Serikali kupitia taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mwanza katika kipindi cha Oktoba hadi Disemba 2024 imefanikiwa kufuatilia

Serikali kupitia taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mwanza katika kipindi cha Oktoba hadi Disemba 2024 imefanikiwa kufuatilia

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Serikali kupitia taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mwanza katika kipindi cha Oktoba hadi Disemba 2024 imefanikiwa kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo 13 yenye thamani ya zaidi ya sh. Bil 4.4 kwenye sekta ya Elimu, Barabara na Biashara ambapo kati ya hiyo, miradi 12 yenye thamani ya shilingi bilioni 3.9 imekutwa na mapungufu.

Ufuatiliaji huo wa TAKUKURU umesaidia utekelezaji wa mapendekezo kwa zaidi ya asilimia 65.2 na kupelekea miradi hiyo kuwa na ubora kwa kiwango kilichokusudiwa.

Kwa upande mwingine, katika kipindi hicho, TAKUKURU mkoani Mwanza imefanikiwa kudhibiti kiasi cha milioni 366 katika eneo la ukusanyaji wa kodi ya zuio TRA pamoja na eneo la mnada wa mifugo Wilaya ya Misungwi.

 
Back
Top Bottom