Serikali kuondoa udhibiti wa sukari kutoka nje kisheria. Bashe adai anaenda kuwatikisa 'Big Boys'

Hii nchi inahitaji dikteta kamili na sio dikteta uchwara kama alivyokuwa magufuli.Wala uhaba wa sukari haipo nchi hii isipokuwa watu wanajua nchi haina uongozi.
 
Kamwe sukari isiwe mojawapo.wa bidhaa ambayo inabidi.itoke.nje ndio bei iwe.ndogo.
Huo ni ukiritimba wa mawazo .
Kwa hiyo unataka kutuaminisha kwamba viwanda vyetu vimezalisha sukari ya kutosha wafanyabiasha tu Kwa tamaa yao wameamua kupandisha bei ili wapate faida.
Wakati viwandani sukari ipo ya kutosha
 
huu mchakamchaka ni wa nguvu

chadema hawapendi mamuzi ya tija kama haya watapinga
 
Ukiritimba wa mawazo ni kusema serikali ndiyo inajua kila kitu, kila bidhaa lazima tuzalishe sisi. Ni kuacha kutumia mazuri ya free-market.

Kwenye uchumi kuna kitu kinaitwa "competitive advantage". Kama hatuna competitive advantage kwenye kitu, tuagize kutoka nje tu if it makes economic sense.

Utafanya protectionism kwenye sukari mpaka lini wakati viwanda havikui na wafanyabiashara wa sukari wanatumia fursa hiyo kupandisha bei na kupiga hela tu?

Ukiritimba ni the opposite of free-market. Wewe ndiye unahubiri ukiritimba kwa kukataa free-market.

Wafanyabiashara hawazalishi sukari ya kutosha makusudi ili sukari iwe chache.

Sukari ikiwa chache bei inapanda juu, kwa hivyo wafanyabiashara wanaweza kutengeneza faida ile ile au kubwa zaidi kwa kuzalisha sukari chache ukilinganisha na kuzalisha sukari nyingi. Kwa kucheza na bei tu.

Kwa mfano.

Ikiwa unazalisha kilo 50 za sukari, na kilo ni shilingi 6,000, hapo unapata shilingi 300,000.

Sasa, ukijua kwamba ukizalisha kilo 100, bei itashuka mpaka shilingi 3,000 (more supply, fall in price per laws of demand and supply ceteris paribus), ambayo itakurudisha kwenye mapato yaleyale ya shilingi 300,000, kwa nini uzalishe kilo 100 wakati unaweza kuzalisha kilo 50 na kupata mapato yaleyale ya kilo 100 kwa kuzidisha bei tu?

Ndicho wanachofanya wafanyabishara wa sukari.

Dawa yao ni kuruhusu sukari ya nje, itakayokuja kuuzwa kwa shilingi 3,000.

Watu wakizoea kununua sukari ya nje kwa shilingi 3,000, wafanyabiashara wa ndani nao watalazimika kuuza sukari yao kwa shilingi 3,000, bila kujali wamezalisha kilo 50 au 100.

*Bei na namba ni za kufikirika tu zimetumika kwa mfano, hazina uhalisi kabisa zaidi ya kuonesha mfano.
 
Muda utasema!
Kuna muda natamani kuhamia Zambia, huko hakuna ushetani wa kutesa raia
 
Hapa nchini viwanda vyote vya sukari vinamilikiwa na wahindi ndio maana inakua rahisi kufanya kichezo mibaya….kagera sugar na mtibwa mmiliki mmoja…na tuna viwanda vinne tu hapa nchini kama sikosei!
 
Tuwe tu Wakweli Maandamano ya Chadema yamechangia pakubwa Waziri wa Kilimo mh Bashe kuwafokea Big Boys wa Sukari na kutengua ile sheria ya kuimport sugar

Kama unawajua Big Boys wa Sukari basi utakuwa umenielewa vizuri

Kwaresma Njema 😀🔥
 
Wenye viwanda vya sukari ndio wanunuzi wakubwa wa vibari vya kuagiza sukari kipitia makampuni ya watu wengine..50 Million to 100M.

Syndicate kubwa
 
Acha yampate kipindi magu anapambana na hawa matycon yeye alikuwa anabwabwaja kuwa tunaua private sector..mbora amejua leo tuna irresponsible private sector but its top late
 
Kama watu wanaficha sukari..serikali ifanyeje? Wacha watu washindane. Tunapenda kutake advantage ya udhaifu wa mifumo yetu na kuumizana.
Hata mafuta inabidi tufilke tu huko maana uhuni ni mwingi sana
 
Morogoro kuna viwanda kma vi 3 hiv ila sukari hakuna na ukiipata iko juuu sana kweli halafu BASHE AKAUJA KUONGEA NGOJERA ZAKE WAKATI BBT IMEMSHINDA RUZUKU YA MBOLEA IMEMSHIDA HAKUNA KAMPUNI YENYE MBOLEA SSA JE HUYU MRU KWELI NI WA KUMUAMIN KWELI? HAPANA
 
Kuliko haya mateso tunayopitia watanzania ni Bora tuagizege sukari kutoka nje mbona wese tunaagiza miaka yote na tunadunda tu. Kuliko huu ukiritimba wa viwanda vya sukari unaofanya mara mia tuagizege tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…