakuwa unafanya tabia zenu za kulalamika kishamba tu kwa conspiracy theories bila ushahidi wala mantiki.
Wewe una tatizo la bei ya sukari. Waziri kakwambia anatatua hilo tatizo kwa kuruhusu sukari kutoka nje. Kakupa na muda maalum wa kutatua hilo tatizo, kwamba atapeleka muswada wa kubadili sheria kwenye bunge la bajeti.
Kwa nini hungojei hilo bunge la bajeti uone kitakachotokea?
Kwa nini unapenda kulalamika kwa conspiracy theories wakati jibu la uhakika utalipata kwenye bunge la bajeti?
Magufuli alikuwa mshamba asiyeelewa uchumi na hiyo solution yake ilikuwa ya kishamba. Huyu ndiye aliyeingusha biashara ya korosho akaiharibu, alitaka wanajeshi wabangue korosho hata kwa meno. Ujinga mtupu.Magafuli anaingi madarakani situation kama hii ilitokea, hatua aliyochukua ni pamoja na msako kwa wanaoficha sukari. Yeye anashindwa nn kuchukua hio hatua wakt akisubir hilo la bunge
Kabisa kama taifa limeshindwa kufanya biashara fulani waachie wengine wafanye kwa manufaa ya wananchi. Wao wanachojua ni kuvizia tu pale festoni na TRA wao na kukamata watu na bidhaa za nchi jirani hawajiulizi ni kwa nini wananchi wananunua hizo bidhaa ilihali na sisi tunazo.Wakafie mbele huko. Kama ni syndicate ya kututesa wananchi kwa kulangua sukari acha ife tu. Tunduma sukari ni 2500/- lakini ukifika Mbeya mjini ni 4800. Kwa nini watu wateseke? Wafungue mipaka sukari ya Zambia na Malawi ije kwa wingi bei zishuke.
Na kwa kuwa ameshasema hadharani ni lazima aliyoyasema yaonekane yametendeka !Kwahiyo anasema hadharani hayo ili kuwatisha wenye viwanda ili wamwone au waongeze dau, kwa maana ya kwann asichukue hatua at first place ili wakilalamika yy ndiyo aje na haya majibu?
Hapo sasa !!Ushawahi sikia kauli ya Serikali Ina mkono mrefu? Kwani siku hizi mkono umefupika Hadi isiwajue waficha sukari?
Ngoja Tusubiri tuone. !!Hafiki May mosi akiwa Waziri wa Kilimo
Amesema mtalima mpunga badala ya miwa !Je sisi wakulima tinaolima miwa tutafanya kazi gani? Sii tutaingia kwenye umaskini?
Aha hahahaUdikteta unasaidia sana.. ila watu hawajui tu
Ni kama ishu ya MADARASA watu wanavyokimbizana dakika za lala salama !!Hayo huwa hawaforecast na kuyaona mapema ili wadhibiti kabla ya usumbufu.
Hii biashara Abduli yupo ndaniNgoja Tusubiri tuone. !!
makampuni mengi nchi hii ni makanjanja, hawana hata aibu. Wanaihujumu serikali, hawabebeki. Acha soko huria ifanye kazi. Ndio maana matajiri wa nchi hii wanachukiwa sana na wananchi na walifurahia kipindi MAgu anawashughulikia. Hawana utu wala ubinadamu. Sijui ni kwa kuwa utajiri wao mwingi ni wa shirki? Wana roho mbaya kuliko shetani, ndio maana Magu aliwaambia wataishi km mashetani. Wanajilimbikizia mali ya dhuluma wakati wanaziacha hapa duniani. Washenzi kabisa, wafungiwe hizo biashara zao nao waje kuishi km mashetaniWaziri Bashe akiwa Ikulu, Dar ameongelea sakata la sukari nchini.
Bashe: Wafanyabiashara wana option mbili tu, waache kuuza sukari, Serikali itatafuta option nyingine. Wenye viwanda wana option mbili, wafate utaratibu wa Serikali au waache hii kazi.
Serikali haiwezi kuruhusu, tumewaprotect vya kutosha kama nchi lakini kwa uwezo wa mwenyezi Mungu mwezi wa sita kwenye Bunge la bajeti kama waziri mwenye dhamana ninapeleka mabadiliko ya sheria kwaajili ya ku libelarize biashara ya sukari, wata- compete na competing companies kutoka nje na wenyewe watapata incentives zilizo ndani ili kuwaprotect.
Hatuwezi kuendelea na irresponsible private sector kwenye nchi kwa hali hii inayoendelea. Wakulima wa miwa wako 12,500 nchini, tutasota mwaka mmoja, mabonde yale tutayageuza ya mpunga, there is no problem.. zipo nchi ambazo zimeacha kulima sukari.
Kwa umeme huu watashindana vipi bila kuwabeba labda waambiwe wafunge viwanda! Au serikali ipunguze makodi tuu!Si kwamba waziri anataka kuiua sekta fulani.
Waziri anawaambia watu wa kwenye hiyo sekta waache kupenda kubebwa na protectionism, ni muda kwa kushindana na bei ya sukari kutoka nje.
Waliosoma uchumi wanajua kitu kinaitwa "competitive advantage".
Anachosema Bashe ni kwamba, kama Tanzania hatuna competitive advantage katika sukari, sukari yetu ina gharama ya juu zaidi kuizalisha, tuseme labda tunazalisha kilo moja kwa shilingi 6,000, wakati wenzetu wanaweza kuzalisha kilo hiyo kwa shilingi 3,000, hapo labda inawezekana ikawa busara kuacha kuzalisha sukari, tuagize ya nje, na hiyo ardhi ya kulima sukari tulime mpunga.
Hapo hatuna "competitive advantage" katika kutengeneza sukari.
Kauli hii pia inaweza kuwa silaha ya kisiasa, kwa mfano, ikiwa waziri anajua kuwa wafanyabiashara wa sukari wanapandisha bei kwa hila, na wanaweza kabisa kupunguza bei ikawa sawa na ile ya sukari kutoka nje ya shilingi 3,000 , kwa kupunguza gharama za uzalishaji na kuondoa upandishaji bei wa kiholela wa kutafuta faida tu, kauli hii inaweza kutumika kulazimisha wadau wa sekta ya sukari kupunguza bei.
Bei ya sukari Tanzania haipo juu naturally, ipo juu artificially. Ndiyo maana sukari ya nchi jirani kama Malawi bei yake iko chini zaidi.
Serikali inafanya kitu sahihi kuruhusu sukari ya nje ije kushindana na ya ndani kwenye soko.
Hili jambo lilitakiwa kufanyika zamani sana. Naona kama wamechelewa.
Ame admit kuna 'monopoly'.
Ni hatari.
Kweli usalama wa nchi unaweza kua vibindoni mwa watu wachache. Duh
Well iko hivi kwa muda mrefu, just tu imefumbiwa macho, ila wafanya biashara wanalifahamu hiliAme admit kuna 'monopoly'.
Ni hatari.
Kweli usalama wa nchi unaweza kua vibindoni mwa watu wachache. Duh